Ufugaji wa mbuzi nchini Tanzania una fursa nzuri.
Wakulima wadogo wanaoweza kuanza kidogo kidogo kulingana na mazingira yao kwa kutumia rasiliali zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo miti ya kujenga mabanda, majani yanayopatikana kulishia mifugo, madawa ya asili kutibu mifugo yao, wanafamili waliopo kuchunga na kusimamia mbuzi wako na rasilimali nyingine ikiwemo miti, mchanga,maji , mabaki ya vyakula n.k.. Lakini mafanikio makubwa yanahitaji usimamizi mzuri, uchangamfu wa soko na kuwekeza katika kuwapatia mbuzi wako lishe nzuri ili wapate afya na uzalishaji uongezeke. Mfano unaweza kukua sana kibiashara ikiwa utaelewa soko lako, aina ya mbuzi unaofuga na kutunza kumbukumbu za gharama zako ili ujue wapi pana kugharimu zaidi ili utafute mbinu za kupunguza gharama.
Ni vizuri uwe na mpango wa biashara (business plan) ya ufugaji wa mbuzi unapoanza kwa mfano unaanza na mbuzi 20–50, ili kujipanga kujua unatoka wapi, unaelekea wapi na uendeje ufike unapotarajia
Picha kwa hisani ya Biosciences, imeandaliwa na Emmanuel Edwin Minja #ShambaniUpdates # #ShambaniNews #ItawatuTanzania


 
No comments:
Post a Comment