Wednesday, October 1, 2014


RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE KWENDA TEGETA LEO
B


BARABARA YA MWENGE KWENDA TEGETA INAYOFUNGULIWA LEO

Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta itakayokazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Sehemu ya barabara ya Mwenge-Tegeta itakayofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta utakaofanyika Oktoba 1, 2014.
Ufunguzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.
Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (CGU), Wizara ya Ujenzi.

Mheshimiwa Dk. Magufuli akikagua ujenzi wa Barabara wkati huo.Hatimaye sasa imekamilika



MZEE KARIBU SANA NYUMBANI,



RAIS KIKWETE AKIWA NA WAKUU WA VYOMBOVYA ULINZI NA USALAMA UWANJA WA MWL. jULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOWASILI KUTOKA MKUTANO WA 69 WA UMOJA WA MATAIFA ULIOFANYIKA NCHINI MAREKANI


Hatimaye Mhe. Kinana aongoza msafara wa baiskeli kwenda Milima ya Usambara, Tanga


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg'aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga,  mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg’aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
Ni safari ndefu lakini yenye faraja na matumaini
Ni safari ndefu lakini yenye faraja na matumaini.
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama baada ya kutumia usafiri wa baiskeli.
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama baada ya kutumia usafiri wa baiskeli.
Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg'aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga.
Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg’aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga.
Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mg'aro ambapo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mkinga itaboreshwa, halafu na umeme utawekwa katika Kata hiyo.
Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mg’aro ambapo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mkinga itaboreshwa, halafu na umeme utawekwa katika Kata hiyo.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya msafara wake kukabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mkinga katika Kata ya Daluni.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya msafara wake kukabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mkinga katika Kata ya Daluni.
Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Maramba.
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Maramba.
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji.
Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga.
Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga. 




































Monday, May 26, 2014

Mambo yaiva Brazil Viwanja 12 kutumika kufanikisha

 
uwanja wa Amazonia_Arena 
Mji wa Recife unafananishwa na mji wa Venice, Italia kwa sababu ya mito na mifereji ya maji. Recife pia inajulikana kwa kuwa na fukwe nzuri. Shujaa wa mji huu ni nyota wa zamani wa Brazil, Rivaldo.


Rio de Janeiro, Brazil
Zimebaki siku 16 kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Mwaka huu, fainali hizo zimepangwa kufanyika Juni 12 mpaka Julai 13 na zitachezwa kwenye viwanja 12.
Vifuatavyo ni viwanja hivyo 12:
Uwanja wa Itaipava Pernambuco (Recife)
Una uwezo wa kuchukua mashabiki 46,000. Inatarajiwa hali ya hewa katika mji wa Recife wakati wa mwezi Juni itakuwa joto la 25°C.
Mji wa Recife unafananishwa na mji wa Venice, Italia kwa sababu ya mito na mifereji ya maji. Recife pia inajulikana kwa kuwa na fukwe nzuri. Shujaa wa mji huu ni nyota wa zamani wa Brazil, Rivaldo.
Uwanja wa Amazonia-Manaus
Una uwezo wa kuchukua mashabiki 44,000. Hali ya hewa mwezi Juni inatarajiwa nyuzijoto 27.5°C.
Uwanja wa Amazonia upo katika mji wa Manaus ambao una msitu wa Amazonia wenye mvua nyingi na unaotembelewa na watalii wengi. Nyota kutoka mji huu ni Francisco Lima Govinho aliyekuwa kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Brazil.
Uwanja wa Pantanal (Cuiaba)
Una uwezo wa kuchukua mashabiki 43,000. Hali ya hewa mjini Cuiaba mwezi Juni inatarajiwa kuwa 24.1°C. Cuiaba ni mji wa tatu kwa kuwa na ng’ombe wengi Brazil. Mchezaji maarufu kutoka mji huu ni kiungo mkabaji Lucas Leiva anayeichezea klabu ya Liverpool ya England.

Mageuzi makubwa usafiri wa Reli yaja

 

Serikali yatangaza mageuzi usafiri wa reli

Treni ikishusha abiria kwenye kituo, Serikali inashirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi katika uendelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Dar es Salaam-Isaka-Musongati kwa kiwango cha kimataifa.

