Saturday, October 21, 2017

KILIMO BORA CHA TANGAWIZI (ZINGIBER OFFICINALE)

Tangawizi


UTANGULIZI

Jina la kitaalamu ni Zingiber officinaleTangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro. 

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achali n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).

AINA ZA TANGAWIZI

Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.

TABIA YA MMEA

Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.
Mmea-wa-tangawizi
Mmea wa tangawizi


HALI YA HEWA NA UDONGO

Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

UPANDAJI

Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja.

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.
shamba-latangawizi
Shamba la tangawizi

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine hutumika.
mimea-midogo-ya-tangawizi
Mimea ya tangawizi ikiota

MAGONJWA NA WADUDU


  • Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
  • Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp
  • Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.

UVUNAJI

Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana. 

Tangawizi-iking'olewa-shambani
Tangawizi iking'olewa

USINDIKAJI

Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.
Tangawizi-iliyovunwa
Tangawizi baada ya kuvunwa

SOKO LA TANGAWIZI

Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni kati ya Tsh. 4000 - 6,500/- kwa kilo (Soko Kuu Morogoro. June, 2017). Bei hutofautiana kulingangana na masoko, ulizia soko la karibu yako.

Bila shaka umepata kitu kwa elimu hii nzuri kabisa ya kilimo cha tangawizi. sasa ni wakati wako ku-share uzoefu wako na wakulima wenzako. weka comment yako hapa chini
LEMONGRASS (MCHAICHAI), ZANZIBAR, TANZANIA.
 
Photo

Lemongrass is a plant. The leaves and the oil are used to make medicine.

Lemongrass is used for treating digestive tract spasms, stomachache, high blood pressure, convulsions, pain, vomiting, cough, achy joints (rheumatism), fever, the common cold, and exhaustion. It is also used to kill germs and as a mild astringent.

Some people apply lemongrass and its essential oil directly to the skin for headache, stomachache, abdominal pain, and muscle pain.

By inhalation, the essential oil of lemongrass is used as aromatherapy for muscle pain.

In food and beverages, lemongrass is used as a flavoring. For example, lemongrass leaves are commonly used as “lemon” flavoring in herbal teas.

In manufacturing, lemongrass is used as a fragrance in soaps and cosmetics. Lemongrass is also used in making vitamin A and natural citral.

How does it work?
Lemongrass might help prevent the growth of some bacteria and yeast. Lemongrass also contains substances that are thought to relieve pain, reduce fever, stimulate the uterus and menstrual flow, and have antioxidant properties.
LEMONGRASS (MCHAICHAI), ZANZIBAR, TANZANIA.

Lemongrass is a plant. The leaves and the oil are used to make medicine.

Lemongrass is used for treating digestive tract spasms, stomachache, high blood pressure, convulsions, pain, vomiting, cough, achy joints (rheumatism), fever, the common cold, and exhaustion. It is also used to kill germs and as a mild astringent.

Some people apply lemongrass and its essential oil directly to the skin for headache, stomachache, abdominal pain, and muscle pain.

By inhalation, the essential oil of lemongrass is used as aromatherapy for muscle pain.

In food and beverages, lemongrass is used as a flavoring. For example, lemongrass leaves are commonly used as “lemon” flavoring in herbal teas.

In manufacturing, lemongrass is used as a fragrance in soaps and cosmetics. Lemongrass is also used in making vitamin A and natural citral.

How does it work?
Lemongrass might help prevent the growth of some bacteria and yeast. Lemongrass also contains substances that are thought to relieve pain, reduce fever, stimulate the uterus and menstrual flow, and have antioxidant properties.

KILIMO CHA ZAO LA SOYA



Utangulizi:
Soya
(Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde ambalo asili yake ni bara la Asia katika nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao hili liingizwa hapa nchini katika mnamo mwaka 1907 katika maeneo ya Amani wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga. Kilimo cha zao hili kiliendelea kupanuka katika miaka ya 1930 na 1960 na kuenea katika mkoa wa Mtwara, Morogoro, na Ruvuma. Kutokana na uhamasishaji juu ya matumizi ya soya kwa lishe. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa uzalishaji ni pamoja na Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine inayofaa kwa kilimo cha zao hili ni pamoja na Tanga, Lindi, Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara



