Lengo letu ni kuelimisha, kuhamasisha na kuwaunganisha wakulima na wafugaji kupitia mbinu bora, za kisasa na zenye tija katika kilimo na ufugaji wa mbuzi kibiashara. Tunalenga kuongeza uzalishaji wa mbuzi na kipato, kuboresha maisha ya jamii vijijini na mijini na kuwa daraja linalowaunganisha moja kwa moja wafugaji na masoko salama, yenye faida na uhakika.
Tuesday, December 12, 2017
Saturday, October 21, 2017

UTANGULIZI
Jina la kitaalamu ni Zingiber officinale. Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili
ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi
za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya
Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga,
Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.
Tangawizi
hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha
katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali
kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achali n.k. Hutumika pia
katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za
meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika
vipodozi kama poda n.k).
AINA ZA TANGAWIZI
Hakuna
uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna
dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii
huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.
TABIA YA MMEA
Tangawizi
ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya
ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin
ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na
nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu
ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea
huu yana rangi nyeupe au manjano.
HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao
hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa
bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha
mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi
vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.
UPANDAJI
Zao
la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi
kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5.
Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi
huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700 cha
vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja.
Nafasi
inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao
huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi
ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua
inakosekana.
![]() |
| Shamba la tangawizi |
Wiki
1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani
25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo
36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli
kinapokosekana.
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine hutumika.
MAGONJWA NA WADUDU
- Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
- Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp
- Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi
huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda,
wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa.
Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger
in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa
huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga.
Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa
kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.
USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi
iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine
huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au
hukamuliwa mafuta. Pia
tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa
na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha
16.0-18.0%.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko
la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini.
Bei yake ni kati ya Tsh. 4000 - 6,500/- kwa kilo (Soko Kuu Morogoro.
June, 2017). Bei hutofautiana kulingangana na masoko, ulizia soko la
karibu yako.
Bila
shaka umepata kitu kwa elimu hii nzuri kabisa ya kilimo cha tangawizi.
sasa ni wakati wako ku-share uzoefu wako na wakulima wenzako. weka
comment yako hapa chini
LEMONGRASS (MCHAICHAI), ZANZIBAR, TANZANIA.
Lemongrass is a plant. The leaves and the oil are used to make medicine.
Lemongrass is used for treating digestive tract spasms, stomachache, high blood pressure, convulsions, pain, vomiting, cough, achy joints (rheumatism), fever, the common cold, and exhaustion. It is also used to kill germs and as a mild astringent.
Some people apply lemongrass and its essential oil directly to the skin for headache, stomachache, abdominal pain, and muscle pain.
By inhalation, the essential oil of lemongrass is used as aromatherapy for muscle pain.
In food and beverages, lemongrass is used as a flavoring. For example, lemongrass leaves are commonly used as “lemon” flavoring in herbal teas.
In manufacturing, lemongrass is used as a fragrance in soaps and cosmetics. Lemongrass is also used in making vitamin A and natural citral.
How does it work?
Lemongrass might help prevent the growth of some bacteria and yeast. Lemongrass also contains substances that are thought to relieve pain, reduce fever, stimulate the uterus and menstrual flow, and have antioxidant properties.

KILIMO CHA ZAO LA SOYA
Utangulizi:
Soya
(Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde ambalo asili yake ni bara la Asia katika nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao hili liingizwa hapa nchini katika mnamo mwaka 1907 katika maeneo ya Amani wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga. Kilimo cha zao hili kiliendelea kupanuka katika miaka ya 1930 na 1960 na kuenea katika mkoa wa Mtwara, Morogoro, na Ruvuma. Kutokana na uhamasishaji juu ya matumizi ya soya kwa lishe. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa uzalishaji ni pamoja na Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine inayofaa kwa kilimo cha zao hili ni pamoja na Tanga, Lindi, Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
. Aina za soya
Zipo aina mbalimbali za soya, hapa nchini aina zinazozalishwa ni pamoja na Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na Kaleya. Aina hizi hutofautiana katika kustawi na kutoa mavuno hata hivyo soya aina ya Bossier huweza kustawi katika maeneo mengi zaidi hapa nchini. Mazingira yanayofaa kwa uzalishaji Soya huhitaji mvua ya kutosha ya wastani wa milimita 350 hadi 1,500 kwa mwaka inayonyesha katika mtawanyiko mzuri au umwagiliaji maji ili kuhakikisha upatikanaji wa unyevu wa kutosha kuanzia upandaji hadi inapotoa maua na matunda.
