Wednesday, March 19, 2014

Ridhiwani Kikwete na Mbio za kusaka Ubunge  wa Jimbo la Chalinze

Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Steven Kazidi (kushoto) akimuinua mkono juu kwa ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo jana Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubi wananchi wa Kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo,wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni zake ulioanza rasmi jana Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubi wananchi wa Kijiji cha Saadani,Wilayani Bagamoyo.wakati wa kampeni zake zilizoanza rasmi jana Machi 14,2014.
Baada ya kumaliza Mkutano na Wananchi wa Kijiji cha Matipwili,Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete alifika katika Kijiji cha Gongo ndani ya Tarafa ya Saadani na kukutana na wananchi wa Kijiji hicho na kuzungumza nao kama aonekanavyo pichani.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wanakijiji wakazi wa Kijiji cha Mkange,Saadani Wilayani Bagamoyo waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza huku wengi wakiahidi kumpa kura zao pindi itakapofika siku ya Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo.
Diwani wa Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze,Said Zikatimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Gongo,huku akiwataka kutofanya ajizi pindi itakapofika siku ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,hivyo kura zao zote wampigie Mgombea wa CCM ambaye ni Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Diwani wa Kata ya Mkange,Ndg. Abdallah Mwendali nae hakuwa nyuma katika kuwasisitiza wananchi wa Jimbo la Chalinze.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akinong'onezwa jambo na Mmoja wa kinamama wa Kijiji cha Matipwili (Jina lake halikuweza fahamika mara moja).
"Ni furaha tupu" Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahia jambo na wanakijiji wa Matipwili.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na Wanakijiji cha Mkange,wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mkutano.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na Sheikh wa Kijiji cha Mkange.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na rafiki yake wa kitambo.
Mwenyekiti wa Kampeni katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Saleh Mpwimbwi akimmwagia sifa kede kede Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete .




JAJI WARIOBA AWASILISHA RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA BUNGE MAALUM LA KATIBA,March 18, 2014



JAJI WARIOBA ASEMA ILI KUUFANYA MUUNGANO UWE IMARA TUNAHITAJI SERIKALI TATU

PG4A2542

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba akiwasilisha Rasimu ya Katiba  mpya mbele ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, bungeni mjini Dodoma Machi 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Warioba akata ngebe za CCM

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amezima rasmi sakata la makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulazimisha Bunge Maalumu la Katiba kukataa pendekezo la Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba bungeni jana, Jaji Warioba alisema uchambuzi uliofanywa na tume yake umezingatia maoni ya wananchi, historia  na hali halisi, na kwamba ili muungano udumu serikali tatu hazikwepeki.
Alisema tume ilitafakari maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananachi na makundi, na ilirejea ripoti kadhaa za miaka zaidi ya 20 mfululizo, ikazingatia malalamiko ya Zanzibar na Tanganyika, mgongano wa kikatiba kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, na mengine mengi.

