Wakulima watakiwa kutumia tafiti
WAKULIMA mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kutumia tafiti mbalimbali za kilimo cha kahawa, ili kuharajkisha jitihada za kufufua zao hilo.Rai hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI), Profesa James Teri, alipokuwa akizungumza na vikundi vya wakulima wa kahawa wa Wilaya ya Moshi Vijijini.
Profesa Teri alisema utafiti ni ghali lakini kama watu wanaamua kuwekeza ,utafiti unalipa vizuri.
Aliwataka wakulima hao kutazama walikotoka na wanakokwenda katika shughuli zao.
Alisema TaCRI ambayo ilianzishwa mwaka 2000 kisheria, imetoa mchango mkubwa katika ufufuaji wa kahawa nchini.
Alisema hata hivyo jitihada hizo zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kutofuata kanuni za kilimo bora na wengine kung,oa kahawa kwa madai kuwa bei yake haitabiliki.
Kuhusu usambazaji wa miche ya kahawa, Profesa Teri alisema TaCRI inawasaidia wakulima kwa kutoa miche ya kuanzisha bustani mama na kuwezesha vikundi mbalimbali mkoani humo.
Akizungumzia usambazaji wa miche hiyo, Mratibu wa Kilimo cha kahawa wilayani humo mViolet Kisanga, alisema kuna vikundi zaidi ya 62 vilivyowezeshwa kupata miche bora.
Kisanga alisema TaCRI imewasambazia wakulima, miche 114,288 iliyowawezesha kuanzisha bustani mama kwenye mashamba 26 yaliyoko kwenye vijiji vya wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment