Friday, July 10, 2015

TANO BORA YA CCM KUJULIKANA LEO DODOMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Dodoma.
Kisu kikali cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo kitaondoka na vichwa 33 kati ya 38 vya walioomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kumrithi Rais Jakaya Kikwete anayemaliza ngwe yake.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula.
Kikao hicho ni hatua ya pili baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati ya Maadili kilichokutana jana usiku chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete huku kikitawaliwa na usiri mkubwa, kuhama ukumbi na kila dalili za kubadili ratiba iliyopangwa awali ili kuvuruga mipango ya kambi za wagombea.

Habari zilizolifikia gazeti hili zilisema kulikuwa na uwezekano wa kubadili ratiba ili vikao vya Kamati ya Maadili na CC ama vifuatane au vifanyike usiku ili kuyanyima makundi nafasi ya kujipanga.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Alipoulizwa jana kuhusu vikao hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alidai kuwa hata yeye hakuwa na uhakika wa lini na muda gani hasa kikao cha Kamati ya Maadili kingefanyika.

Awali, vifaa vya ukaguzi wa wajumbe vilikuwa vimewekwa katika Makao Makuu ya CCM, White House lakini baadaye jioni viliondolewa na hapakuwa na taarifa zozote zilizotolewa.

Habari zilizopatikana baadaye zilidai kuwa kikao hicho cha Maadili kilitarajiwa kufanyika Ikulu ya Dodoma kuanzia saa nne usiku wa jana.

Haya yanajitokeza wakati macho na masikio ya Watanzania yakiwa hapa Dodoma kusikiliza namna kazi ya kuchuja wagombea itakavyofanyika na kujua ni watu gani 33 watakaoanza kulambwa na kisu cha CC, hasa kwa majina makubwa yanayotazamwa na wengi, mara tu baada ya kujadiliwa na Kamati ya Maadili.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kazi za Kamati Kuu leo

Kikao cha CC kina majukumu matatu leo ambayo ni kufikiria na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), majina yasiyozidi matatu ya walioona kuwania urais wa Zanzibar ambayo imeombwa na Rais wa sasa, Dk Ali Mohamed Shein pekee, kufikiria na kutoa mapendekezo kwa NEC majina yasiyozidi matano ya walioomba kuwania urais wa Muungano na kuandaa mkutano wa NEC.

Vigezo vya maadili

Kulingana na kanuni za Uongozi na Maadili, toleo la 2012 kifungu cha 4(ii), kuhusu taratibu za kuomba uongozi, wanachama wanaogombea uongozi ambao uteuzi wao hufanywa na vikao vya kitaifa, watachunguzwa kwanza uadilifu wao na chombo cha maadili cha CCM kwa ushirikiano na vyanzo vingine.

Kanuni hizo zinasema mwanachama wa CCM anapoomba uongozi katika ngazi yoyote, itikadi na mwenendo wake vitachunguzwa kwanza na Kamati ya Usalama na Maadili inayohusika, ndipo maombi hayo yaliyoambatanishwa na mapendekezo ya kamati hiyo yatakapofikishwa mbele ya kikao chenye madaraka ya kutoa uamuzi.
Ikiwa mwanachama hakupendekezwa kwa sababu ya kukiuka Katiba ya CCM, Kanuni za CCM na sheria ya nchi, hatakuwa na haki ya kukata rufaa kwa mtu yeyote au kikao chochote. Lakini ikiwa mwanachama atakataliwa kugombea kwa sababu ya madhambi yake katika chama, basi ni wajibu wa Kamati ya Usalama na Maadili kumjulisha makosa yaliyomnyima haki ya kugombea, naye anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa haki zake kikatiba.

