Aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, na Mbunge wa Ruangwa Mhe. Kasimu Majaliwa, amechaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk John Magufuli amempendekeza Mhe Kasim Majaliwa kuwa Waziri
Mkuu wa 11 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kasimu Mjaliwa ambaye ni mbunge wa
Ruangwa amepigiwa kura na kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu muda mfupi uliopita na wabunge wa bunge la 11. Mhe Majaliwa aliwahi kuwa Naibu waziri wa Tamisemi (Elimu) katika Serikali ya awamu ya nne ya Mhe Dk Jakaya Kikwete.
Kitaaluma Mhe Majaliwa ni mwalimu, hivyo
kufanya Serikali ya awamu ya 5 kuongozwa na viongozi wengi ambao kwa taaluma
wamewahi kuwa waalimu.
Jina la Mhe. Majaliwa liliwasilishwa kwa ‘style’ ya aina yake ambayo haijawahi kutokea na
kuonekana katika Serikali nne zilizopita.
Wakizungumza nje ya uwanja wa
Bunge, wabunge wa Bunge hilo la 11 wamesema kuwa tukio hilo ni la aina
yake na la kihistoria kwa kuwa halijawahi kufanyika.Wamesema kwa nyakati tofauti kuwa
kitendo cha jina la Mhe Kasimu Majaliwa kuwasilishwa na mpambe wa karibu
wa Rais(CB) ADC ni historia na kuonyesha kuwa ni jinsi gani suala hilo
lilivyopewa uzito wa kipekee na Mhe Rais