 PG4A2567

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya  Mabmadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) baada ya Mwenyekiti huyo kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya bele ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bungeni Mjini Dodoma Machi 18, 2014.Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba, Samia Suluhu (kuli), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Profesa  Anna Tibaijuka,  Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (watatu kushoto) na  watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani  , Mathias Chikawe. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Shivji na Mtizamo wa Muundo wa Serikali
Mwandishi Wetu
Raia  Mwema .Toleo la 300 , 26 Jun 2013
WAKATI Profesa Issa Shivji akihoji asili ya wazo la serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya ambayo imejenga uhalali wake kutokana na hati ya Muungano ya mwaka 1964 inayotaka serikali mbili, Jaji Joseph Warioba, amewatolea uvivu wakosoaji wa rasimu hiyo, Raia Mwema linaripoti.
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Warioba ameelezea kufurahishwa zaidi na ukosoaji wanaopendekeza pia mbadala wa kile wanachokikosoa kutoka katika rasimu hiyo ambayo itajadiliwa kwa kina katika mabaraza ya katiba hivi karibuni.
“Tumetoa rasimu, tunataka mawazo ya watu kwa sababu tulipokwenda kwao tulichukua maoni ambayo pengine katika rasimu hii hayapo au yapo kwa sababu tulichambua na kuchagua maoni hayo. Watoe maoni yao kwa uhuru, lakini si kukosoa tu pekee, bali wakosoe na kupendekeza. Ukikosoa pekee haitusaidii sana.
“Lakini hadi sasa katika hatua hizi za awali mara baada ya kutolewa rasimu, tunaridhika na mchakato na kwa kweli ndicho tulichotarajia, ukosoaji na maoni mengine mbadala,” alisema Warioba.
Mtazamo huo wa Warioba unajitokeza ikiwa ni takriban wiki moja tangu Profesa Issa Shivji, ambaye ni gwiji wa masuala ya katiba na sheria, awasilishe mada juu ya rasimu hiyo katika kongamano la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Juni 21, mwaka huu, katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kati ya ukosoaji aliofanya Profesa Shivji ni pamoja na kuhoji uhalali wa mapendekezo ya serikali tatu, katika rasimu ambayo inajieleza kujenga nguvu zake kutokana na hati ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, ya mwaka 1964.
Katika mada yake ambayo imeanza kuchapishwa na gazeti hili kwa awamu, Shivji anasema hati ya makubaliano ya 1964 ni msingi wa rasimu ya katiba na katiba hiyo ni mwendelezo wa makubaliano hayo.
“Ukiangalia kwa jicho la kisheria, ukisema Hati ndio msingi, maana yake ni kwamba Hati bado inaendelea kuwa na nguvu ya kisheria na ndiyo sheria kuu inayotawala Katiba. Lakini Hati iliweka serikali mbili; sasa, iweje rasimu inayozungumzia serikali tatu iwe na msingi ambao ulijengeka kwenye serikali mbili?
“Katiba iliyojikita kwenye serikali tatu haiwezi, kwa vyovyote vile, ikawa mwendelezo wa Hati. Ni kweli kabisa kwamba Hati ya Makubaliano ya 1964 ni chanzo cha Muungano. Historia hii, kama inavyostahili, imewekwa kwenye Utangulizi (wa rasimu). Lakini masharti ya katiba yenye nguvu za kisheria hayawezi tena kurudia historia.
“Ukitaja maneno kama haya katika masharti ya Katiba, kimahakama inachukuliwa kwamba nia yako ilikuwa kuipa Hati nguvu ya kisheria. Nina uhakika kabisa kwamba haikuwa nia ya Tume kuifufua Hati ya 1964 na kuipa nguvu ya kisheria.
Pia, ninaamini kabisa kwamba Tume iliyosheheni wanasheria wazoefu na waliobobea huenda walijua na kuelewa kabisa walichokuwa wanaandika.
“Kwa hivyo, haiwezekani kwamba walikosea, au kuteleza, bali ilikuwa ‘kusalimu amri’ na “kuelewana” ili mambo yaendelee. Ndivyo tulivyopata ibara legelege ambayo kisheria haina kichwa wala mkia,” anasema Shivji.
Ingawa Shivji hakutaja kwa majina watalaamu wenzake wa sheria walioko katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini ni dhahiri alikuwa akiwazungumzia Profesa Palamagamba Kabudi, Dk. Sengodo Mvungi, Said El Maamry na wengine.
Hata hivyo, wakati Shivji akihoji uhalali wa rasimu ya Katiba kupendekeza serikali tatu kinyume cha Hati ya Makubaliano, habari za uhakika zinaeleza kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kipo katika mvutano wa ama kuweka wazi msimamo wake kuhusu idadi ya serikali zinazotajwa kwenye rasimu ya Katiba ama kuwaachia kwanza wanachama wake kuamua kwenye mabaraza ya Katiba.
Kutokana na mvutano huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameitisha ‘kimyakimya’ Kamati Kuu ya chama hicho ili kufikia uamuzi wa pamoja wa ama kuweka wazi msimamo wake wa idadi ya serikali ndani ya rasimu ya Katiba ama la.
Gazeti hili limetaarifiwa kwamba sehemu kubwa ya wanachama wa chama hicho wanashinikiza chama chao kuweka msimamo na kutamka wazi kinaunga mkono serikali mbili, na si tatu, tofauti na vyama vingine, kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Lakini msomi mashuhuri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, naye amekosoa rasimu ya Katiba mpya akisema imeshindwa kuwabeba vijana, akirejea suala la ukomo wa umri katika kugombea nafasi za urais na hata ubunge na maelezo yake hayo yamechapishwa kwa kirefu katika gazeti hili.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba mara kadhaa, baada ya kuzinduliwa kwa rasimu ya Katiba, alikaririwa akiunga mkono rasimu hiyo kwa kiwango kikubwa.
Ingawa rasimu hiyo ya Katiba mpya imependekeza masuala mbalimbali mapya katika utawala nchini, lakini mjadala mkali umekuwa ukijikita zaidi katika idadi ya serikali, wengine wakiunga mkono serikali tatu kama ilivyopendekezwa na wengine wakipinga.











Sunday, March 16, 2014



Jana March 13 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ilitoka stori iliyowahusisha Wagombea Ubunge jimbo la Chalinze ambao ni Fabian Leonard Skauki wa CUF na Matheo wa  Chadema juu ya kusemekana kuwa Mathayo Mang’unda Torongey aliongopa kwenye ujazaji wa fomu zake za kugombea Ubunge jimbo hilo.

Leo millardayo.com imefika tena hadi Bagamoyo makao makuu ya wilaya Chadema kwa ajili ya kufahamu undani wa madai hayo ya Mgombea wa Cuf ambapo Matheo ameanza kwa kusema>>’kwanza labda niweke sawa zile fomu hakuna sehemu ambayo inasema uambatanishe na vielelezo vya shughuli unayofanya’
MATHEO
‘Kiuhalisia mimi ni mfanyabiashara wa siku nyingi nafanya biashara na maduka ya nyama kuhusu kughushi sahihi ya wadhamini hili ni suala ambalo sio la ukweli kwa sababu wakati  tunarudisha fomu ilihakikiwa na mkurugenzi ambae ndiye msimamizi wa uchaguzi’
‘Na sio saini za mkono peke yake zipo za dole gumba na zipo mchanganyiko na tunazo pia zile shahada za wapiga kura,tulifanya uhakiki na shahada zenyewe hivyo mkurugenzi alihakiki na kusema zipo sawa sawa’

‘Kuhusu kusema kuwa mimi sio Mtanzania hilo suala sio la kwangu nafikiri la uhamiaji au wanalo wenyewe lakini mimi ni Mtanzania halalai na ninacho kitambulisho cha kupigia kura ambacho nafikiri watanzania wengi wanakitumia’
CHANZO:MILLARDAYO.COM


Mgombea Chadema Chalinze apingwa

By Waandishi wetu;   14th March 2014

Mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze, Pwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Fabian Skauki, amemwekea pingamizi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey kwa msimamizi wa uchaguzi, akisema hana sifa za kugombea.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zililifikia NIPASHE jana, mgombea wa CUF ametaja sababu kadhaa zilizomfanya amwekee pingamizi mgombea wa Chadema kuwa ni pamoja na kutojua kusoma na kuandika lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Katika pingamizi hilo ambalo liliwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Chalinze, Skauki alidai kuwa mgombea huyo wa Chadema amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza wakati ni uongo.

