RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE KWENDA TEGETA LEO
B
BARABARA YA MWENGE KWENDA TEGETA INAYOFUNGULIWA LEO
Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta itakayofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta utakaofanyika Oktoba 1, 2014.
Ufunguzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.
Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (CGU), Wizara ya Ujenzi.
Mheshimiwa Dk. Magufuli akikagua ujenzi wa Barabara wkati huo.Hatimaye sasa imekamilika
MZEE KARIBU SANA NYUMBANI,
RAIS KIKWETE AKIWA NA WAKUU WA VYOMBOVYA ULINZI NA USALAMA UWANJA WA MWL. jULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOWASILI KUTOKA MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA ULIOFANYIKA NCHINI MAREKANI
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg’aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
Ni safari ndefu lakini yenye faraja na matumaini.
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama baada ya kutumia usafiri wa baiskeli.
Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg’aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga.
Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mg’aro ambapo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mkinga itaboreshwa, halafu na umeme utawekwa katika Kata hiyo.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya msafara wake kukabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mkinga katika Kata ya Daluni.
Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Maramba.
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji.
Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga.
No comments:
Post a Comment