Friday, October 24, 2025

Ufugaji wa mbuzi nchini Tanzania una fursa nzuri.

Wakulima wadogo wanaoweza kuanza kidogo kidogo kulingana na mazingira yao kwa kutumia rasiliali zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo miti ya kujenga mabanda, majani yanayopatikana kulishia mifugo, madawa ya asili kutibu mifugo yao, wanafamili waliopo kuchunga na kusimamia mbuzi wako na rasilimali nyingine ikiwemo miti, mchanga,maji , mabaki ya vyakula n.k.. Lakini mafanikio makubwa yanahitaji usimamizi mzuri, uchangamfu wa soko na kuwekeza katika kuwapatia mbuzi wako lishe nzuri ili wapate afya na uzalishaji uongezeke. Mfano unaweza kukua sana kibiashara  ikiwa utaelewa soko lako, aina ya mbuzi unaofuga na kutunza kumbukumbu za gharama zako ili ujue wapi pana kugharimu zaidi ili utafute mbinu za kupunguza gharama.

Ni vizuri uwe na mpango wa biashara (business plan) ya ufugaji wa mbuzi unapoanza kwa mfano unaanza na mbuzi 20–50, ili kujipanga kujua unatoka wapi, unaelekea wapi na uendeje ufike unapotarajia


Picha kwa hisani ya Biosciences, imeandaliwa na Emmanuel Edwin Minja #ShambaniUpdates # #ShambaniNews #ItawatuTanzania

 

Ufugaji wa mbuzi ni fursa inayolipa


 Kuna soko kubwa na la kudumu

Mbuzi wanahitajika kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi na hata mbolea. Mahitaji haya yapo mijini na vijijini mwaka mzima hivyo ni fursa.

Uwekezaji wa awali si mkubwa

Ukilinganisha na uwekezaji wa ng’ombe, gharama za kuanzisha ufugaji wa mbuzi ni ndogo (linahitajika banda, chakula, ununuzi wa mbuzi, msimamizi au mchungaji , gharama za matibabu , chanjo n.k).

Wanastahimili mazingira magumu

Mbuzi ni miongoni mwa wanayama wanavumilia ukame na magonjwa fulani, hivyo wanafaa hata maeneo yenye hali ngumu ya hewa.

Wanazaliana kwa haraka

Jike linaweza kuzaa watoto 2–3 mara mbili kwa mwaka ukipata mbegu bora, hivyo kuongeza idadi ya mifugo yako kwa kasi.

Bidhaa nyingi kwa faida : Nyama (chevon) ; Maziwa yenye virutubisho vingi ; Ngozi bora ; Mbolea ya asili nzuri


Misingi, kanuni na taratibu nzuri za ufugaji bora wa mbuzi

1. Uchaguzi wa aina bora ya mbuzi : 

Kwa maziwa: Mbuzi wa SaanenToggenburg au Alpine.

Kwa nyama: Mbuzi wa BoerGalla au Small East African (Mbuzi wa kienyeji walioboreshwa).

2. Makazi (Banda/zizi) Liwe safi, lenye hewa ya kutosha na linalokinga mvua na jua. Kama ni sakafu inashauriwa iwe na mteremko mdogo ili maji na uchafu vitoke kirahisi. Zingatia nafasi ya kutosha kwa kila mbuzi (~1.5 m² kwa mmoja).

3. Lishe bora

  • Wape majani mabichi, mikunde (lucerne, desmodium) na nyasi zilizokaushwa.

  • Ongeza chakula cha ziada (concentrates) kama pumba, dagaa na chumvi ya madini.

  • Hakikisha wana maji safi muda wote.

4. Afya na usafi

  • Chanjo za mara kwa mara dhidi ya magonjwa (kama PPR, CBPP na nimonia).

  • Dhibiti minyoo ya ndani na nje kwa kutumia dawa.

  • Dumisha usafi wa zizi na vyombo vya kulia chakula.

5. Uzalishaji na uongezaji wa thamani

  • Hakikisha unapanga uzalishaji kwa kuchagua madume bora.

  • Fanya usajili na kumbukumbu za uzalishaji (tarehe ya kuzaa uzito, afya).