“Mgombea wa Chadema amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza wakati ni uongo, hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala Kiingereza, amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea,” alisema Skauki katika pingamizi hilo.

Sababu nyingine iliyoelezwa ni kwamba mgombe wa Chadema amedanganya kwa kughushi sahihi za wadhamini, ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea.

Alidai kuwa katika fomu hizo wadhamini wote na sahihi zao zimeghushiwa na hazifanani na kwamba zile zilizokuwapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura sahihi zote zimesainiwa na mtu mmoja ambaye siyo mhusika.

Sababu ya nne ni kwamba mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini saba siyo wapiga kura halali wa jimbo la Chalinze, hivyo wadhamini halali ni 21 ambao hawafikii idadi  inayotakiwa.

Kadhalika, Skauki anadai katika pingamizi lake dhidi ya mgombea wa Chadema kwamba katika fomu zake alisema kuwa shughuli anazojihusisha nazo ni biashara, lakini hakuonyesha vielelezo kuthibitisha.

Vile vile, Skauki anadai kwamba Torongey siyo raia wa kuzaliwa Tanzania kwa kuwa hakuna vielelezo alivyowasilisha kuthibitisha kama ni raia wa kuzaliwa.

Baada ya kutoa tuhuma hizo, aliiomba Tume ya Uchaguzi (NEC) kutengua uteuzi wa Torongey kwa kuwa anakosa sifa za kuendelea kuwa mgombea.

Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi jimbo la Chalinze, Hoza Mohamed, alithibitisha kupokea pingamizi la mgombea wa CUF na kusema kwamba ofisi ya msimamizi inashughulikia suala hilo kwa ajili ya kutoa maamuzi.

“Ni kweli nimepokea pingamizi kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na hivi sasa tunalifanyia kazi,” alisema Mohamed.

Hata hivyo, Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Nickson Tugara, alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa mgombea wa CUF anatapatapa kwa vile anajua nafasi hiyo itachukuliwa na Chadema.

“Sisi hatujaweka wadhamini mamluki, bali ni watu wenye sifa ambao wako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na pia Chadema imefuata taratibu zote kwa kwenda mahakamaani na Halmashauri ya Bagamoyo kuwalipia gharama za fomu,” alisema Tugara.

Alisema kuwa majina ya wadhamini na sura zao zipo kwenye kompyuta za halmashauri, hivyo anachofanya mgombea kupitia CUF ni kutapatapa na hajui taratibu za kisheria zinavyokwenda.

“Mgombea wetu anajua kusoma na kuandika na ana sifa zote za kuwania nafasi hiyo, ila CUF wamepanga kumchafua na hawataweza kwani Chadema tuko makini tunaposimamia mambo yetu na tutazindua kampeni zetu Machi 16,” alisema.

Meneja kampeni wa mgombea wa Chadema, John Mrema, alisema wamepata taarifa za kuwekewa pingamizi mgombea wao, lakini alisema ofisi ya msimamizi wa uchaguzi bado haijatoa taarifa rasmi kwa Chadema.

Mgombea mwingine katika uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu ni Ridhiwani Kikwete kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo Januari 22, mwaka huu.
SOURCE: NIPASHE




Friday, March 14, 2014




MATREKTA KWA AJILI YA KUFANIKISHA SHUGHULI ZA KILIMO

Wabunge 42 Chadema kufunika kalenga

Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo vimeendelea kuchuana katika wiki ya lala salama ya kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa kwa kumwaga makada wa kitaifa na vijana wa kulinda kura.

 Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe na wabunge 42 wa chama hicho wameitwa na Katibu Mkuu wake,  Dk. Willibrad Slaa, kuongeza nguvu kwenye kata 13 za jimbo hilo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jumapili ijayo.

Meneja kampeni wa chama hicho na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, akizungumza jana wakati akimnadi mgombea wa chama chake, Grace Tendega, katika Kijiji cha Magulilwa alisema uamuzi huo unalenga kupambana na hujuma za wizi wa kura unaoweza kufanywa na mahasimu wao kisiasa.

“Mwenyekiti na wabunge wengine 42 kesho (leo) watakuwa  wameshasambazwa kila kata ya jimbo hili kwa ajili ya kuongeza nguvu. Hawa CCM bila kuwadhibiti kwa staili hiyo watatuumiza. Kwa hiyo tayari Dk. Slaa ameshawaita na mtakutana nao huko kwenye maeneo yenu wakiwaomba mumchague Tendega (Grace) kuwawakilisha bungeni,” alisema Lema.

Alisisitiza kwamba ili kuhakikisha Tendega anatwaa kiti hicho, wabunge wenzake wamechangishana kila mmoja Sh. milioni mbili kwa ajili ya kumwongezea nguvu ya kupambana na mahasimu wake kisiasa.

MANGULA KUONGOZA CCM

Wakati Chadema ikiongeza nguvu, wapinzani wao CCM, wamesema hawana mpango wa kuongeza wapiganaji kutoka nje ya mkoa wa Iringa kwa kuwa makada pamoja na vikosi vyake ambavyo kwa sasa vinaongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula, vina uwezo mkubwa wa kukabiliana na wabunge, makada na wafuasi wa Chadema.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye, aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu jana kwamba hawana mpango wa kuongeza nguvu wala kukodi watu kutoka mikoa mingine ili kukabiliana na wapinzani wao katika wiki ya lala salama kuelekea uchaguzi huo.

