Wednesday, January 16, 2013

Rais wa Zanzibar a lipokutana na Viongozi wanaosimamia zao la karafuu Wete Pemba

Jumla ya shs Billioni 71 wamejipatia Wakulima wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba baada ya kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC)  Karafuu zao zao katika msimu wa Karafuu unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameyaeleza hayo   leo hapo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  alipokuwa akitowa shukrani kwa Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo wakiwamo vikosi vya ulinzi vya Polisi,JKU,KMKM,,ZIMAMOTO,VALANTIA, MAFUNZO, MASHEHA, WANANCHI NA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA  USIMAMIZI WA ZAO LA  KARAFUU ZANZIBAR.
 
 Amesema kuwa kiasi hicho cha Fedha kimo mikononi mwa Wananchi ambapo kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwasaidia sana katika maendeleo yao.
 
Dkt Shein amefurahishwa na juhudi mbali mbali mbali za Maendleo zinazochukuliwa na Wakulima kwa kuweza kujenga Nyumba  za Kisasa baada yakupata Fedha hizo za Karafuu ambapo pia amewataka kuchukuwa kila juhudi yakusafisha  Mashamba yao na  kupanda Mikarafuu mipya.
 
 Aidha Dkt Shein amefurahishwa na juhudi ya pamoja ziliochukuliwa na Viongozi mbali mbali, Wananchi, Masheha pamoja na Vikosi vya Ulinzi katika kuhakikisha kuwa msimu huu zao la Karafuu halitoroshwi kwa njia ya Magendo.
 
Amesema kuwa kosa juhudi za pamoja mafanikio hayo yasingeweza kupatikana ambapo mwaka jana  Mkoa wa Kaskazini Pemba ZSTC ilinunuwa jumla ya Tani 25 .6 tu wakati msimu huo katika Mkoa huo jumla ya tani 2180.5 za Karafuu zimenunuliwa.
   
Ameeleza kuwa kutokana na kazi nzuri iliofanywa safari hii hakuna hata Mkulima moja ,wala taasisi za binafsi na Serikali ambazo inalidai Fedha Shihirika la Taifa ZSTC.
 
Hata hivyo aliliagiza  Shirika la ZSTC kuziangali changamotozilizojitokeza katika msimu huu na baadae kuzipatia ufumbuzi ili msimu ujao uweze kwenda vizuri zaidi
 
 Changamoto hizo ni  kwa Vituo vya kununuwa Karafuu kujitosheleza katika hali zote  zikiwamo sehemu za kujisaidia ,Vifaa vya kukalia na pia kuweka Umeme katika vituo.
  
Mapema Dkt Shein amesema kuwa kwa upande wa Serikali itajitahidi katika kutengeneza Barabara za Vijijini   ili zao  hilo na mengine yaweze kupita bila ya matatizo na kusisitiza kuwa vita dhidi ya Magendo ya Karafuu ni lazima kwa Wananchi kuendelea kupiga vita ili nchi izidi
kufaidika kwa zao hilo am,balo ni tegemeo kwa Uchumi wa Nchi na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment