Ridhiwani kikwete aendelea na kampeni za lala salama chalinze
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa
Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita
kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la
Chalinze,Jana Machi 30,2014.Picha zote na Othman Michuzi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini Mzee Hussein
Mwindadi ambaye ni Baba wa Diwani wa Kata ya Mkange.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa
Kijiji cha Manda Mazingara wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika
jana Machi 30,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akionyeshwa maendeleo ua ujenzi wa
Msikiti (haupo pichani) na Sheikh Yahya Abdullah Imam wa Msikiti huo.
Wananchi wa Kijiji cha Manda Mazinga wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika jana Machi 30,2014.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
(Yesterday)
Daily News 31 MarChalinze warned against voter card buyers
Chalinze warned against voter card buyers
Daily News
CHALINZE residents in Bagamoyo District, Coast Region, have been cautioned against being tricked into selling or giving up their voter cards to anyone as it is against the law. The warning was sounded by the campaigns manager of the Chama Cha ...
2 days ago
Fullshangwe 30 MarTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA KAMPENI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA CHALINZE
Sisty Nyahoza Msajili masidizi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
akizungumza na waandhishi wa habari katika ukumbi wa Masai Chalinze
kuhusu mwenendo wa kampeni za vyama na wagombea wa uchaguzi mdogo wa
jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu, kutoka
kushoto ni Muhidini Mapayo Mwanasheria na kiongozi wa timu ya Ofisi ya
Msajili Chalinze na Erald Martin Ofisa Sheria.
2 days ago
Tanzania Daima 30 MarMvua zaathiri kampeni Chalinze
MVUA zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa
nchini zimesababisha baadhi ya mikutano ya kampeni katika Jimbo la
Chalinze kutofanyika. Kampeni hizo zinazoendelea katika maeneo ya Jimbo
la Chalinze zinatarajiwa kuhitimshwa...
3 days ago
MichuziCCM YAENDELEA NA MBIO ZAKE KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA CHALINZE
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Hondogo,Kata ya Mandera wakati wa muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,leo Machi 29,2014.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,Suleiman Jaffo akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mandera Kibaoni wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kuruka sambamba na wakina Mama wa Kabila la Wamasai,wakati alipowasili kwenye Kitongoji cha Nameloki Chatanga,Kijiji cha Umasaini,Kata ya Mandera.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Magole,Kata ya Mandera wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.
Wananchi wa Kijiji cha Hondogo katika Kata ya Mandera ndani ya Jimbo la Chalinze,wakinyoosha mikono juu kuashiria kumpigia kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Mkutano wa Kampeni zake zilizofanyika Machi 29,2014.Picha na Othman Michuzi.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
3 days ago
MichuziMSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA CHALINZE ULIVYOKABILIWA CHANGAMOTO YA BARABARA
Mwenyekiti wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze,Saleh Mpwimbwi akiangalia
gari linaloongoza Msafara wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze wa
tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete likipita kwa shinda kwenye
barabara yenye tope kutoka Kijiji cha Hondogo kwenda Kilemela,wakati wa
safari ya kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo,Machi
29,2014.hali hiyo imekuja kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha kwa siku
mbili mfululizo katika Maeneo mbali mbali hapa nchini.Ridhiwani Kikwete
amewaahidi wakazi wa Kijiji cha Kilemela kuwa,moja ya kazi zake za awali
atakazoanza nazo pindi atakapopata Ubunge ni kuhakikisha barabara hii
inapitika vizuri kwa kipindi chote.
Gari hilo likiendelea kwenda kwa shida shida huku likiteleza na kupelekwa pembeni ya barabara kama inavyoonekana pichani.
Likafika mahala likanasa.
Wadau wakijaribu kulinasua gari hilo.
Mbinu mbadala za kulitoa gari hilo zikiendelea.
Mambo yakiendelea na baadae walifanikiwa kulinasua gari hilo na kulirudisha barabarani ili liendelee na safari yake.
3 days ago
Fullshangwe 29 MarMWENYEKITI WA CCM PWANI:RIDHIWANI KIKWETE NI (TANGANYIKA JEKI) ITAWAKWAMUA WANACHALINZE KATIKA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mhalinze wakati wa mkutano wa
kampeni uliofanyika kijiji cha Kibindu na kuhudhuriwa na wakazi wa
kijiji hicho, akimuombea kura Ridhiwani Kikwete mgombea wa kupitia Chama
cha Mapinduzi amemfananisha mgombea huyo na Jeki aina ya (Tanganyika
Jack) na kusema atawakwamua wana Chalinze katika changamoto
zinazowakabili katika maendeleo jimboni humo,Uchaguzi mdogo wa jimbo la
Chalinze unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu.(PICHA NA KUKOSIKAZI
CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)
3 days ago
Tanzania Daima 29 MarWawekezaji Chalinze feki wamkera diwani
DIWANI wa Lugoba, Rehema Mwene, amelalamikia kitendo cha
baadhi ya wawekezaji kuomba kuwekeza na kushindwa kutekeleza makubaliano
ya maombi yao. Mwene alitoa kauli hiyo juzi kwenye mikutano ya kampeni
ya...
4 days ago
Fullshangwe 28 MarRIDHIWANI KIKWETE AFUNIKA KATA YA PERA CHALINZE
Mgombea
ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani
Kikwete akiwahutubia wananchi katika viwanja vya kwa Mwarabu kata ya
Pera Chalinze leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
jimbo hilo, Unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo,
Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6
ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na
wananchi kwa ujumla wake uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo. (PICHA
NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
WENGI WAMPA UBUNGE RIDHIWANI CHALINZE
Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Ridhiwan Kikwete. WANANCHI wa vijiji kadhaa vilivyomo katika Jimbo la
Chalinze, ambalo Aprili 6, mwaka huu litafanya uchaguzi mdogo wa Ubunge,
wamempa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM). Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Ijumaa katika vijiji saba
vya jimbo hilo, wengi wa waliohojiwa kuhusu mshindi wa nafasi hiyo,
walisema…
5 days ago
Habarileo 27 MarCCM: Ridhiwani suluhisho Chalinze
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Mwishee Mlau amesema mwenye uwezo wa kutatua changamoto zilizopo katika Jimbo la Chalinze ni mgombea wa chama hicho, Ridhiwani Kikwete na sio mgombe