“Mzee Mangula anatosha kuwaumbua Chadema katika uchaguzi wa Kalenga kwa sababu anayo timu iliyokamilika huko Kalenga na hatuna sababu ya kuongeza nguvu kama Chadema wanavyofanya hivi sasa. Nawahakikishia Watanzania kwamba CCM itatwaa kiti cha Kalenga Jumapili ijayo,” alisema Nape.

MANGULA AISHANGAA CHADEMA
Naye Mangula akimnadai mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa, kwenye vijiji vya Tosamaganga na Kalenga, wilaya ya Iringa Vijijini jana, alisema wamejipanga kulinda wapiga kura wake kwa kutumia vijana zaidi ya 260 ambao  wamesambazwa katika kata zote 13 za jimbo la Kalenga kwa uwiano wa  vijana 20 kila kata.

Alisema anawashangaa Chadema kwa  kupeleka idadi kubwa ya makada kutoka nje ya Kalenga, magari 75 na helikopta mbili kwa kisingizio cha kulinda kura wakati jukumu hilo ni la Jeshi la Polisi pamoja na mawakala wa vyama vya siasa ambao watakuwapo ndani ya vituo kwa ajili ya kila mmoja kuhakiki kura za mgombea wake.

 “Nawashangaa sana Chadema kwa kuleta makada 1,000 na magari 75 pamoja na helkopta mbili kwa kisingizio cha kulinda kura wakati kila kituo kitakuwa na mawakala wa kila chama kwa ajili ya kuhakiki kura zao,” alisema Mangula.

CHIFU KULINDA KURA ZA CHADEMA

Katika hatua nyingine, uchaguzi ambao umeugawa ukoo wa Chifu wa Kabila la Wahehe baada ya Naibu Chifu, Gerald Malangalila, kutangaza kukiunga mkono Chadema na kwamba  atakuwa mmoja wa mawakala watakaosimamia kura za mgombea wa chama hicho.

“Nimeanza mageuzi ya kifikra katika mikutano tisa niliyoifanya kwa helkopta jana, lakini pia nasema wazi wazi kwamba mimi ni mmoja wa mawakala wa Grace Tendega siku ya Machi 16. Ndugu zangu, kwa Wahehe, uchifu unarithiwa lakini ubunge haurithiwi...na kwa namna ya pekee, nimejitosa kulinda heshima yetu isivurugwe na mtu yeyote kwa sababu ya tamaa ya madaraka,” alisema Malangalila akimnadi mgombea huyo katika kijiji cha Mgama.

Februari 19, mwaka huu, wakati Chadema wanazindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Kalenga, Chifu wa Kabila la Wahehe, Mtwa Mfuwimi wa II, Abdul Adam Sapi Mkwawa, alivitaka chama hicho na CCM kuendesha kampeni zao kistaarabu bila ya kuruhusu vurugu wala umwagaji damu.

 Wiki moja baadaye, akiwa katika uzinduzi wa kampeni za CCM, Chifu Abdul Mkwawa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Igwachanya, Kata ya Mseke, alisema anakiunga mkono chama hicho na kutoa baraka kwa mgombea wake, Mgimwa kuvaa viatu vya ubunge vya marehemu baba yake, Dk. William Mgimwa.

 Wakati huo huo; Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Wilaya ya Iringa Vijijini, Bonus Kivawo, amejitosa pia kumnadi mgombea wa Chadema huku akiahidi pia kuwa mmoja wa mawakala wake katika Kijiji cha Magulilwa ambacho pia yeye ni Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho.

Uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha Kalenga unafanyika kujaza nafasi iliyoachwa na Marehemu Dk. Mgimwa, aliyefia hospitali ya Kloof Med- Clinic mjini Pretoria, Afrika Kusini Januari mosi mwaka huu


TASWIRA ZAIDI ZA KAMPENI ZA UBUNGE KALENGA

Meneja Kampeni wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Alphonse Mawazo, akicheza ngoma ya jamii ya kimasai baada ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Grace Tendega Mvanda, jana asubuhi. 


Mzee wa Mila wa Kimasai katika Kijiji cha Mfyome, Lioper Ilmuduji, akimpatia baraka mgombea ubunge  wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda, wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyuma kuomba kura kwa wananchi katika kijiji hicho jana asubuhi.

. Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda akishiriki chakula cha kimila pamoja na watu wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Mfyome jana asubuhi baada ya msafara wa mgombea huyo kufika kijijini hapo kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.

Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Grace Tendega Mvanda, akizungumza kuomba kura wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu katika Kijiji cha Mfyome, jana asubuhi.


TASWIRA ZA KAMPENI YA UBUNGE KALENGA

Mgombea akipokelewa Lumuli

Heche akihutubia Lumuli;

Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.

Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.






Rais Dkt. Kikwete na Viongozi wa Bunge Maalum la Katiba Dodoma.March 14, 2014

D92A4522











































Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu na naibu katibu wa Bunge maalum la Katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha katika ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.Kushoto ni Katbu Wa Bunge hilo Bwana Yahya Khamis Hamad na kulia ni Naibu Katibu Dkt.Thomas Kashililah.


D92A4644

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho(picha na Freddy Maro).

D92A4568

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta(kushoto) na Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu(kulia) wakati wa hafla  ya kuwaapisha katibu na naibu katibu wa Benge maalum la katiba zilizofanyika katika viwanja vya ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi



Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakiingia bungeni mjini Dodoma jana kuhudhuria semina ya kuchangia taarifa ya Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa Muda wa Bunge kuhusu Kanuni.