Mtu yeyote anayetuhumiwa mbele ya Kamati ya Usalama na Maadili ya ngazi yoyote, kwa kosa lolote linalohusiana na maadili au nidhamu ya chama atasomewa na kutakiwa kuzijibu tuhuma hizo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo ama kwa kauli yake mwenyewe au kwa maandishi, lakini hataambiwa nani aliyezileta tuhuma hizo, isipokuwa kama imekwishajulikana mapema kutokana na mijadala ya vikao, vyombo vya sheria au vyombo vya habari.

Kanuni ya maadili inaendelea kusema kuwa uchambuzi wa tuhuma hizo utafanywa kwa kutumia njia mbalimbali pamoja na mashahidi watakaopatikana.

Uchunguzi utakapokamilika na endapo itadhihirika kwamba tuhuma zina uzito, mtuhumiwa ataitwa mbele ya kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya ngazi inayohusika, kama ni lazima, ili apate kuhojiwa ana kwa ana.

Pia, kanuni inasema Kamati ya Usalama na Maadili ya ngazi inayohusika itatoa mapendekezo yake kuhusu suala hilo kwenye kikao cha uamuzi kinachohusika. Mtuhumiwa atapewa nakala ya uamuzi kwa maandishi.

Wagombea wanne kukosa CC

Katika kikao cha CC kinachofanyika leo, wajumbe wanne ambao ni miongoni mwa majina 38 yatakayojadiliwa katika mchujo huo watalazimika kukaa kando ili kukwepa mgongano wa masilahi.

Wajumbe hao ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal na Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira.

Kwa mujibu wa Kanuni za Uteuzi wa Wagombea wa CCM katika Vyombo vya Dola, Toleo la Pili – Februari, 2005, ukurasa wa 25, kifungu cha 21 (3); wajumbe wa vikao vya uchujaji na uteuzi wa wagombea kwa ngazi inayohusika hawaruhusiwi kuendelea na kazi ya uchujaji na uteuzi iwapo wao ni wagombea katika ngazi hiyo.

Kanuni hiyo pia imetoa miiko ya shughuli za uchujaji na uteuzi wa wagombea na wajumbe wote wanatakiwa na kanuni kuzingatia maadili na nidhamu ya chama katika kusimamia na kutekeleza shughuli za uteuzi.

Kanuni hizo zinasema ni mwiko kwa kiongozi yeyote kwa maneno au vitendo kumpendelea au kumsaidia kupata kura nyingi mwombaji mmoja dhidi ya mwingine, kutumia au kuhusisha ukabila, dini, rushwa, rangi, hila na eneo analoishi au anakotoka katika shughuli yoyote ya uchaguzi.

Pia, ni mwiko kwa kiongozi yeyote au mwombaji yeyote wa nafasi ya uongozi au mwanachama yeyote aliyekabidhiwa dhamana ya usimamizi au uangalizi au uratibu wa kura za maoni, uchujaji na uteuzi, kufanya vitendo vya ukiukwaji wa kanuni.
Kuhusu misaada, kifungu cha tano (a) kinasema ni marufuku kwa mgombea yeyote mtarajiwa au wakala wake, kufanya vitendo vyovyote vinavyoonekana dhahiri kuwa ni sehemu ya kampeni za kuwania nafasi anayoitafuta kabla ya muda rasmi wa uongozi unaohusika haujamalizika.

Kanuni imetoa adhabu kwa watakaovunja miiko hiyo na kwa kiongozi atakayethibitika kuivunja atavuliwa uongozi na kwa mwanachama anayeomba kugombea nafasi yoyote atakayethibitika kuivunja hiyo hatateuliwa kugombea nafasi anayowania.

