Kuna soko kubwa na la kudumu
Mbuzi wanahitajika kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi na hata mbolea. Mahitaji haya yapo mijini na vijijini mwaka mzima hivyo ni fursa.
Uwekezaji wa awali si mkubwa
Ukilinganisha na uwekezaji wa ng’ombe, gharama za kuanzisha ufugaji wa mbuzi ni ndogo (linahitajika banda, chakula, ununuzi wa mbuzi, msimamizi au mchungaji , gharama za matibabu , chanjo n.k).
Wanastahimili mazingira magumu
Mbuzi ni miongoni mwa wanayama wanavumilia ukame na magonjwa fulani, hivyo wanafaa hata maeneo yenye hali ngumu ya hewa.
Wanazaliana kwa haraka
Jike linaweza kuzaa watoto 2–3 mara mbili kwa mwaka ukipata mbegu bora, hivyo kuongeza idadi ya mifugo yako kwa kasi.
Bidhaa nyingi kwa faida : Nyama (chevon) ; Maziwa yenye virutubisho vingi ; Ngozi bora ; Mbolea ya asili nzuri
1. Uchaguzi wa aina bora ya mbuzi :
Kwa maziwa: Mbuzi wa Saanen, Toggenburg au Alpine.
Kwa nyama: Mbuzi wa Boer, Galla au Small East African (Mbuzi wa kienyeji walioboreshwa).
2. Makazi (Banda/zizi) Liwe safi, lenye hewa ya kutosha na linalokinga mvua na jua. Kama ni sakafu inashauriwa iwe na mteremko mdogo ili maji na uchafu vitoke kirahisi. Zingatia nafasi ya kutosha kwa kila mbuzi (~1.5 m² kwa mmoja).
3. Lishe bora
Wape majani mabichi, mikunde (lucerne, desmodium) na nyasi zilizokaushwa.
Ongeza chakula cha ziada (concentrates) kama pumba, dagaa na chumvi ya madini.
Hakikisha wana maji safi muda wote.
4. Afya na usafi
Chanjo za mara kwa mara dhidi ya magonjwa (kama PPR, CBPP na nimonia).
Dhibiti minyoo ya ndani na nje kwa kutumia dawa.
Dumisha usafi wa zizi na vyombo vya kulia chakula.
5. Uzalishaji na uongezaji wa thamani
Hakikisha unapanga uzalishaji kwa kuchagua madume bora.
Fanya usajili na kumbukumbu za uzalishaji (tarehe ya kuzaa uzito, afya).
Zingatia kutoa bidhaa zenye ubora (maziwa yaliyopakiwa vizuri, nyama safi, ngozi kavu vizuri n.k).
6. Masoko
Unaweza kutafuta mikataba na wauzaji wa nyama, maziwa, mighahawa au hoteli.
Shirikiana na vikundi au vyama vya wafugaji ili kupanuka na kuongeza nguvu yako ya soko.
Mfano wa makadirio ya faida
Mfugaji mwenye mbuzi 20 anaweza kupata kupata faida kwa wastani :
Maziwa: lita 2–3 kwa siku × mbuzi 15 × miezi 8 ( Kuna miezi hukamui) = zaidi ya lita 7,000 kwa mwaka.
Chukulia bei ya maziwa: Kwa lita Tshs 1,500 ⇒ utapata zaidi ya Tsh 10 milioni kwa mwaka.
Utapata uzao wa watoto wa mbuzi: wastani wa 30–40 kwa mwaka
Faida nyingine ya ni kuuza au kuongeza idadi.
Ukifuata utaratibu, ufugaji wa mbuzi unaweza kukuingizia kipato kizuri na kuwa biashara endelevu yenye tija.


No comments:
Post a Comment