Tuesday, February 19, 2013



Serikali yamkaanga Sheikh Ponda!
- DPP asema anadaiwa kuhusika na Al-Shabaab, vurugu za Zanzibar
- Ahusishwa na mauaji ya sheikh mmoja kule Mombasa, Kenya
- Polisi yawaonya Waislamu wanaotaka kuandamana kesho (Ijumaa) kwenda kwa DPP
(February 14 2013)
 


MAMBO YA KIJIJINI






 WAKATI wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, Rais Jakaya Kikwete aliahidi kusambaza pikipiki za matairi matatu (bajaj) zipatazo 400,000 katika hospitali, zahanati na vituo vya afya nchini kwa nia ya kusaidia wagonjwa hususani wanawake wajawazito kuwahishwa hospitali wakati wa kujifungua.

Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, Bajaji hizo hazitumiki kubeba wajawazito kama ilivyokusudiwa kutokana na ubovu wa barabara

Endelea kusoma kuhusu hizi Bajaj za Kikwete na changamoto ya Usafiri kwa Wajawazito vijijini



 
 Baba Mtakatifu, Papa Benedict XVI atangaza kuachia madaraka ya kuongoza Kanisa Katoliki duniani Februari 28 Mwaka huu kwa sababu za kiafya.

 

February 11 2013
Mheshimiwa  Tundu Lissu na Mama Anne Makinda wakila good time baada ya kazi ngumu bungeni.Yabungeni yanaishia huko huko.Nje ya mjengo wote sawa!

 

 

February 10 2013

Mambo ya CCM na CHADEMA wakigomea bendera.Inasemekana CCM waliondoa ya CHADEMA ili wasimike yao ndipo mambo yakawa hivi.....Na hii ndiyo Picha ya kufungia wiki hii...
 

February 10 2013

MAMBO YA RAIS WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETA NA JACOB ZUMA.Tufurahie na Rais wetu, tuna mengi ya kujivunia
 

 

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko
- Kwa wastani tikiti maji huchukua hadi SIKU 90 (maximum) kuanzia kupanda hadi kuvuna, kwa mwaka unaweza kulima mara 4, Mbegu ya 'Sugar Baby' hukomaa mapema
- Spacing kati ya mmea na mmea ni 2m x 2m na kila ekari inakuwa na mashimo (mimea) 1,000 kila mmea ukitoa walau matunda 5


  February 9 2013

Bungeni: Wanne watajwa kuwa 'watovu wa nidhamu'!

- Ni Wabunge Tundu Lissu (Singida Mashariki, CHADEMA), Joshua Nassari (Arumeru Mashariki, CHADEMA), Pauline Gekul (Viti Maalumu, CHADEMA) na John Mnyika (Ubungo, CHADEMA)
- Hatua kuchukuliwa dhidi yao...
Nikawaida yao wakishaambiwa ukwel wanadai ni fujo ndan ya bunge,niserikan ya aina gan hii icyo taka kuambiwa ukweli, karne hii ya 20 kwel kaz ipo..

 

 Kwanini hiki kinaitwa "Kibao cha MBUZI?" February 8 2013




February 7 2013

Tanzia: Askofu Thomas Laizer wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini alifariki dunia.


 
R.I.P THOMAS LAIZER.

 February 6 2013 AT NATIONAL STADIUM

FIFA International Friendly Match - Tanzania beats Cameroon!

Full Time Results: Tanzania 1 - 0 Cameroon (Goli limefungwa na Mbwana Samatta)


 Wape maneno Lissu na Ndugai...Msigwa na Nassari watakuwa wanasemaje? February 5 2013

 


January 23 2013 Madawa ya Kulevya Tanzania: Serikali imeshindwa, tufanyeje?

- Vijana wengi wa kitanzania wanazidi kuumia tokana na biashara hii haramu inayowanufaisha wachache huku 'wakiwaua' ndugu zetu
- Baadhi ya wasanii wanadaiwa kuwa watumiaji na kwa namna moja ama nyingine wameathirika kiufanisi
katika usanii wao





January 19 2013 Tanzania: Tume ya Uchaguzi (NEC) yakiri haiko uhuru!

* Yataka iitwe Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
* Yasisitiza isiingiliwe na mamlaka yoyote nchini
* Lubuva: Wajumbe wa tume waapishwe na Jaji Mkuu 
 


 
Guinness World Records kutoka central India imethibitisha kuwa Jyoti Amge mwenye urefu wa inchi 24.7 aliyeshelehekea hivi juzi siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 18, kuwa ndiye mwanamke mfupi kuliko wanawake wengine duniani.
February 2013
 
 January 28 2013

UPDATES: Kutoka Baraza Kuu la CHADEMA - Diamond Jubilee Hall

- Wataka gesi isiondoke Mtwara mpaka serikali iiweke wazi mikataba yote kwa wananchi, Serikali ikae na wananchi ili wapate maridhiano
- Wadai Kinana ni mmojawapo wa Wakurugenzi wa ARTUMAS, hivyo Kinana na CCM wananufaika na mikataba hii
- Wasema 'Wawekezaji wanakaribishwa lakini wawe makini na mikataba ya kifisadi'


 January 28 2013

Breaking News: Lulu (Elizabeth Michael) aachiwa kwa dhamana!

