MAKALLA AKAGUA UJENZI WA BWAWA KUBWA LA MAJO CHOLE, WILAYANI KISARAWE
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akizungumza baada ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa vijiji vya Chole na Kwala, wilayani Kisarawe mkoani Pwani leo. Bwawa hilo linalotarajia Bwawa limejengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 1.5, linawezo wa kutoa lita milioni 250 kwa mwaka. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Selemani Jaffo
Bwawa la Chole linalojengwa na kampuni ya kitanzania ya Kika
Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Chole, wilayani Kisarawe.
Makalla akimtwisha ndoo ya maji Zena Mwinyihija baada ya kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mengo, wilayani Kisarawe.
Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Jaffo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Chole, wilayani Kisarawe.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Makalla akihutubia baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Tanki la maji katika Kijiji cha Chole.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chakenge, Mohamed Ndege akimkabidhi zawadi ya mbuzi Naibu Waziri Makalla.
Wananchi wa Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe wakicheza muziki wa Mwanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond Platinamuz' kufurahia kuzinduliwa kwa mradi wa maji uliofanywa na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akiungana na wananchi kucheza muziki mpya mdogo mdogo wa Mwanamuziki Diamond, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Chakenge, wilayani Kisarawe, Pwani. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG August 01, 2014
No comments:
Post a Comment