Sakata la Escrow, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Siku
moja baada ya Rais Kikwete kuhutubia wazee wa Dar es Salaam na
kumsimamisha kazi aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Prof. Anna Tibaijuka na kutoa taarifa kwamba suala la Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi linashughulikiwa na
mamlaka husika kwa kuwa Katibu Mkuu huyo ni Mtumishi wa Umma saa chache
zilizopita kuna taarifa rasmi iliyotolewa na Kurugrnzi ya Mawasiliano
yaIkulu Tanzania.
Taarifa hiyo inasema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi,
Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini ili kupisha uchunguzi wa
tuhuma dhidi yake kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Uchunguzi huu ni moja ya hatua za
utekelezaji wa maazimio nane yaliyotolewa na Bunge ambayo yalimtaka Rais
Kikwete kuwawajibisha wahusika wote waliohusika na ubadhilifu wa pesa
za Escrow.
Hii hapa taarifa kamili iliyotolewa na Kurugeni hiyo muda mfupi uliopita.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com Website : www.ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE, 1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi, Katibu
Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma
dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu
Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka
aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na
Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C.
Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia
imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana,
Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa
na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka
kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za
kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa
Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza
kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme
(TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha
tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014
No comments:
Post a Comment