- Baadhi ya masharti aliyopewa Lulu ni pamoja kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20







HIVI HII NI KWELI AU WANAMSINGIZIA MHESHIMIWA?

January 28 2013

Mbunge wa Bukoba Vijijini [Jason Rweikiza (CCM)]: Wanaohoji ahadi zangu ni wagonjwa wa akili!

- Alitoa ahadi ya kuwasomesha watoto watano kila kata ambao wanatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza pamoja na watoto watano kila kata ambao wana umri wa kuanza shule ya awali, ambao alisema kuwa atawasomesha bure hadi darasa la saba
- Asema hakuwa na mkataba nao!







January 25 2013
Gari linalosadikiwa kuwa lilikuwa limeandaliwa kwenda kumchukua Bibi Somoye Issa (90) ambaye ni Mkuu wa Kaya aliyetoa kauli kuwa gesi ikisafirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, itageuka kuwa maji, kuchomwa moto usiku wa jana huko kijijini Msimbati, Mtwara. Kijiji cha Msimbati ndicho ambacho miradi ya kuvuna gesi asilia imesimikwa




Saturday, February 16, 2013


JK AKISALIMIANA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, FREEMAN MBOWE LEO

 b2ap3_thumbnail_8E9U0691.JPG

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akisalimiana na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe wakati wa ibada ya Mazishi ya Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer yaliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati Leo.

 

JK AKISALIMIANA NA MKAPA KWENYE MAZISHI YA ASKOFU THOMAS LAIZER ALIYEZIKWA HUKO ARUSHA JANA IJUMAA TAREHE 15/02/2013 KATIKA  KANISA LA KUU LA KKKT ARUSHA KATI

 b2ap3_thumbnail_8E9U0688.JPG

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa wakati wa ibada ya Mazishi ya Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer yaliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati Leo.

 

 

RAIS KIKWETE AKITETA JAMBO NA WAZIRI MSTAAFU EDWARD LOWASSA LEO KWENYE MAZISHI YA LAIZER

 b2ap3_thumbnail_8E9U0705.JPG

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakati wa ibada ya Mazishi ya Marehemu askofu Thomas Laizer iliyofanyika katika kanisa la KKKT mjjini Kati Arusha LEO.Katikati ni Rais Mstaafu awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi. Picha zote na Freddy Maro.


 b2ap3_thumbnail_nje-ndani.JPG

BAADHI YA VIJANA WAKIANDAMANA KUELEKEA OFISI YA DDP JANA MARA BAADA YA SWALA YA IJUMAA KUSHINIKIZA KUACHIWA KWA SHEIKH PONDA

 b2ap3_thumbnail_maandamano-Wislam.JPG

 Polisi wakitumia staili ya kimyakimya kuwadhibiti Waislamu kwa kupanda magari aina ya Noah kuelekea ofisi za DDP, Elisha Felicia ambako waumini hao walikuwa wanakusanyika kwa kutumia staili yao ya kupanda daladala na wengine kwa kutembea. Waislamu hao wanashinikiza mahakama kumuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake. 

 

NASSARI NA NCHEMBA WAKITETA NJE YA BUNGE ALHAMISI TAREHE 31 JANUARI 2013


 b2ap3_thumbnail_7-Mchemna-na-Nasari.jpg

 Mbunge wa Iramba Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari leo Dodoma katika viwanja vya Bunge- Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.


MAKAMANDA WAKIWA KATIKA MAANDAMANO DAR ES SALAAM


b2ap3_thumbnail_Chadema-leo.JPG





 Maandamano ya Chadema yaliyofanyika Jumapili tarehe kuanzia  Mtaa wa Sokota jijini Dar es Salaam hadi viwanja vya Mwembeyanga Temeke. Maandamano hayo yalifanyika kwa amani, na mkutano  wilayani Temeke.

b2ap3_thumbnail_LULU-10.JPG


LULU AKIINGIA MAHAKAMA KUU JUMATANO 30 JANUARI 2013 KABLA YA DHAMANA KUKAMILIKA


 b2ap3_thumbnail_Waziri-wa-fedha.jpg

 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki(katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Ester Bulaya(kushoto)katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).








































































