MHE. EDWARD LOWASA ALIPOWASILI MKOANI MWANZA
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha wageni VIP baada ya kuwasili leo Jijini Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha .
Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege .
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege .
Shekh Hassan Kabete wa JASUTA
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa.
Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza naye alikuwepo kumpokea .
Mzee maarufu na Kada wa CCM wa siku nyingi Ally Zagamba akisalimiana na rafiki yake Mhe.Lowassa
Mwanahabari na Mdau wa Blog ya G. Sengo Peter K. Fabian akisalimiana na Mhe. Lowassa.
Umati wa wanawake wa dini ya kisilam waliokuwa wamejipanga nje ya VIP kusalimiana na Mhe.Lowassa
Mama maarufu wa Jijiji Mwanza Mama Magige akiteta jambo na Mhe. Lowassa baada ya kusalimiana naye.
Moja ya wanawake wa kisilam ambaye ni kiongozi akisalimiana na Mhe. Lowassa
Wanawake waliojitokeza kumpokea Mhe. Lowassa |
WAZIRI
Mkuu mstaafu Edward Lowassa tarehe 05/06/2013 amelitikisa Jiji la Mwanza baada ya
mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha pikipiki (Bodaboda) kujitokeza
kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini
kati.
Mapokezi
hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya dini,wamachinga ambao
ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza
kufunika mapokezi ya awali ya leo asubuhi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili
Jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta
ndogo ya Pamba unaofanyika jijini hapa.
Baadhi
ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa serikali na
Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini walifurika kwa mamia
kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka
uwanja wandege wakimshangilia huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na
pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba msafara huo.
Waziri
mkuu mstaafu huyo leo anataraji
kushiriki harambee ya kuchangia kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili
kusaidia kuongeza usikivu wa matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha
katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia
majira ya saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja
wa Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika ukumbi wa
New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.
Mheshimiwa
Lowassa
katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge
wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyabiashara,
Taasisi na
makampuni ili kufanikisha adhma na lengo lililokusudiwa kutokana na
ushawishi
alionao na kwa muonekano wa mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege
imeonyesha Mhe. Lowassa ni kipenzi cha watu na bado ananguvu ya
kukubalika kwa wananchi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo cha radio IQRA
ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe
Hassan Kabete alisema maandalizi tayari yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa
na kuwasili kwa mgeni rasmi Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani
Arusha.
“Tunayo
matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji kukusanya kwenye
harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400, ambapo tayari mfuko wetu
umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni 190 hivyo tunataraji lengo
litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh Kabete
No comments:
Post a Comment