Tuesday, May 19, 2015



Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi leo alihutubia wananchi wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano huko mkoani Dodoma ambapo aliitaka Tanzania kuwa karibu kiushirikiano na Msumbiji kwa nyanja zote ikiwemo elimu na biashara.
Rais huyo aliyewasili nchini juzi kwa ziara yake ya kikazi ambapo alikaribishwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Baada ya dhifa maalumu iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Nyusi alitembelea Zanzibar na kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambapo waliongea mengi huku wakitaka Zanzibar na Msumbiji zifungue mipaka na kuwa karibu kibiashara.
Baada kutua mnjini Dodoma leo Rias Mbise akiwa na mwenyeji wake rais Kikwete, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kwenda Msumbuji kwa ajili ya kufanya biashara na hata kusomavfani mbalimbali zinazopatikana kwenye vyuo vya nchi hiyo, huku akisisitiza kuimarisha urafiki wao uliodumu kwa miaka mingi sasa tangu nchi hizo kupata uhuru toka mikononi mwa wakoloni.
Naye Spika wa Bunge, Bi Anne Makinda alimpongeza Raisi Nyusi kwa ziara yake nchini ikizingatiwa kwamba hiyo ni ziara ya kwanza kwa Rais huyo kutembelea nchi za nje ya Msumbiji tangu alipotawazwa rasmi kuwa raisi mnamo oktoba mwaka jana

 
Rais Filipe Jacinto Nyusi Amelihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Rais wa Msumbiji Fellipe Jacinto Nyusi leo amelihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema ziara yake imelenga kuja kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili tangu enzi za harakati za ukombozi.

Rais Nyusi amesema hayo leo wakati alikilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini ambapo amesema siku zote maendeleo ya nchi yanatokana na uhusiano mzuri baina ya nchi na nchi.
Bw. Nyusi ambaye anakuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji kuhutubia bunge la Tanzania, amesema kuwa mbali na ushirikiano mzuri wa kisiasa angependa kuendeleza ushirikiano wa kibiashara, elimu na katika nyanja nyingine mbalimbali.
Rais Nyusi ambaye aliingia nchini Juzi ameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kisha akaelekea visiwani Zanzibar ambapo alikutana na Rais wa visiwa hivyo Dkt, Ali Mohammed Shein na leo amemalizia ziara yake Bungeni mjini Dodoma.
Katika hotuba, Rais Nyusi pia ameahidi kushirikiana na Tanzania katika ulinzi wa amani pamoja na vita dhidi ya ugaidi katika mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake spika wa bunge la Muungano Mh. Anne Makinda amesema kuwa ni heshima kubwa kwa Rais huyo wa kwanza wa msumbiji kuhutubia bunge na kuongeza wataendelea kukuza uhusiano baina ya nchi hizo ili kuleta maendeleo ya nchi hizo.
Makinda amesema kumekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa ambao kwa sasa wataendeleza mshikamano kati ya wabunge wa Tanzania na Msumbuji ili kuboresha maisha ya wananchi wa nchiu zote mbili.





Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam


Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimkaribisha Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mh. Filipe Nyusi ,Ikulu ya Zanzibar

Rais Kikwete akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Msumbiji zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi








Tuesday, May 5, 2015

Mwenyekiti wa ‪ CHADEMA‬ Freeman Mbowe alivyoungana na DC wa Kinondoni Paul Makonda kutatua mgomo wa Mabasi Ubungo Dar es Salaam '

Mbowe akiwapungia wananchi

 

 

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mh Freeman Mbowe alipokuwa katika stendi ya mabasi Ubungo kuzungumza na madereva ambao walikuwa wakiendelea na mgomo na kuitaka serikali iwasikilize shida zao.
 
Mbowe ambaye aliwasili  majira ya saa nne kasoro robo asubuhi alijikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku wengine wakifuta barabara ili gari yake ipite huku nyimbo za Ukawa zikiimbwa, jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.

Kuhusu mgomo huo mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh PAUL MAKONDA aliwaomba madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakua tayari imeshatoa tamko.

Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba wawe wamesikilizwa kero zao.

Tuesday, May 5, 2015

MGOMO WA MADEREVA WAMALIZIKA-TUME KUUNDWA NA MAJIBU KUPATIKANA NDANI YA SIKU SABA




Mgomo  wa  Madereva  umemalizika baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya viongozi wa madereva, jeshi la polisi na mkuu wa wilaya  ya  Kinondoni.
Akisoma  makubaliano  hayo  mbele  ya  wenzake, kiongozi wa madereva   amesema  kuwa wamekubaliana madai  yao  kutatatuliwa  ndani  ya  siku 7 kupitia  timu  ya  madereva iliyoundwa kushughulikia  madai  hayo pamoja na tume itakayoundwa.
Mabasi ya mikoani kutoka Ubungo sasa yameanza safari baada ya mgomo wamadereva uliodumu kwa  takriban siku 2. 
 
Makubaliano yaliyofikiwa ni kuundwa kwa kamati ya madereva zaidi ya 8 watakaokutana na mkuu wa wilaya kuanzia kesho.
 
Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai yao kwa muda usiozidi siku 7 kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya Paul Makonda.
 

Tuesday, May 5, 2015

Mgomo Wa Madereva: Mbowe Apokelewa Kwa Shangwe Na Madereva Waliogoma Ubungo, Dar

 
 
Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewasili kituo cha mabasi Ubungo na kupokelewa kwa shangwe na Madereva walioko kwenye mgomo
Mgomo huo  leo  umeingia  siku  ya pili na  hali  bado haieleweki kuwa lini mwisho wa ukomo wa mgomo huu kutokana na  ukimya  wa  mamlaka  husika.