Balozi Juma Volter Mwapachu ahama rasmi CCM ,arudisha kadi za CCM
Balozi Mwapachu (kulia)
akikabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa Siasa na Uenezi
CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu leo amerejesha
kadi yake ya uanachama ofisi za chama hicho zilizopo Mikocheni A jijini
Dar es Salaam.Balozi Mwapachu aliyetangaza kukihama chama hicho juzi (Jumanne) kwa
madai kuwa kimepoteza dira, amekabidhi kadi hiyo kwa Katibu wa Siasa na
Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba. Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 alisema bado hajaamua ahamie chama gani.
No comments:
Post a Comment