Samia achaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bunge maalum la Katiba



IMG_4141

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akitoa shukrani zake kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.

IMG_4129

Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akimpongeza Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutangazwa kuwa Makamu mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.

IMG_4024

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge Hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.



































Wednesday, January 8, 2014

Mstahiki  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Aman Mwamwindi  akizungumza na wanahabari  leo kuhusu  mambo mbali mbali yanayoendelea







HALMASHAURI  ya  Manispaaa ya  Iringa  imepiga marufuku ujenzi  holela  unaoendelea  katika milima ndani ya mji wa Iringa .
 Kauli  hiyo  imetolewa leo na mstahiki meya  wa Halmashauri  ya  Manispaa ya  Iringa Amani  Mwamwindi wakati  akizungumza na wanahabari  ofisini  kwake. 
Alisema   kuwa  udhaifu  wa  usimamizi  wa sheria  katika maeneo mbali mbali ndio  umepelekea  ujenzi  holela  kuendelea.
Hata  hivyo  alisema nyumba  ambazo  zinajengwa  kiholela  katika mji  wa Iringa zitaendelea  kuvunjwa  iwapo itabainika  kuwa  zimejengwa kiholela.
Kuhusu  uwekezaji  alisema  kuwa  vipo  viwanja kama  vitatu ambavyo  vinahitaji uwekezaji na  hivyo  kuwataka  wananchi  kujitokeza  kuwekeza katika maeneo hayo. 
 
 IMG_0892

 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Jipya la Kiswahili






RAIS KIKWETE AKUTANA WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Januari 7, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na  Migodi  wa Algeria Mheshimiwa  Youcef Yousfi ambaye yuko katika ziara ya siku sita nchini.
Katika ziara hii, Mheshimiwa Yousfi na ujumbe wake unaojumuisha viongozi wa mashirika ya umma, wanatarajia kutembelea kituo cha umeme cha Gridi ya Taifa cha Ubungo mjini Dar es Salaam, ujenzi wa bomba la gesi katika eneo la Vikindu na Mkuranga mkoani Pwani, machimbo ya Mererani  na Minjingu mkoani Manyara.
Rais Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akisisitiza kwamba Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki na washirikia wa karibu wa siku nyingi katika masuala ya siasa na uchumi, kufuatia  misingi imara iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Ahmed Ben Bella,
Rais amebainisha kwamba ushirikiano wa nchi hizi mbili  ni muhimu sana sio tu katika kuendeleza uhusiano wao wa  muda mrefu, bali pia katika  uwekezaji na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
Alisema Rais: "Tunahitaji washirika wazoefu, waaminifu na wenye ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi kama Algeria katika kuendeleza sekta hiyo ambayo ni mpya kwetu”.
Alitolea mfano wa uzoefu wa miaka mingi wa Algeria katika uchimbaji na usafirishaji wa gesi asilia katika mradi wa bomba la gesi la Maghreb–Europe, unaounganisha machimbo ya gesi ya Hassi R'Mel nchini Algeria, na kusafirisha gesi asilia hadi nchi za Morocco, Hispania na Ureno
"Tanzania itanufaika sana na juzi na uzoefu wa Algeria katika sekta ya gesi hasa katika wakati huu ambapo Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) limepewa jukumu la kujiendesha kibiashara hivyo linahitaji washirika mahiri", alisema Rais
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
07 Januari, 2014
 
Hili ni gari  la JWTZ lililobeba mwili wa  waziri Dr Wiliam Mgimwa  kutoka uwanja wa Ndege Nduli hadi kijiji cha Magunga nyumbani alikozaliwa
 
 Ndege aliyotumia  rais  Dr Jakaya  Kikwete ikitua  uwanja wa ndege nduli Iringa


 
 Msafara  wa waziri mkuu Mizengo Pinda  ukiwasili  uwanja waNdege Nduli  Iringa



 Mafundi  ujenzi  wakijenga kaburi la Dr Mgimwa


 

 

 Barabara  iliyetengenezwa kwa ajili ya ugeni wa kitaifa   japo eneo hilo la barabara ya Masumbo - Kiponzero lilikuwa korofi  siku nyingi
 
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuwasili nyumbani kwa Dr Mgimwa kijiji cha Magunga
 .......................................................
WAKATI  Rais wa jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete akiwa katika mtihani wa  kuziba nafasi ya  aliyekuwa  waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa aliyezikwa  juzi kijijini kwake Magunga Kalenga wilaya ya Iringa , wabunge na  mawaziri mbali mbali wameibuka na kumzungumzia Dr Mgimwa   huku mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akidai kuwa kati ya mawaziri  wasikivu kwa  wabunge alikuwa ni Dr Mgimwa na kuwa hakuwa na ndoto ya  kumshambulia ama kumsema vibaya bungeni.

Akiungumza  mahojiano maalum na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com juu ya   kifo  cha Dr Mgimwa  kilichokuwa  kikirushwa moja kwa moja na Radio Nuru Fm  iliyopo mkoani Iringa , Mbunge  Filikunjombe  alisema  kuwa  mbali ya  kuwa wananchi  wa  jimbo la Kalenga  wamempoteza mbunge mchapa kazi  ila bado Taifa  limempoteza  waziri  mwadilifu zaidi.

