Magufuli afanya kampeni za kuomba nafasi ya Urais Kisarawe Pwani na Moshi Bar Ukonga Dar es Salaam
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano
wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi
Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la
Kisarawe,Ukonga na baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba
na Unguja.
Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Jerry Slaa wakijadiliana jambo.
Wakazi wa Ukonga walivyompokea Magufuli kwa kupiga push up.
Wakazi wa Ukonga wakimshangilia Magufuli baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Moshi bar Ukonga.
wakazi wa Kisarawe wakimsiliza Magufuli alipokuwa akimwaga sera.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Pombe Magufuli baada ya
mapumziko ya Nyerere day leo alianza kampeni kwa kishindo katika viwanja
vya Bomani Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, baada ya mkutano huo
Magufuli alipokelewa kwa hoihoi na vifijo kwenye jimbo la Ukonga ambapo
alikwenda kufanya mkutano uliohudhuliwa na umati mkubwa wa watu kwenye
viwanja vya Moshi bar jimboni Ukonga.Katika mikutano hiyo Magufuli aliwaahidi wananchi hao kutatau mataizo mbalimbali likiwemo suala la kuweka lami kwenye maeneo hayo.
Magufuli alisema atatengeneza barabara mpya kutoka Dar Chalinze mpaka Morogoro ambayo itakuwa na fly over saba. Leo saa saba mchana anatarajia kusaini mkataba mpya wa kuweka fly over pale makutano ya Tazara.
Source : Global Publisher www.global publisher
No comments:
Post a Comment