Monday, January 21, 2013



Michelle Obama rolls eyes at John Boehner, sets Internet a
flame

Monday’s post-inaugural luncheon was a case study in body language--and nearly all of the physical evidence centered on House Speaker John Boehner. One interaction in particular already became an Internet meme: Michelle Obama rolling her eyes after listening to a comment from the Ohio Republican congressman.
Tumblr blogger “Mattyrab” was the first to capture the eye roll in action, sharing video of the exchange in a display described as a “historical moment in shade throwing.” The video has already been shared thousands of times across social media sites with viewers speculating on what sparked the First Lady’s facial expression.
We don’t have audio of their exchange so, for now, it’s impossible to know exactly what Boehner had said. In fact, it’s entirely possible that Michelle Obama's eye roll was simply a reaction to an innocuous joke from Boehner.
That moment was only one of several interactions involving the House speaker. For example, after Boehner’s brief and gracious remarks during the luncheon, he shook hands with President Obama and Vice President Joe Biden. Anyone watching the two exchanges closely would notice a distinct difference: While Boehner and Obama look friendly enough in the actual handshake, at no point do they appear to make eye contact; in contrast, Biden and Boehner appear to share a warmer greeting, smiling at each other and pulling in close.
Of course, any analysis is inevitably colored by one’s own estimation of these three men. But it certainly appears to correlate with the understanding that Biden has far more amicable relations with Congress than Obama.
Interestingly, House Majority Leader Eric Cantor even appeared to have a warmer exchange with Obama after his remarks than the president had with Boehner, as the two men looked each other in the eyes and traded what appeared to be firm, but friendly, greetings. If that indeed is the case, it’s noteworthy since Cantor is viewed as being even more ideologically opposed then the House speaker to Obama’s political agenda.
What do you think? Are political audiences overreacting to Michelle Obama’s facial expression? Or was it a candid moment captured on film showing that even during the most benign of political events, personality conflicts and personal feelings rise to the surface?President Barack Obama, first lady Michelle Obama, and Speaker of the House John Boehner take part in the Inaugural Luncheon. (Reuters)

President Barack Obama, from left, with first lady Michelle Obama, Speaker of the House John Boehner, R-Ohio, and his wife Deborah Gunlack, attend a luncheon after his ceremonial swearing-in on Capitol Hill in Washington, Monday, Jan. 21, 2013. (AP Photo/Manuel Balce Ceneta)

New Book About the First Lady Michelle Obama's FashionMichelle Obama wows at inaugural ball2013 Inauguration

Wednesday, January 16, 2013

Rais wa Zanzibar a lipokutana na Viongozi wanaosimamia zao la karafuu Wete Pemba

Jumla ya shs Billioni 71 wamejipatia Wakulima wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba baada ya kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC)  Karafuu zao zao katika msimu wa Karafuu unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni.
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameyaeleza hayo   leo hapo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  alipokuwa akitowa shukrani kwa Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo wakiwamo vikosi vya ulinzi vya Polisi,JKU,KMKM,,ZIMAMOTO,VALANTIA, MAFUNZO, MASHEHA, WANANCHI NA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA  USIMAMIZI WA ZAO LA  KARAFUU ZANZIBAR.
 
 Amesema kuwa kiasi hicho cha Fedha kimo mikononi mwa Wananchi ambapo kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwasaidia sana katika maendeleo yao.
 
Dkt Shein amefurahishwa na juhudi mbali mbali mbali za Maendleo zinazochukuliwa na Wakulima kwa kuweza kujenga Nyumba  za Kisasa baada yakupata Fedha hizo za Karafuu ambapo pia amewataka kuchukuwa kila juhudi yakusafisha  Mashamba yao na  kupanda Mikarafuu mipya.
 
 Aidha Dkt Shein amefurahishwa na juhudi ya pamoja ziliochukuliwa na Viongozi mbali mbali, Wananchi, Masheha pamoja na Vikosi vya Ulinzi katika kuhakikisha kuwa msimu huu zao la Karafuu halitoroshwi kwa njia ya Magendo.
 
Amesema kuwa kosa juhudi za pamoja mafanikio hayo yasingeweza kupatikana ambapo mwaka jana  Mkoa wa Kaskazini Pemba ZSTC ilinunuwa jumla ya Tani 25 .6 tu wakati msimu huo katika Mkoa huo jumla ya tani 2180.5 za Karafuu zimenunuliwa.
   
Ameeleza kuwa kutokana na kazi nzuri iliofanywa safari hii hakuna hata Mkulima moja ,wala taasisi za binafsi na Serikali ambazo inalidai Fedha Shihirika la Taifa ZSTC.
 
Hata hivyo aliliagiza  Shirika la ZSTC kuziangali changamotozilizojitokeza katika msimu huu na baadae kuzipatia ufumbuzi ili msimu ujao uweze kwenda vizuri zaidi
 
 Changamoto hizo ni  kwa Vituo vya kununuwa Karafuu kujitosheleza katika hali zote  zikiwamo sehemu za kujisaidia ,Vifaa vya kukalia na pia kuweka Umeme katika vituo.
  