Kwani  alisema  kwa  kipindi  chake  chote  cha uwaziri  alikuwa ni msikivu na mwenye  kupenda  kushauriwa na kila mmoja  katika  kuitumikia nafasi  hiyo  na kuwa Dr Mgimwa alikuwa ni tofauti na  mawaziri  wengine ambao  wameendelea  kuikwamisha  serikali  ya  rais Dr Jakaya  Kikwete kwa kutokuwa  wasikivu .

Filikunjombe  ambae   alipata  kumshambulia bungeni  aliyekuwa  waziri  wa  fedha kabla ya Dr Mgimwa Bw  Mustafa Mkullo kwa  kushindwa  kutoa  fedha kwa  wakati kwa ajili ya kununua mahindi ya  wananchi  wa Ludewa ,alisema  kuwa  Dr Mgimwa kwa  kila  jambo ambalo alikuwa akielezwa na  wabunge alikuwa akiwatekelezea kwa  wakati.

"Binafsi  nimeumia  sana na kifo cha Dr Mgimwa  kwani katika ndoto  zangu za mbeleni sikufikiria  kuja   kutofautiana na waziri Dr Mgimwa ... kwani alikuwa ni mtu wa kujishusha na  kutenda na sio  kujisikia na  kupuuza mambo"

Filikunjombe  alisema  pia  la kifo  chake  linaumiza  wengi ambao  walipata  kufanya nae kazi kwa karibu wakiwemo  wabunge .

Naibu  waziri  wa chakula na ushirika  Adam Malima  alisema  kuwa siku  zote  Dr Mgimwa alikuwa  ni wa mfano  katika utendaji kazi wake na kuwa kati ya  viongozi  waadilifu katika Taifa pia  alikuwa  ni mmoja  wapo.

Alisema  Dr Mgimwa alikuwa akiishi maisha ya  kawaida  sana  ukilinganisha  na wengine na  kuwa hakupenda  kujilimbikizia mali ila alipenda  zaidi kulitumikia Taifa lake kwa nafasi aliyokuwa nayo ya  uwaziri na kuwatumikia  wana Kalenga kwa nafasi yake ya ubunge.

Malima  aliwataka  watanzania  kuendelea  kutafakari na kuendelea  moyo  wa  kulipenda Taifa  na  kuepuka kauli  za  kichochezi ambazo  hazina maana  katika Taifa letu .
 

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema  kuwa miongoni mwa  mawaziri  wachakapa kazi ambao Taifa  limewapoteza ni  pamoja na Dr Mgimwa .

Msigwa alisema  kwa  kipindi  chote cha uongozi  wake Dr Mgimwa hakuwa ni mwenye  kujisikia na alikuwa akisikiliza kwa makini na  kukubali kushauriwa na kamwe hakumpuuza  mbunge yeyote  wakati  wa uchangiaji  bungeni juu ya wizara  yake.

Hata  hivyo  mbunge Msigwa alisema  kuwa itikadi za vyama vinapaswa  kuwekwa kando katika kipindi  hiki  cha maombolezo kwa  wana Kalenga na  watanzania  na kuwa  ni vema kwa  kila mmoja kujitafakari  yupo upande gani katika  kulitumikia Taifa  na kuwa wapo baadhi ya  watu  wamekaa sana  duniani na badala ya  kulipa Taifa msaada kwa  uwepo  wao  ila  wamekuwa ni hasara katika Taifa na  wapo waliishi kwa muda mfupi na  wameonyesha mchango  wao mkubwa katika Taifa.

Hivyo  alisema ni vema  kila mmoja  kujiuliza yupo upande upi katika kulitumikia Taifa  yupo tayari kuishi kwa muda  mwingi  bila msaada wowote ama  yupo tayari  kuishi muda  mfupi na mchango  wake  kukumbukwa  daima.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akielezea  jinsi alivyopata  kufanya kazi na Dr Mgimwa alisema  kuwa ni kiongozi aliyekuwa na uwezo mkubwa wa  kiutendaji na alikuwa tayari  kuwashauri waliopo chini  yake kwa lengo la  kuifanya  wizara  yake  kuendelea  kuwa  bora  zaidi.
  Nyumbani kwa  Dr Mgimwa  kijiji  cha Magunga
 
Mbene alisema  kuwa mbali ya  Dr Mgimwa kuwa waziri ila alikuwa akijichanganya na wafanyakazi wa chini na  kuwaelekeza kwa  upendo  pale ambao walikuwa  wanahitaji msaada  wake na  kuwa  siku zote  alikuwa ni mwenye furaha na mwenye  kujishusha  zaidi asiyependa makuu katika wizara  yake.

MATOKEO YA SENSA YA TEMBO NCHINI KUTANGAZWA JANUARY 10 JIJINI DAR ES SALAAM

 

ASAS DAIRY FARM NI DARASA KWA WAFUGAJI TANZANIA

 Ndama  waliozaliwa  siku  za  hivi karibuni


 


 

MAAZIMIO YA KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU HATUA ZA KINIDHAMU DHIDI YA WANACHAMA ZITTO ZUBERI KABWE, DR. KITILA MKUMBO NA SAMSON MWIGAMBA


 

 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed wakati wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam
................................................................................
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilikaa kikao cha dharura ili kupokea, kujadili na kuamua juu ya utetezi wa mashtaka ya ukiukaji wa Katiba, Kanuni na Mwongozo wa Chama yaliyokuwa yanawakabili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Zuberi Kabwe, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu Dr. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba. Kikao hicho cha dharura kilifanyika Dar es Salaam kati ya tarehe 3-4 Januari, 2014. 
 
Kabla ya kuanza kwa kikao, Kamati Kuu ilipokea taarifa kwamba Zitto Zuberi Kabwe amefungua mashtaka dhidi ya CHADEMA katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam. 
 