.
Aina za soya
Zipo aina mbalimbali za soya, hapa nchini aina zinazozalishwa ni pamoja na Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na Kaleya. Aina hizi hutofautiana katika kustawi na kutoa mavuno hata hivyo soya aina ya Bossier huweza kustawi katika maeneo mengi zaidi hapa nchini. Mazingira yanayofaa kwa uzalishaji Soya huhitaji mvua ya kutosha ya wastani wa milimita 350 hadi 1,500 kwa mwaka inayonyesha katika mtawanyiko mzuri au umwagiliaji maji ili kuhakikisha upatikanaji wa unyevu wa kutosha kuanzia upandaji hadi inapotoa maua na matunda.
Uvunaji ni muhimu ufanyike wakati hakuna mvua ili kuruhusu soya kukauka vizuri na kutunza ubora wake.
Soya kama yalivyo mazao mengine, huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji. Hivyo kama shamba halina rutuba ya kutosha, ni muhimu kutumia mbolea.
Mbolea za viwandani zinazoweza kutumika ni aina ya DAP na TSP (wastani wa kilo 80 hadi 100 kwa hekta moja) kwa ajili ya kupandia na (wastani wa kilo 60 hadi 80 kwa hekta) za
mbolea ya kukuzia kama CAN. Ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam juu ya rutuba ya udongo kabla ya kuamua kutumia mbolea.
Uzalishaji
Ni muhimu kuzingatia misimu ya mvua ya mahali husika na aina ya soya inayofaa ili kuruhusu soya kukomaa wakati hakuna mvua
na hivyo kuhifadhi ubora wake.
1. Shamba liandaliwe kwa kuondoa magugu na kutifuliwa. Soya inaweza kupandwa katika matuta au katika mistari.
2. Nafasi inayofaa katika kupanda soya ni Sm.5 hadi 10 kati ya mashina na Sm. 45 hadi 60 kati ya mstari na mstari kutegemea aina ya soya na rutuba ya udongo.
3. Kila shimo lipandwe mbegu moja katika kina cha sentimita 2 hadi tano na kufukiwa vizuri kwa udongo.
4. Palizi ifanyike kuondoa magugu, ikiwa soya itastawi na kufunika udongo vizuri inaweza kupunguza uhitaji wa kupalilia zaidi.
5. Soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina,mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba.
Ni vema kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka.
6. Soya iliyovunwa itolewe maganda na kukaushwa vizuri tayari matumizi au.kwa kuhifadhi.
7.Mavuno yanaweza kuwa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta sawa na kilo 600 hadi 1,000 kwa ekari moja kutegemea na aina na
mazingira ya uzalishaji.
Magonjwa na wadudu
Zao la soya halishambuliwi sana na magonjwa na wadudu. Inafaa kuzingatia kanuni za kilimo bora na kupata ushauri wa kitaalamu hasa inapolazimu kutumia madawa ya wadudu na magonjwa. Ni muhimu kuzingatia matumizi ya mbegu safi (zisizo na vimelea vya magonjwa) na kutumia mbinu za mzunguko wa mazao.
Maandalizi ya soya
Ni muhimu kuondoa kemikali zisizofaa kabla ya kutumia soya kwa lishe. Zingatia hatua zifuatazo:-
1. Chemsha maji
2.Tumbukiza soya kidogo kidogo ili iendeleekuchemka
3. Baada ya kuweka soya kwenye maji yanayochemka, chemsha kwa dakika 30 ili kuondoa kemikali zisizofaa.
4. Opoa, suuza na maji safi.
5. Anika hadi zikauke
6. Saga kupata unga kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Unga wa soya unaweza kutumika katika upishi wa vyakula kama vile uji, maziwa,ugali, biskuti , keki n.k
Umuhimu wa Soya
1. Soya ina viini lishe aina ya protini kwa wingi kuliko jamii zote za mikunde na hata baadhi ya protini zinazotokana na wanyama.
2. Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini inaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini.
3. Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu wagonjwa hasa wa UKIMWI;
4. Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato .cha chini katika kuondoa utapiamlo.
5. Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto
yanasaidia viungo kukua kwa haraka;
6. Soya hurutubisha udongo.
7. Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini.
8. Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel
MCHAICHAI NA FAIDA ZAKE KIAFYA

Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai.

Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya.

1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai un uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.
2. Hutibu magonjwa ya kuhara.
Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.
3. Husaidia kusafisha figo na mkojo.
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.
4. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango.
“Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”

5. Mchaichai hutibu vidonda vya tumbo na kupunguza kiwango cha gesi tumboni.
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.
Unachotakiwa kufanya ni ;
Kuendelea kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017

SHULE 10 ZILIZOFANYA VIZURI NA ZILIZOFANYA VIBAYA KITAIFA 

Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.


Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.

Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.

Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters - Kagera,
St, Severine - Kagera,
Alliance – Mwanza
Sir. John – Tanga
Palikas – Shinyanga
Mwanga – Kagera
Hazina - Dar es salaam
St. Anne Marie - Dar es salaam
Rweikiza – Kagera
Martin Luther - Dodoma. 

Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni

Nyahaa – Singida
Bosha - Tanga
Ntalasha – Tabora
Kishangazi – Tanga
Mntamba – Singida
Ikolo – Singida
Kamwala – Songwe
Kibutuka - Lindi
Mkulumanzi – Tanga
Kitwai A – Manyara

Saturday, October 7, 2017

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Pombe Magufuli, leo Oktoba 7 amefanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo.

Rais Magufuli pia amegawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake,  na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

Mhe. Magufuli amemteua Mhe. George Haruma Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri wateule wataapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi: Jenista Mhagama, Umi Mwalimu, balozi Augustino Mahiga, Mwakyembe, Kabudi, wamendelea na wizara zao.Seleman Jaffo: TAMISEMI, Katibu wa Bunge: Aondolewa na kuwekwa mpya ndugu Kagaigai, Medadi Kalemani: Wizara ya Nishati
Angela Kairuki: Waziri wa Madini .