Uvunaji ni muhimu ufanyike wakati hakuna mvua ili kuruhusu soya kukauka vizuri na kutunza ubora wake.
Soya kama yalivyo mazao mengine, huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji. Hivyo kama shamba halina rutuba ya kutosha, ni muhimu kutumia mbolea.
Mbolea za viwandani zinazoweza kutumika ni aina ya DAP na TSP (wastani wa kilo 80 hadi 100 kwa hekta moja) kwa ajili ya kupandia na (wastani wa kilo 60 hadi 80 kwa hekta) za
mbolea ya kukuzia kama CAN. Ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam juu ya rutuba ya udongo kabla ya kuamua kutumia mbolea.
Uzalishaji
Ni muhimu kuzingatia misimu ya mvua ya mahali husika na aina ya soya inayofaa ili kuruhusu soya kukomaa wakati hakuna mvua
na hivyo kuhifadhi ubora wake.
1. Shamba liandaliwe kwa kuondoa magugu na kutifuliwa. Soya inaweza kupandwa katika matuta au katika mistari.
2. Nafasi inayofaa katika kupanda soya ni Sm.5 hadi 10 kati ya mashina na Sm. 45 hadi 60 kati ya mstari na mstari kutegemea aina ya soya na rutuba ya udongo.
3. Kila shimo lipandwe mbegu moja katika kina cha sentimita 2 hadi tano na kufukiwa vizuri kwa udongo.
4. Palizi ifanyike kuondoa magugu, ikiwa soya itastawi na kufunika udongo vizuri inaweza kupunguza uhitaji wa kupalilia zaidi.
5. Soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina,mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba.
Ni vema kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka.
6. Soya iliyovunwa itolewe maganda na kukaushwa vizuri tayari matumizi au.kwa kuhifadhi.
7.Mavuno yanaweza kuwa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta sawa na kilo 600 hadi 1,000 kwa ekari moja kutegemea na aina na
mazingira ya uzalishaji.
Magonjwa na wadudu
Zao la soya halishambuliwi sana na magonjwa na wadudu. Inafaa kuzingatia kanuni za kilimo bora na kupata ushauri wa kitaalamu hasa inapolazimu kutumia madawa ya wadudu na magonjwa. Ni muhimu kuzingatia matumizi ya mbegu safi (zisizo na vimelea vya magonjwa) na kutumia mbinu za mzunguko wa mazao.
Maandalizi ya soya
Ni muhimu kuondoa kemikali zisizofaa kabla ya kutumia soya kwa lishe. Zingatia hatua zifuatazo:-
1. Chemsha maji
2.Tumbukiza soya kidogo kidogo ili iendeleekuchemka
3. Baada ya kuweka soya kwenye maji yanayochemka, chemsha kwa dakika 30 ili kuondoa kemikali zisizofaa.
4. Opoa, suuza na maji safi.
5. Anika hadi zikauke
6. Saga kupata unga kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Unga wa soya unaweza kutumika katika upishi wa vyakula kama vile uji, maziwa,ugali, biskuti , keki n.k
Umuhimu wa Soya
1. Soya ina viini lishe aina ya protini kwa wingi kuliko jamii zote za mikunde na hata baadhi ya protini zinazotokana na wanyama.
2. Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini inaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini.
3. Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu wagonjwa hasa wa UKIMWI;
4. Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato .cha chini katika kuondoa utapiamlo.
5. Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto
yanasaidia viungo kukua kwa haraka;
6. Soya hurutubisha udongo.
7. Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini.
8. Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel
Subscribe to:
Posts (Atom)