Aidha, Kamati Kuu ilijulishwa kwamba Mahakama Kuu imetoa amri ya zuio la muda ya kuizuia Kamati Kuu au chombo kingine cha Chama kutokukaa, kujadili na kuamua suala la uanachama wa Zitto Zuberi Kabwe.
 
 Kutokana na amri hiyo ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu haikujadili na kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.
MASHTAKA
Watuhumiwa wote watatu walishtakiwa jumla ya mashtaka 11 yanayohusu ukiukaji wa vifungu mbali mbali vya Katiba ya Chama, Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Kanuni za Kusimamia Shughuli, Mwenendo na Maadili ya Wabunge wa Chama na Mwongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi za Uongozi Kwenye Chama, Mabaraza na Serikali. Mashtaka yote yalitokana na watuhumiwa kuandaa kile kinachoitwa Mkakati wa Mabadiliko, 2013 kama ifuatavyo:

Endelea.......


1.   Kukashifu Viongozi Wakuu wa Chama, yaani Mwenyekiti wa Chama Taifa Mh. Freeman A. Mbowe, na Katibu Mkuu Dr. Wilbrod P. Slaa;
2.   Kutokuwa wakweli na wawazi kwa kushirikiana na vikundi vya majungu kwa kuanzisha na kuratibu mtandao wa siri ulioitwa ‘Mtandao wa Ushindi’ nje ya utaratibu wa Chama ili kumwezesha Zitto Zuberi Kabwe kutwaa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa;
3.   Kutoa tuhuma za uongo dhidi ya viongozi wa Chama na bila kupitia vikao halali vya Chama;
4.   Kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini na ukanda vyenye makusudi ya kubaguana ndani ya Chama na miongoni mwa jamii;
5.   Kujihusisha na vikundi na vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa Chama na wanachama wake;
6.   Kuandaa na kutekeleza mpango wa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa bila kutangaza kusudio la kufanya hivyo kwa mujibu wa Mwongozo wa Chama;
7.   Kutengeneza makundi na mitandao haramu ya kuwania uongozi ndani ya Chama kinyume cha Mwongozo wa Chama;
8.   Kuwachafua viongozi na wanachama wenye nia au kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama kinyume cha Mwongozo wa Chama;
9.   Kujihusisha na upinzani dhidi ya Chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa Chama;
10.                Kukashifu Chama na viongozi wa Chama nje ya Bunge kinyume cha Kanuni za Maadili ya Wabunge; na
11.                Kuchochea mgawanyiko ndani ya Chama kinyume cha Kanuni za Maadili ya Wabunge.
UTETEZI WA WATUHUMIWA
Watuhumiwa wote walijitetea kwa maandishi. Zaidi ya utetezi huo wa maandishi, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu wa kujitetea kwa mdomo mbele yake.
 
 Hata hivyo, siku ya utetezi wao, ni Dr. Kitila Mkumbo peke yake aliyejitokeza kwenye Kamati Kuu na kujitetea kwa mdomo. Katika utetezi wake wa maandishi, licha ya kukiri kushiriki katika maandalizi ya kile kinachoitwa Mkakati wa Mabadiliko 2013, Dr. Kitila Mkumbo – kama ilivyokuwa kwa Samson Mwigamba – alikanusha na kukataa tuhuma zote za kukiuka Katiba ya Chama, Kanuni zake na Mwongozo wa Chama. 
 
Kwa maneno yake mwenyewe, Dr. Mkumbo alikanusha “kila tuhuma mojamoja na kwa ujumla wake dhidi ya[ke]”, na kwamba mashtaka hayo sio ya kweli na hakuvunja Katiba, Kanuni wala Mwongozo wa Chama. 
 
Aidha, licha ya kukiri kwake katika kikao cha Kamati Kuu ya Novemba mwaka jana kwamba walioshiriki kuandaa Mkakati huo ni pamoja na mtu anayejulikana kama M2, mara hii Dr. Kitila Mkumbo aliiambia Kamati Kuu kwamba “waraka husika ulikuwa ni wa siri na haukuwahi kusambazwa wala kushirikisha … wanachama au viongozi wa CHADEMA isipokuwa mimi binafsi na Samson Mwigamba….” Vile vile, ijapokuwa katika Kamati Kuu ya Novemba mwaka jana Dr. Mkumbo alidai kutokumfahamu kabisa M2, mara hii aliiambia Kamati Kuu kwamba anamfahamu fika M2 lakini hayuko tayari kumtaja mbele ya Kamati Kuu hadi atakapowasiliana naye!
 
USHIRIKI WA ZITTO ZUBERI KABWE KATIKA MKAKATI WA MABADILIKO
Itakumbukwa kwamba katika kikao cha Novemba 2013, Dr. Kitila Mkumbo na Zitto Zuberi Kabwe walikataa kata kata kuhusika kwa Zitto Zuberi Kabwe katika maandalizi ya Mkakati wa Mabadiliko. 
 
Aidha, Zitto Zuberi Kabwe alidai mbele ya Kamati Kuu kwamba alikuwa ameusikia Mkakati huo kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu, na amerudia kauli hiyo mara nyingi na hadharani tangu avuliwe nafasi zake za uongozi.
 
