Tuesday, December 23, 2014

Kazimzumbwi residents ordered to vacate forest reserves to allow forest sustainability.

By The guardian reporter, 20th December 2014

Ministry of Natural Resources and Tourism,Lazaro Nyalandu.
The Government has issued 48-hour ultimatum until today for Kazimzumbwi residents to stop cultivation activities and vacate the forest reserve they  had invaded in the Coast Region’s district of Kisarawe.

Fatma Kimario, Kisarawe district commissioner issued the ultimatum in a meeting with the local residents at Magulue on Friday where she gave violators a repeated warning over the non-sanctioned activities in a forest reserve  belonging to the Ministry of Natural Resources and Tourism.

She said the rainforest that stretches tens of kilometers into the Eastern zone of  Dar Es Salaam is of special significance in protecting water sources and resisting the prevailing climate change.

There has been a serious tug-of-war that involved court battles between the Kisarawe residents and the government authorities over appropriation of the forest since 2011.

While the residents claim that the forest is an ancestral heritage the government says it is a public heritage falling under the government laws of natural resources preservation.

Though the residents have repeatedly ended up losers in court battles, they had been so reluctant to vacate the area that by Thursday about 300 residents were still holding the non-sanctioned plots in the area.  Jackson Rwehumbiza, a resident of Kisarawe is just one of the 300 people who have vowed not to vacate come what may.

“We can not just leave the place as if we were chickens… these plots belonged to our ancestors,” he said adding, “they demolished our houses in 2011, and when they went to the responsible Ministry we were told we were eligible to live here.”

He said they will file complaints before the Prime Minister’s Office to demand a better place if they would be evacuated.
But Kimario insisted legal actions be taken immediately if her orders would be defied.
SOURCE: THE GUARDIAN




Sakata la Escrow, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Siku moja baada ya Rais Kikwete kuhutubia wazee wa Dar es Salaam na kumsimamisha kazi aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na kutoa taarifa kwamba suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi linashughulikiwa na mamlaka husika kwa kuwa Katibu Mkuu huyo ni Mtumishi wa Umma saa chache zilizopita kuna taarifa rasmi iliyotolewa na Kurugrnzi ya Mawasiliano yaIkulu Tanzania.
Taarifa hiyo inasema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi,  Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Uchunguzi huu ni moja ya hatua za utekelezaji wa maazimio nane yaliyotolewa na Bunge ambayo yalimtaka Rais Kikwete kuwawajibisha wahusika wote waliohusika na ubadhilifu wa pesa za Escrow.

Hii hapa taarifa kamili iliyotolewa na Kurugeni hiyo muda mfupi uliopita.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi,  Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014
Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow




Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.

Mheshimiwa Rais Akiingia ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick akimkaribisha mhe. Rais ili kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam
















Makundi ya watu mbalimbakli yaliyohudhuria mkutano huo wa Rais na Wazee wa Dar es Salaam


Mheshimiwa Rais akiondoka kwenye Ukumbi wa Diamond jubilee ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kuwashughulikia wote waliotajwa kwenye ripoti ya ESCROW kulingana na mamlaka zao za uteuzi na maadili. Katika mkutano huo alimfuta kazi Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makaazi  Mhe. Anna Tibaijuka kwa kosa la Maadili ya Utumishi wa Umma