Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kwenye mazishi ya Dkt. Abdallah Kigoda mjini Handeni, Tanga
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi
Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri
huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo
nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu
Dkt.Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015
RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA DK.KIGODA HANDENI LEO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akiungana na
wananchi wa Handeni Mkoani Tanga, katika kumzika aliyekuwa waziri wa
Viwanda na Biashara Dk. Kigoda Rais akiwa na chepe ya mchanga.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGWA MWILI WA MAREHEMU DKT. KIGODA KARIMJEE
Maafisa wa Bunge wakibebea Jeneza
lenye mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati ulipowasili kwenye
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Oktoba 15, 2015 kwa ajili ya
kuagwa.
Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, akizungumza kutoa salamu kwa niaba ya Bunge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi
ya Waumini wa dini ya Kiislamu, kumswalia Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda,
aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati wa swala hiyo
iliyoswaliwa kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es
Salaam, leo asubuhi. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni
kwake Handeni, mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za
mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na
Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa
mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,
leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake
Handeni, mkoani Tanga.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa
heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli
ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo
Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Baadhi ya Wanafamilia wa marehemu Dkt. Kigoda.
Sehemu ya waombolezaji na Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo ya msiba Karimjee.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, wakijumuika na baadhi ya biongozi wa Kitaifa na Waombolezaji,
kushiriki katika shughuli ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda
na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, iliyofanyika leo Okt. 15,
2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mufti
Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, wakati alipowasili kwenye Msikiti wa
Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya
kuswalia mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara, aliyefariki dunia majuzi Hospitali ya Apollo nchini
India, alipokuwa amelazwa akitibiwa. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa
leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Marehemu Dk. Abdallah Kigoda enzi za Uhai wake
MAKAMU wa Rais, Dk.Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda, wameongoza kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, aliyefariki Oktoba 12 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Akitoa pole za rambirambi kwa wafiwa, Spika wa Bunge la Tanzania aliyemaliza muda wake, Anne Makinda, amesema kuwa msiba huo ni pigo la nne mfululizo kwa Bunge la Tanzania tangu kuvunjwa kwake.
Makinda akizungumza leo wakati wa kuuaga mwili wa Kigoda kitaifa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, amesema bunge limepata msiba mkubwa mwingine tangu kuvunjwa kwake ambapo katika uongozi wake limepoteza wabunge 12.
Makinda amesema Dk. Abdallah Kigoda alikuwa ni mtumishi aliyetukuka na hodari aliyeweza kupanua wigo kwa wawekezaji na wafanyabiashara kiasi cha kukuza uchumi wa taifa kwa kutoa ajira na kuchochoea maendeleo ya taifa.
Mwili wa marehemu Kigoda umesafirishwa kwenda nyumbani kwake Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika jioni leo huku ikitarajiwa mazishi hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Kifo cha Kigoda ambaye alikuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Handeni Mjini, kimesababisha kampeni za ubunge mjini hapo kuahirishwa ili kusubiri ratiba mpya ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaruhusiwa kuteua mgombea mwingine.
Mgombea huyo ni wa nne kufariki ambapo wengine ni Mohamed Mtoi wa Chadema aliyekuwa akigombea Jimbo la Lushoto, mwingine ni Celina Kombani wa CCM aliyekuwa akigombea Jimbo la Ulanga na Estomi Malla wa ACT-Wazalendo wa Arusha Mjini.
No comments:
Post a Comment