Tuesday, December 23, 2014

Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow




Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.

Mheshimiwa Rais Akiingia ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick akimkaribisha mhe. Rais ili kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam
















Makundi ya watu mbalimbakli yaliyohudhuria mkutano huo wa Rais na Wazee wa Dar es Salaam


Mheshimiwa Rais akiondoka kwenye Ukumbi wa Diamond jubilee ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kuwashughulikia wote waliotajwa kwenye ripoti ya ESCROW kulingana na mamlaka zao za uteuzi na maadili. Katika mkutano huo alimfuta kazi Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makaazi  Mhe. Anna Tibaijuka kwa kosa la Maadili ya Utumishi wa Umma


No comments:

Post a Comment