Rais Mugabe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika Au kwenye mkutano unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia
Wajumbe walimteuwa Rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini kwa kauli moja katika mkutano huo na kumtakia mema kwenye harakati mbalimbali za kuimarisha uchumi wa bara la Afrika.
Mugabe amechukua nafasi hiyo ya Uenyekiti kuziba nafasi inayoachwa na Rais wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wametilia shaka uteuzi huo wa Rais Mugabe kuongoza Zaidi ya nchi arobaini ambazi ni wanachama wa umoja huo wakieleza kuwa Mwenyekiti huyo mpya hana mahusiano mazuri mataifa ya Magharibi
Shaka hiyo dhidi ya Mugabe pia imejadiliwa na wanasiasa kuwa pengine ikiwa chachu ya maendeleo kwa Afrika kwa kujitawala yenyewe bila kutegemea nchi wafadhili.
No comments:
Post a Comment