Tuesday, May 19, 2015



Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi leo alihutubia wananchi wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano huko mkoani Dodoma ambapo aliitaka Tanzania kuwa karibu kiushirikiano na Msumbiji kwa nyanja zote ikiwemo elimu na biashara.
Rais huyo aliyewasili nchini juzi kwa ziara yake ya kikazi ambapo alikaribishwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.
Baada ya dhifa maalumu iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Nyusi alitembelea Zanzibar na kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambapo waliongea mengi huku wakitaka Zanzibar na Msumbiji zifungue mipaka na kuwa karibu kibiashara.
Baada kutua mnjini Dodoma leo Rias Mbise akiwa na mwenyeji wake rais Kikwete, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kwenda Msumbuji kwa ajili ya kufanya biashara na hata kusomavfani mbalimbali zinazopatikana kwenye vyuo vya nchi hiyo, huku akisisitiza kuimarisha urafiki wao uliodumu kwa miaka mingi sasa tangu nchi hizo kupata uhuru toka mikononi mwa wakoloni.
Naye Spika wa Bunge, Bi Anne Makinda alimpongeza Raisi Nyusi kwa ziara yake nchini ikizingatiwa kwamba hiyo ni ziara ya kwanza kwa Rais huyo kutembelea nchi za nje ya Msumbiji tangu alipotawazwa rasmi kuwa raisi mnamo oktoba mwaka jana

 
Rais Filipe Jacinto Nyusi Amelihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Rais wa Msumbiji Fellipe Jacinto Nyusi leo amelihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema ziara yake imelenga kuja kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili tangu enzi za harakati za ukombozi.

Rais Nyusi amesema hayo leo wakati alikilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini ambapo amesema siku zote maendeleo ya nchi yanatokana na uhusiano mzuri baina ya nchi na nchi.
Bw. Nyusi ambaye anakuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji kuhutubia bunge la Tanzania, amesema kuwa mbali na ushirikiano mzuri wa kisiasa angependa kuendeleza ushirikiano wa kibiashara, elimu na katika nyanja nyingine mbalimbali.
Rais Nyusi ambaye aliingia nchini Juzi ameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kisha akaelekea visiwani Zanzibar ambapo alikutana na Rais wa visiwa hivyo Dkt, Ali Mohammed Shein na leo amemalizia ziara yake Bungeni mjini Dodoma.
Katika hotuba, Rais Nyusi pia ameahidi kushirikiana na Tanzania katika ulinzi wa amani pamoja na vita dhidi ya ugaidi katika mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake spika wa bunge la Muungano Mh. Anne Makinda amesema kuwa ni heshima kubwa kwa Rais huyo wa kwanza wa msumbiji kuhutubia bunge na kuongeza wataendelea kukuza uhusiano baina ya nchi hizo ili kuleta maendeleo ya nchi hizo.
Makinda amesema kumekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa ambao kwa sasa wataendeleza mshikamano kati ya wabunge wa Tanzania na Msumbuji ili kuboresha maisha ya wananchi wa nchiu zote mbili.





Rais Filipe Jacinto Nyusi akipokea shada la maua baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam


Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimkaribisha Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mh. Filipe Nyusi ,Ikulu ya Zanzibar

Rais Kikwete akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Msumbiji zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi








Tuesday, May 5, 2015

Mwenyekiti wa ‪ CHADEMA‬ Freeman Mbowe alivyoungana na DC wa Kinondoni Paul Makonda kutatua mgomo wa Mabasi Ubungo Dar es Salaam '

Mbowe akiwapungia wananchi

 

 

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mh Freeman Mbowe alipokuwa katika stendi ya mabasi Ubungo kuzungumza na madereva ambao walikuwa wakiendelea na mgomo na kuitaka serikali iwasikilize shida zao.
 
Mbowe ambaye aliwasili  majira ya saa nne kasoro robo asubuhi alijikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku wengine wakifuta barabara ili gari yake ipite huku nyimbo za Ukawa zikiimbwa, jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.

Kuhusu mgomo huo mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh PAUL MAKONDA aliwaomba madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakua tayari imeshatoa tamko.

Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba wawe wamesikilizwa kero zao.

