Kilimo kikitumika kwa usahihi ni mkombozi wa mwananchi. Shime twendeni shambani tukalime,tutokomeze umaskini na njaa. Emmanuel Edwin Minja
MAENDELEO HUJA KWA WATU KUJITUMA .WANA KIKUNDI CHA HAVILA WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUSINDIKA MATUNDA MAENEO YA MARKAZ UKONGA ILALA DAR ES SALAAM. EMMANUEL MINJA
Monday, April 10, 2017
KIJUE KILIMO CHA MAHINDI YA KUCHOMA (GOBO) PAMOJA NA MCHANGANUO WAKE
Biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo)ni biashara ambayo inaweza kumtoa mkulima kimaisha. Unaweza kulima
kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha. Angalia mchanganuo
ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa tsh 50,000/=, kulima
30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa
wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi
mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea
hatua husika. Mahindi huchukua wastani wa siku 90 (miezi mitatu) tangu kupanda hadi kugoboa (yaani kuvuna haya mahindi mabichi).
Unaweza
kupanda kwa kutumia mvua au kutumia umwagiliaji mahali popote Tanzania.
Kwa ekari moja ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna
kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa tsh. 150/= hadi 250/=,
kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa
ekari moja unaweza kupata tsh. 1,470,000/= kwa kadirio la chini na tsh.
2,450,000/= kwa kadirio la juu.
Ukitoa
gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi
tsh 2,140,000/= kwa kadirio la juu. Ukilima eka 5, una uhakika wa faida
ya tsh milioni 10.7. Je, ukilima misimu kadhaa, bado utashindwa kujenga
nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza!
Unachohitaji wewe ni mambo yafuatayo: utayari, uthubutu, kuwa-up-to-date
kwa taarifa za misimu na masoko na uwe ni mtu wa kufuatilia fursa na
kujifunza. Fursa zipo 'bwerere', kama una 'allergy' na kilimo tafuta na
ujifunze fursa nyinginezo; LAKINI; mtu YEYOTE anaposema fedha ni ngumu,
kiukweli anakuwa hayupo "serious" kabisa na haya maisha!
MAISHA NI VITA!MAMBO YA UJASIRIAMALI HAYO
KILIMO CHA MBOGA MBOGA - KUNDE |
Subscribe to:
Posts (Atom)