Mapema Dkt Shein amesema kuwa kwa upande wa Serikali itajitahidi katika kutengeneza Barabara za Vijijini   ili zao  hilo na mengine yaweze kupita bila ya matatizo na kusisitiza kuwa vita dhidi ya Magendo ya Karafuu ni lazima kwa Wananchi kuendelea kupiga vita ili nchi izidi
kufaidika kwa zao hilo am,balo ni tegemeo kwa Uchumi wa Nchi na Taifa kwa ujumla.


Kilimo kinawezekana tukiunganisha nguvu zetu kwa pamoja








Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,Gilles Muroto (wa tatu kulia) akimtambulisha Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Arusha,Mrakibu wa Polisi (SP),Mary Lugola pamoja na askari wengine wa kitengo hicho mkoani Arusha. (Picha na mahmoud ahmad).




Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,Gilles Muroto akiongea na wananchi wa Mtaa wa Sanawari (hawapo pichani) uliopo kata ya Sekei halmashauri ya jiji la Arusha juu ya uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi


Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto amewaambia wakazi wa Mtaa wa Sanawari waliopo Kata ya Sekei iliyopo halmashauri ya jiji la Arusha waunganishe nguvu zao pamoja ili waweze kuushinda uhalifu.

Hayo aliyasema jana katika mkutano kati jeshi la Polisi na wananchi hao uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo mtaani hapo ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa jeshi hilo juu ya utoaji wa elimu ya polisi jamii kuanzia ngazi ya mtaa na vitongoji vya Mkoa huu wa Arusha.

Mkuu huyo wa Polisi wilaya alisema kitendo cha watu wachache kujitokeza kuhudhuria katika mkutano huo ambao ulikuwa unajadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya mtaa pamoja na masuala ya ulinzi ni dalili tosha kwamba baadhi ya wakazi wa eneo hilo hawana umoja.

“Hii inashangaza yaani mkutano ambao umetangazwa karibu kila nyumba na una lengo la kujadili maendeleo ya mtaa ambao umehudhuriwa na viongozi wa mtaa pamoja na Diwani wa kata lakini watu wachache, hii ni hatari na hamtaweza kusonga mbele.” Alionya Mkuu huyo wa Polisi wilaya.

Alisema hali hiyo ya utengano ndio inayotoa mwanya kwa wahalifu kufanya uhalifu kwani mpaka hivi sasa mtaa huo hauna vikundi vya ulinzi shirikishi kwa kuwa wananchi hawahudhurii katika mikutano ili waweze kushirikiana na jeshi la Polisi kujadili suala hilo.

Mrakibu huyo Mwandamizi wa Polisi alisema kwamba, suala la ulinzi si la kiitikadi za kisiasa bali watu wa vyama vyote wanatakiwa washiriki kwani mhalifu anapovamia sehemu hamuulizi mwenye mali kama ni kiongozi, mwanachama au shabiki wa chama gani bali anaangalia kile anachokiihitaji.

Aliwataka wananchi wa Mtaa huo kuanza kuchukua hatua za kupambana na wahalifu kwa kuanzisha kikundi cha ulinzi shirikishi ambacho kitaendeshwa kwa michango ya kila mkazi ambaye atapaswa kufanya hivyo kwa ajili ya kuwalipa posho walinzi pamoja na ununuzi wa vifaa kama vile tochi, sare na kadhalika.

Aliongeza kwa kusema ili kikundi kikamilike inatakiwa wawe na silaha ya moto ambayo itawasaidia katika shughuli za doria badala ya kutumia marungu pekee. Alisema kikundi hicho kitakuwa kinafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi ambapo pale wanapoona kuna matatizo watakuwa wanawasiliana na yeye au viongozi wengine wa jeshi hilo moja kwa moja ili waongezewe nguvu.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Diwani wa Kata ya Sekei Mh. Chrispin Tarimo, Mwenyekiti wa mtaa huo Godfrey Mollel, Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Mary Lugola, Polisi Tarafa ya Themi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Zuhura na askari wengine toka kitengo hicho ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mkuu huyo wa Polisi wilaya kwa wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya jiji Arusha ya kufanya mikutano na wananchi ili kuimarisha ulinzi ndani ya wilaya ya Arusha.
Maprofesa wakiwa wanaendelea na kazi ya kuchimbua nyayo za zamadamu(WANACHIMBUA NYAYO ZA LAITOLI HUKO NGORONGORO)

JAKAYA KIKWETE NDANI YA LAITOLI NGORONGORO. Hapa Mheshimiwa Rais akiwa anashika nyayo hizo kwa makini ilikuthibitisha kweli ni za watu wa kale waliopita katika kijiji hicho cha Laitoli ndani ya hifadhi ya ngorongoro