Update Kuhusu Helikopta ya CCM Iliyoanguka Mbugani Ikiwa na Mbunge Deo Filikunjombe
Mpekuzi blog
Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 majukwaa ya siasa Tanzania yametawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).
Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Nyalandu aliandika;
"Tumetuma
vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous kulikotokea ajali
ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya helikopta imetokea
katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na mashuhuda wanasema
ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha
"Mashuhuda
wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na
walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3,
Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe
na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji
"Mashuhuda
wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema ilianguka
baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia wizara ya
maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na majeruhi
wa ajali ya helikopta Selous usiku huu
"Nimeagiza
section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous) kwenda
eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous)
wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya
helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa Mungu"
Katika
taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri wa
mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita usiku
ilisema: "Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous.
Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye
kampeni ziko salama"
Baadae aliandika :"Kwakuwa
ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya CCM imeanguka,
tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama hakuna
iliyoanguka". Hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandikwa na January
Makamba usiku lakini badae aliretweet kilichoandikwa na Waziri Nyalandu
na Zitto Kabwe.
Zitto aliandika:
"Naomba utulivu.(1) ajali ya helkopta imethibitishwa (2) kuwaka
hakujathibitishwa (3) ndugu yangu Deo alikuwamo (4) hakuna uthibitisho
wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate taarifa rasmi zilizothibitishwa
na mamlaka husika, naomba sana hilo ili kuepuka sintofahamu"
No comments:
Post a Comment