  • Zingatia kutoa bidhaa zenye ubora (maziwa yaliyopakiwa vizuri, nyama safi, ngozi kavu vizuri n.k).

6. Masoko

  • Unaweza kutafuta mikataba na wauzaji wa nyama, maziwa, mighahawa au hoteli.

  • Shirikiana na vikundi au vyama vya wafugaji ili kupanuka na kuongeza nguvu yako ya soko.

Mfano wa makadirio ya faida 

Mfugaji mwenye mbuzi 20  anaweza kupata kupata faida kwa wastani :

  • Maziwa: lita 2–3 kwa siku × mbuzi 15  × miezi 8 ( Kuna miezi hukamui) = zaidi ya lita 7,000 kwa mwaka.

  • Chukulia bei ya maziwa: Kwa lita Tshs 1,500  ⇒ utapata zaidi ya Tsh 10 milioni kwa mwaka.

  • Utapata uzao wa watoto wa mbuzi: wastani wa 30–40 kwa mwaka

  •  Faida nyingine ya ni kuuza au kuongeza idadi.

Ukifuata utaratibu, ufugaji wa mbuzi unaweza kukuingizia kipato kizuri na kuwa biashara endelevu yenye tija.

Thursday, September 18, 2025

 Tanzania ni nchi nzuri, twiga ni ishara moja tuu

Inaelezea kwa uzuri jinsi mnyama kama twiga alivyo alama ya fahari ya taifa lakini pia ni sehemu ndogo tu ya uzuri wa jumla wa nchi ya Tanzania. Kuna mengi zaidi yanayofanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee ambayo kila mtu duniani angetamani kutembelea kuona:

Hifadhi za Taifa – Serengeti, Ngorongoro, Mikumi, Ruaha... ni hazina ya wanyama pori .
Mlima Kilimanjaro – ni mlima mrefu kuliko milima yote Afrika.
Ziwa Tanganyika & Ziwa Victoria – Ni miongoni mwa maziwa makubwa zaidi duniani.
Zanzibar – Historia yake, fukwe na utamaduni wa Kiswahili.
Lugha ya Kiswahili – Lugha ya umoja, upendo na mawasiliano.
Utamaduni na Sanaa – Ngoma zetu, vazi la kitenge, chakula kama ugali, wali, samaki, ndizi za uchaggani, unyakiusani , bukoba... na mengine mengi yanaongeza uzuri wa Tanzania
Watu wake ni wakarimu kuanzia Kaskazini, Magharibi, Mashariki hadi kusini mwa nchi wamejaa wananchi wenye upe npendo na ukarimu wa pekee kwa wageni. 

Twiga, akiwa mrefu na mtulivu, anawakilisha mwelekeo wa juu na uzuri wa asili lakini ni kiwakilishi tu cha hazina kubwa iliyopo nchini  Tanzania. Wewe unawezaje kuielezea Tanzania  na watu wake kwa uzoefu wako ?

Friday, December 23, 2022

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama vile madini ya Zinki, Copper, Magnesium, Manganese, na chuma

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama vile madini ya Zinki, Copper, Magnesium, Manganese, na chuma.Mbegu za maboga ni tamu na unaweza kuzitafuna tu kama karanga.

Kama ulikuwa hujui basi zifuatazo ni faida za mbegu za maboga.

1. UGONJWA WA MOYO.
Kutokana na wingi madini ya magnesium katika mbegu za maboga huwasaidia watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo.
Madini ya magnesium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hivyo kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.
Mbegu hizi pia zina mafuta aina ya OMEGA 3 ambayo ni muhimu kwa watu wenye ugonjwa wa moyo.

2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI.
Mbegu za maboga zina kiasi kikubwa cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zinki ni kuimarisha kinga ya mwili.
Upungufu wa madini ya zinki mwilini unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine ya kimwili na kiakili.

3. KUIMARISHA UWEZO WA MACHO KUONA.
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin ambavyo ni muhimu macho.
Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa MELANIN kimeng’enya muhimu ambacho hutengenezwa ndani ya mwili kwa ajili ya kinga ya macho.

