BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Pombe
Magufuli, leo Oktoba 7 amefanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri na
kuongeza wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo
zilikuwepo.
Rais Magufuli pia amegawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake, na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

Mhe. Magufuli amemteua Mhe. George
Haruma Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla
alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Mawaziri wateule wataapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kwa ufupi: Jenista Mhagama, Umi Mwalimu, balozi Augustino Mahiga, Mwakyembe, Kabudi, wamendelea na wizara zao.Seleman Jaffo: TAMISEMI, Katibu wa Bunge: Aondolewa na kuwekwa mpya ndugu Kagaigai, Medadi Kalemani: Wizara ya Nishati
Angela Kairuki: Waziri wa Madini .
No comments:
Post a Comment