Faida
za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha
kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila
mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma
makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai.
Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya.
1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani.
Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel
waligundua mchaichai un uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha
saratani.
2. Hutibu magonjwa ya kuhara.
Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu
wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya
tumbo ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu
magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa
na malaria kali.
3. Husaidia kusafisha figo na mkojo.
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni
kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa
na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo
zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta
akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.
4. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango.
“Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”
5. Mchaichai hutibu vidonda vya tumbo na kupunguza kiwango cha gesi tumboni.
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.
Unachotakiwa kufanya ni ;
Kuendelea kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara
No comments:
Post a Comment