4. KINGA YA KISUKARI.
Mbegu za maboga zina NICOTINIC ACID, TRIGONELLINE na D-CHIRO-INOSITOL ambavyo husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye mwili na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuwapa nafuu watu wenye kisukari.

5. DAWA YA USINGIZI.
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi, usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress.
Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.

6. DAWA BORA YA UVIMBE.
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation).
Kama ujuavyo sehemu kubwa ya uvimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara pia zina OMEGA 3.
Mama mjamzito hata anayenyonyesha anaweza kutumia mbegu za maboga na atakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.

8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME.
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.
Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni muhimu sana kwa afya ya tezi dume.

9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME.
Sababu zinazopelekea kuondoa tatizo hili kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinashusha sukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na pia zina madini ya ZINKI madini ambayo ni muhimu kwa upande wa nguvu za kiume pia zinaongeza uwingi wa mbegu za kiume (sperm count).

10. ZINAONDOA MSONGO WA MAWAZO (STRESS).
Kama maisha yako ni ya stress fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku utaona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya muhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho TRYPTOPHAN na Amino asidi zingine muhimu zinazohusika katika utengenezaji wa homoni ya SEROTONIN ambayo ni katika kuratibu matendo kadhaa katika ubongo.

11. HUZUIA MCHANGA KWENYE KIBOFU CHA MKOJO.
Madini ya phosphorous kwenye mbegu za maboga ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo.
Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili.

12. AFYA YA MIFUPA.
Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na virutubisho vingine vingi muhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

13. KUWEKA SAWA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU.
Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili muhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.

14. AFYA YA UBONGO.
Mbegu za maboga zina asidi mafuta aina ya OMEGA 3 zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘ALPHA-LINOLENIC ACID’ ambazo ni muhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo.
Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo.

15. TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU.
Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma.
Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito.

16. KUPUNGUZA UZITO.
Mbegu hizi zina uwezo wa kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula kula ovyo.

17. UPONYAJI WA VIDONDA.
Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi.

MATUMIZI:
Unaweza kuzitumia zikiwa kavu yaani baada ya kukauka kwenye jua.
Unakuwa unazitafuna tu kama karanga wala usihofu siyo chungu na unatafuna na maganda yake.

Pia unaweza kuzikaanga kwenye mafuta isizidi dakika tano kama utapenda weka chumvi kidogo kuongeza ladha ila sio lazima.
Tafuna angalau nusu kikombe cha chai kwa siku.

Unweza kuzisaga au kuzitwanga kupata unga ambao utakuwa unauchanganya kwenye juisi yako ya matunda au uji angalau vijiko viwili kwa siku siyo mbaya.
Hata kwa mtoto pia kumchanganyia kwenye uji siyo mbaya hayo ndo matumizi yote kwa tiba unayokusumbua hapo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcOloDcA99sK9fU3ZmYV7nZSyYYDM78wE1viHakIigoqclufq9YOerp6lyBZprD12qXFzEWWHBbVAVt7dPcWMRY4LePDCYOjyxsyloy4E0kXEs6eK0t1UMHi6QWO4O33xt28b3s8Tv9Dc/s1600/MABOGA.jpg

Maandalizi ya Krismas kwa mwaka 2022 yanaendelea kupamba moto. Picha inaonyesha harakati za maandalizi ya sherehe za Krismasi yanaendelea kwa kasi, watu wakijiandaa kwa chakula cha sikukuu

 


Mzee wa kabila moja maarufu huko Kaskazini mwa Tanzania mkoani Kilimanjaro akitokea sokoni kujipatia mbuzi wa kitoweo. Hii ni taswira ya kiutamaduni na kiuchumi, inaonyesha desturi ya kununua mbuzi kwa ajili ya sikukuu. Picha na Emmanuel Minja

#UPENDO 

Pichani ni familia ya mzee Maliaki Barto Nanga Laizer wakiongozwa na mama yao Flora Elimeleck Sandi na Mdogo wake wakiwa katika teto 2022 huko Sinza Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Minja)

 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.Zab 133:1-2