Tuesday, May 5, 2015

MGOMO WA MADEREVA WAMALIZIKA-TUME KUUNDWA NA MAJIBU KUPATIKANA NDANI YA SIKU SABA




Mgomo  wa  Madereva  umemalizika baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya viongozi wa madereva, jeshi la polisi na mkuu wa wilaya  ya  Kinondoni.
Akisoma  makubaliano  hayo  mbele  ya  wenzake, kiongozi wa madereva   amesema  kuwa wamekubaliana madai  yao  kutatatuliwa  ndani  ya  siku 7 kupitia  timu  ya  madereva iliyoundwa kushughulikia  madai  hayo pamoja na tume itakayoundwa.
Mabasi ya mikoani kutoka Ubungo sasa yameanza safari baada ya mgomo wamadereva uliodumu kwa  takriban siku 2. 
 
Makubaliano yaliyofikiwa ni kuundwa kwa kamati ya madereva zaidi ya 8 watakaokutana na mkuu wa wilaya kuanzia kesho.
 
Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai yao kwa muda usiozidi siku 7 kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya Paul Makonda.
 

Tuesday, May 5, 2015

Mgomo Wa Madereva: Mbowe Apokelewa Kwa Shangwe Na Madereva Waliogoma Ubungo, Dar

 
 
Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewasili kituo cha mabasi Ubungo na kupokelewa kwa shangwe na Madereva walioko kwenye mgomo
Mgomo huo  leo  umeingia  siku  ya pili na  hali  bado haieleweki kuwa lini mwisho wa ukomo wa mgomo huu kutokana na  ukimya  wa  mamlaka  husika.
 
 



Saturday, January 31, 2015

MUGABE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA AU


Rais Mugabe 
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika Au kwenye mkutano unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia
Wajumbe walimteuwa Rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini kwa kauli moja katika mkutano huo na kumtakia mema kwenye harakati mbalimbali za kuimarisha uchumi wa bara la Afrika.
Mugabe amechukua nafasi hiyo ya Uenyekiti kuziba nafasi inayoachwa na Rais wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wametilia shaka uteuzi huo wa Rais Mugabe kuongoza  Zaidi ya nchi arobaini ambazi ni wanachama wa umoja huo wakieleza kuwa Mwenyekiti huyo mpya hana mahusiano mazuri mataifa ya Magharibi
Shaka hiyo dhidi ya Mugabe pia imejadiliwa na wanasiasa kuwa pengine ikiwa chachu ya maendeleo kwa Afrika kwa kujitawala yenyewe bila kutegemea nchi wafadhili.


 MAKALLA AKAGUA UJENZI WA BWAWA KUBWA LA MAJO CHOLE, WILAYANI KISARAWE


 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akizungumza baada ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa vijiji vya Chole na Kwala, wilayani Kisarawe mkoani Pwani leo. Bwawa hilo linalotarajia Bwawa  limejengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 1.5, linawezo wa kutoa lita milioni 250 kwa mwaka. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Selemani Jaffo



Makalla akikagua ujenzi wa bwawa hilo la Chole


Bwawa la Chole linalojengwa na kampuni ya kitanzania ya Kika


Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Chole, wilayani Kisarawe.




Makalla akimtwisha ndoo ya maji Zena Mwinyihija baada ya kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mengo, wilayani Kisarawe.




Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Chole, wilayani Kisarawe.



Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Makalla akihutubia baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Tanki la maji katika Kijiji cha Chole.






Katibu wa Bodi ya Maji ya Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe, Pwani, Fatuma Chambuso akisoma taarifa ya usimamizi wa mradi wa maji uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Maji katika Kijiji hicho 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chakenge, Mohamed Ndege akimkabidhi zawadi ya mbuzi Naibu Waziri Makalla.




Wananchi wa Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe wakicheza muziki wa Mwanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond Platinamuz' kufurahia kuzinduliwa kwa mradi wa maji uliofanywa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akiungana na wananchi kucheza muziki mpya mdogo mdogo wa Mwanamuziki Diamond, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe, Pwani. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG   August 01, 2014