Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama vile madini ya Zinki, Copper, Magnesium, Manganese, na chuma.Mbegu za maboga ni tamu na unaweza kuzitafuna tu kama karanga.
Kama ulikuwa hujui basi zifuatazo ni faida za mbegu za maboga.
1. UGONJWA WA MOYO.
Kutokana na wingi madini ya magnesium katika mbegu za maboga huwasaidia watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo.
Madini ya magnesium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hivyo kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.
Mbegu hizi pia zina mafuta aina ya OMEGA 3 ambayo ni muhimu kwa watu wenye ugonjwa wa moyo.
2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI.
Mbegu za maboga zina kiasi kikubwa cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zinki ni kuimarisha kinga ya mwili.
Upungufu wa madini ya zinki mwilini unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine ya kimwili na kiakili.
3. KUIMARISHA UWEZO WA MACHO KUONA.
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin ambavyo ni muhimu macho.
Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa MELANIN kimeng’enya muhimu ambacho hutengenezwa ndani ya mwili kwa ajili ya kinga ya macho.
4. KINGA YA KISUKARI.
Mbegu za maboga zina NICOTINIC ACID, TRIGONELLINE na D-CHIRO-INOSITOL ambavyo husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye mwili na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuwapa nafuu watu wenye kisukari.
5. DAWA YA USINGIZI.
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi, usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress.
Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.
6. DAWA BORA YA UVIMBE.
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation).
Kama ujuavyo sehemu kubwa ya uvimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.
7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara pia zina OMEGA 3.
Mama mjamzito hata anayenyonyesha anaweza kutumia mbegu za maboga na atakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.
8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME.
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.
Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni muhimu sana kwa afya ya tezi dume.
9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME.
Sababu zinazopelekea kuondoa tatizo hili kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinashusha sukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na pia zina madini ya ZINKI madini ambayo ni muhimu kwa upande wa nguvu za kiume pia zinaongeza uwingi wa mbegu za kiume (sperm count).
10. ZINAONDOA MSONGO WA MAWAZO (STRESS).
Kama maisha yako ni ya stress fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku utaona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya muhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho TRYPTOPHAN na Amino asidi zingine muhimu zinazohusika katika utengenezaji wa homoni ya SEROTONIN ambayo ni katika kuratibu matendo kadhaa katika ubongo.
11. HUZUIA MCHANGA KWENYE KIBOFU CHA MKOJO.
Madini ya phosphorous kwenye mbegu za maboga ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo.
Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili.
12. AFYA YA MIFUPA.
Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na virutubisho vingine vingi muhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
13. KUWEKA SAWA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU.
Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili muhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.
14. AFYA YA UBONGO.
Mbegu za maboga zina asidi mafuta aina ya OMEGA 3 zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘ALPHA-LINOLENIC ACID’ ambazo ni muhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo.
Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo.
15. TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU.
Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma.
Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito.
16. KUPUNGUZA UZITO.
Mbegu hizi zina uwezo wa kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula kula ovyo.
17. UPONYAJI WA VIDONDA.
Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi.
MATUMIZI:
Unaweza kuzitumia zikiwa kavu yaani baada ya kukauka kwenye jua.
Unakuwa unazitafuna tu kama karanga wala usihofu siyo chungu na unatafuna na maganda yake.
Pia unaweza kuzikaanga kwenye mafuta isizidi dakika tano kama utapenda weka chumvi kidogo kuongeza ladha ila sio lazima.
Tafuna angalau nusu kikombe cha chai kwa siku.
Unweza kuzisaga au kuzitwanga kupata unga ambao utakuwa unauchanganya kwenye juisi yako ya matunda au uji angalau vijiko viwili kwa siku siyo mbaya.
Hata kwa mtoto pia kumchanganyia kwenye uji siyo mbaya hayo ndo matumizi yote kwa tiba unayokusumbua hapo