 Hata hivyo, wakati wa mahojiano na wajumbe wa Kamati Kuu, Dr. Kitila Mkumbo alikiri kwamba yeye na waandishi wenzake wa Mkakati walimpa Zitto Zuberi Kabwe briefing juu ya Mkakati na kwamba alikuwa anaufahamu. Ukweli huu pia umethibitishwa na mawasiliano ya baruapepe iliyotumwa na Zitto Zuberi Kabwe mwenyewe kwa mtu anayeitwa ‘CHADEMA Mpya 2014’ tarehe 27 Oktoba, 2013, karibu mwezi mmoja kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya Novemba iliyowavua madaraka. 
 
Zaidi ya hayo, baada ya kuonyeshwa waraka wa Chama juu ya mabadiliko ya Katiba ya Chama uliotumwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama wakati huo Shaibu Akwilombe Julai 2006 unaothibitisha kwamba mabadiliko ya Katiba yaliyoondoa ukomo wa uongozi yalifanywa kwa uwazi na kwa kushirikisha ngazi zote za Chama, Dr. Kitila Mkumbo alikataa kata kata kujadili suala hilo kwa madai kwamba tayari walishapeleka malalamiko yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa. 
 
Kuhusu tuhuma zao kwamba kuna ufisadi na ubadhirifu wa fedha za Chama unaofanywa na Mwenyekiti wa Chama, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Anthony Komu na kwamba taarifa za matumizi ya fedha ni siri ya viongozi hao watatu, Dr. Mkumbo alionyeshwa taarifa mbali mbali za fedha zilizowasilishwa mbele ya vikao vya Kamati Kuu a Chama ambavyo yeye mwenyewe na Zitto Zuberi Kabwe walishiriki kama wajumbe wa Kamati Kuu. 
 
Aidha, Dr. Mkumbo alionyeshwa taarifa za kibenki zinazoonyesha jinsi michango ya Mzee Jaffer Sabodo na michango mingine ya watu binafsi zilivyopokelewa na kutumiwa na taarifa zake kuwasilishwa kwenye vikao vya Kamati Kuu walivyohudhuria yeye na Zitto Zuberi Kabwe. 
 
Zaidi ya hayo, Dr. Mkumbo alionyeshwa nyaraka za manunuzi ya vifaa vya Chama kama vile vile pikipiki, kadi, bendera, n.k, na jinsi ambavyo uamuzi wa manunuzi hayo yalifanywa na Kamati Kuu ambayo wao wenyewe ni wajumbe na walihudhuria vikao husika.
 
 Vile vile, Dr. Mkumbo alionyeshwa ushahidi wa maandishi kwamba Mwenyekiti wa Chama hakuhusika kwa namna yoyote ile katika manunuzi hayo na hakuna karatasi yoyote inayoonyesha saini ya Mwenyekiti katika manunuzi ya vifaa hivyo. 
 
Aidha, Dr. Mkumbo hakuweza kuthibitisha kwa namna yoyote kwamba CHADEMA ina mkataba wowote na watu binafsi wanaouza vifaa vya uenezi vya Chama kwa vile Kamati Kuu ya Chama katika vikao ambavyo vilihudhuriwa na Dr. Mkumbo na Zitto Zuberi Kabwe ilikwisharuhusu wafanya biashara binafsi kuagiza vifaa hivyo na kuviuza kwa wanachama wanaotaka kuvinunua. Kwenye yote haya, Dr. Kitila Mkumbo hakuwa na lolote la maana la kuiambia Kamati Kuu. 
 
MAAMUZI YA KAMATI KUU
Baada ya kusikiliza utetezi wa Dr. Kitila Mkumbo na baada ya kumhoji kwa kirefu, Kamati Kuu imeridhika bila mashaka yoyote kwamba Mkakati wa Mabadiliko 2013 haukuwa na lengo la kumwezesha Zitto Zuberi Kabwe kutwaa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama peke yake. 
 
Mkakati huo ulikuwa na malengo makubwa zaidi ya kukibomoa Chama kwa kukichafua kwa wananchi na kuwachafua viongozi wake wa juu kwa kutumia tuhuma za uongo za ufisadi. 
 
Hii ni kwa sababu, kwa maoni ya Kamati Kuu, Chama cha siasa ambacho viongozi wake wa juu wanatuhumiwa kwa ufisadi hakiwezi kuaminiwa na wananchi kama tumaini lao la ukombozi. 
 
Kamati Kuu imeridhika kwa ushahidi wa nyaraka mbali mbali zilizoandaliwa na Zitto Zuberi Kabwe mwenyewe ama na mawakala wake wakitumia vitambulisho bandia katika mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwamba mkakati wa kukibomoa Chama umeandaliwa na kutekelezwa kwa muda mrefu.
 
 Mkakati huo ulihusisha pia hujuma dhidi ya Chama kwa kuwaengua wagombea wake katika chaguzi mbali mbali kama ilivyotokea katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini na Singida Mjini ambapo Zitto Zuberi Kabwe alishiriki moja kwa moja.
 
Kwa sababu zote hizo, Kamati Kuu imeazimia ifuatavyo:
1.    Kwamba kuanzia tarehe ya uamuzi wake, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wafukuzwe uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); na
2.    Kwamba, kwa vile Zitto Zuberi Kabwe amekishtaki Chama kinyume na matakwa ya Katiba ya Chama na Kanuni zake, na kwa vile Mahakama Kuu imeamuru vikao vyote vya Chama visijadili wala kuamua suala lolote linalohusu uanachama wa Zitto Zuberi Kabwe, viongozi wa ngazi zote za Chama, wanachama, washabiki na wapenzi wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya Tanzania wasishiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yoyote ya nje au ya ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto Zuberi Kabwe na mawakala wake kwa jina la CHADEMA.
--------------------------------
Dr. Wilbrod P. Slaa

KATIBU MKUU