Saturday, October 21, 2017

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017

SHULE 10 ZILIZOFANYA VIZURI NA ZILIZOFANYA VIBAYA KITAIFA 

Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.


Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.

Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.

Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters - Kagera,
St, Severine - Kagera,
Alliance – Mwanza
Sir. John – Tanga
Palikas – Shinyanga
Mwanga – Kagera
Hazina - Dar es salaam
St. Anne Marie - Dar es salaam
Rweikiza – Kagera
Martin Luther - Dodoma. 

Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni

Nyahaa – Singida
Bosha - Tanga
Ntalasha – Tabora
Kishangazi – Tanga
Mntamba – Singida
Ikolo – Singida
Kamwala – Songwe
Kibutuka - Lindi
Mkulumanzi – Tanga
Kitwai A – Manyara

Saturday, October 7, 2017

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Pombe Magufuli, leo Oktoba 7 amefanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo.

Rais Magufuli pia amegawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake,  na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

Mhe. Magufuli amemteua Mhe. George Haruma Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri wateule wataapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi: Jenista Mhagama, Umi Mwalimu, balozi Augustino Mahiga, Mwakyembe, Kabudi, wamendelea na wizara zao.Seleman Jaffo: TAMISEMI, Katibu wa Bunge: Aondolewa na kuwekwa mpya ndugu Kagaigai, Medadi Kalemani: Wizara ya Nishati
Angela Kairuki: Waziri wa Madini .


Sunday, June 25, 2017

Wadau wa Mkutano wa Elimu wa Umma wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakiwa kwenye viunga vya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu jijini Arusha uliofanyika tarehe 12-17 Juni 2017. Kutoka kulia ni  Afisa Habari wa Muhimbili Patrick J. Mvungi, Elinipa Lupembe PRO Halmashauri ya Manispaa Arusha, Nyamagory Omary Kitwara PRO ofisiya Waziri Mkuu, Florah Mbilinyi PRO Halmashauri ya Meru, Emmanuel Minja Afisa Masoko Mwandamizi TBC na Ndugu Rodrick Ngolly wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Viijijini - IRD Dodoma
Wadau wa Mkutano wa Elimu wa Umma wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakiwa kwenye viunga vya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu jijini Arusha uliofanyika tarehe 12-17 Juni 2017. Kutoka kulia ni  Afisa Habari wa Muhimbili Patrick J. Mvungi, Elinipa Lupembe PRO Halmashauri ya Manispaa Arusha, Nyamagory Omary Kitwara PRO ofisiya Waziri Mkuu, Florah Mbilinyi PRO Halmashauri ya Meru, Emmanuel Minja Afisa Masoko Mwandamizi TBC na Ndugu Rodrick Ngolly wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Viijijini - IRD Dodoma

Monday, April 10, 2017

Kilimo kikitumika kwa usahihi ni mkombozi wa mwananchi. Shime twendeni shambani tukalime,tutokomeze umaskini na njaa. Emmanuel Edwin Minja
MAENDELEO HUJA KWA WATU KUJITUMA .WANA KIKUNDI CHA HAVILA WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUSINDIKA MATUNDA MAENEO YA MARKAZ UKONGA ILALA DAR ES SALAAM. EMMANUEL  MINJA

KIJUE KILIMO CHA MAHINDI YA KUCHOMA (GOBO) PAMOJA NA MCHANGANUO WAKE

                  


Biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo)ni biashara ambayo inaweza kumtoa mkulima kimaisha. Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa tsh 50,000/=, kulima 30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea

hatua husika. Mahindi huchukua wastani wa siku 90 (miezi mitatu) tangu kupanda hadi kugoboa (yaani kuvuna haya mahindi mabichi).

Unaweza kupanda kwa kutumia mvua au kutumia umwagiliaji mahali popote Tanzania. Kwa ekari moja ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata tsh. 1,470,000/= kwa kadirio la chini na tsh. 2,450,000/= kwa kadirio la juu.

Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi tsh 2,140,000/= kwa kadirio la juu. Ukilima eka 5, una uhakika wa faida ya tsh milioni 10.7. Je, ukilima misimu kadhaa, bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza! Unachohitaji wewe ni mambo yafuatayo: utayari, uthubutu, kuwa-up-to-date kwa taarifa za misimu na masoko na uwe ni mtu wa kufuatilia fursa na kujifunza. Fursa zipo 'bwerere', kama una 'allergy' na kilimo tafuta na ujifunze fursa nyinginezo; LAKINI; mtu YEYOTE anaposema fedha ni ngumu, kiukweli anakuwa hayupo "serious" kabisa na haya maisha!
MAISHA NI VITA!


MAMBO YA UJASIRIAMALI HAYO
KILIMO CHA MBOGA MBOGA - KUNDE
''Katika maisha fanya mambo mbalimbali kwa umakini na kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu Utafanikiwa''. Picha iliyoko kulia  ni sehemu ya bustani ya mwanachama wa Kipunguni B Luthen Church SACCOS Ltd ( KBLC SACCOS ) Witness Living Kowero ambaye ameamua kupambana na umaskini kwa vitendo kwa kuanzisha kilimo cha mbogamboga  nyumbani kwake maeneo ya Mazizini Kota Ukonga Dar es Salaam

Wednesday, January 25, 2017







UFUGAJI NA KILIMO KINAHITAJI UVUMILIVU. HAPA NI BI DIGNA MOSHI AKIMWAGILIA BUSTANI YAKE YA MBOGA MBOGA , YEYE PIA NI MFUGAJI WA KUKU.