Dodoma. Serikali imekamilisha taratibu za ununuzi wa vichwa vipya 13 vya treni na mabehewa 355 ambayo yataanza kuwasili nchini kati ya Julai na Desemba mwaka huu.
Serikali inashirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi katika uendelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Dar es Salaam-Isaka-Musongati kwa kiwango cha kimataifa.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma juzi usiku wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 inayofikia Sh527 bilioni.
Alisema kazi inayoendelea sasa ni kumtafuta mshauri (Transact Advisor) atakayekuwa na jukumu la kuandaa, kusimamia na kuongoza mpango wa kuwapata wawekezaji watakaojenga reli hiyo.
“Kazi ya usanifu wa kina wa kuinua kiwango cha Reli ya Isaka-Mwanza ilianza Septemba 2013 na inatarajiwa kukamilika Julai 2014 kwa gharama ya Sh4.53 bilioni...Hatua hizi ni muhimu katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuboresha Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge)” alisema Dk Mwakyembe katika hotuba yake hiyo.”
Pia Dk Mwakyembe alisema kuwa tayari mtaalamu mwelekezi amepatikana kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa Reli ya Mtwara-Songea-Mbambay.
Mkataba wa kutekeleza kazi hiyo itakayohusisha pia ujenzi wa reli ya mchepuko kwenda Mchuchuma na Liganga utasainiwa wakati wowote kabla ya mwisho wa Juni mwaka huu.
Pia mshauri mwelekezi, Kampuni ya Cowi kutoka Denmark ameanza kazi ya usanifu wa uboreshaji wa njia ya Reli ya Tanga-Arusha na usanifu huo utagharimu Sh5 bilioni.
Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe alisema Kampuni ya H.P Gauf ya Ujerumani inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli mpya ya Arusha-Musoma.
Ununuzi wa mabehewa
Dk Mwakyembe alisema katika mwaka ujao wa fedha wa 2014/2015, Serikali imetenga Sh126.9 bilioni kununua vichwa vipya 11 vya treni na mabehewa 204.
Alisema fedha hizo zitatumika pia kufanya matengenezo ya njia ya reli ya kati yenye mtandao wa urefu wa kilometa 2,707.

Tuesday, April 1, 2014

Ridhiwani kikwete aendelea na kampeni za lala salama chalinze

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Dini kwenye Kijiji cha Mkange,Kata ya Mkange wakati alipopita kuwasalimia na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Jana Machi 30,2014.Picha zote na Othman Michuzi. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa Makini Mzee Hussein Mwindadi ambaye ni Baba wa Diwani wa Kata ya Mkange. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Manda Mazingara wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika jana Machi 30,2014. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akionyeshwa maendeleo ua ujenzi wa Msikiti (haupo pichani) na Sheikh Yahya Abdullah Imam wa Msikiti huo. Wananchi wa Kijiji cha Manda Mazinga wakifatilia kwa makini Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika jana Machi 30,2014.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

(Yesterday)

Daily News

Chalinze warned against voter card buyers


Chalinze warned against voter card buyers
Daily News
CHALINZE residents in Bagamoyo District, Coast Region, have been cautioned against being tricked into selling or giving up their voter cards to anyone as it is against the law. The warning was sounded by the campaigns manager of the Chama Cha ...


2 days ago

Fullshangwe

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA KAMPENI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA CHALINZE

1 Sisty Nyahoza Msajili masidizi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa akizungumza na waandhishi wa habari katika ukumbi wa Masai Chalinze kuhusu mwenendo wa kampeni za vyama na wagombea wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu, kutoka kushoto ni Muhidini Mapayo Mwanasheria na kiongozi wa timu ya Ofisi ya Msajili Chalinze na Erald Martin Ofisa Sheria. 2

2 days ago

Tanzania Daima

Mvua zaathiri kampeni Chalinze

MVUA zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini zimesababisha baadhi ya mikutano ya kampeni katika Jimbo la Chalinze kutofanyika. Kampeni hizo zinazoendelea katika maeneo ya Jimbo la Chalinze zinatarajiwa kuhitimshwa...

3 days ago

Michuzi

CCM YAENDELEA NA MBIO ZAKE KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA CHALINZE


Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Hondogo,Kata ya Mandera wakati wa muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,leo Machi 29,2014.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,Suleiman Jaffo akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mandera Kibaoni wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo  Machi 29,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kuruka sambamba na wakina Mama wa Kabila la Wamasai,wakati alipowasili kwenye Kitongoji cha Nameloki Chatanga,Kijiji cha Umasaini,Kata ya Mandera.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Magole,Kata ya Mandera wakati akimuombea Kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo Machi 29,2014.
Wananchi wa Kijiji cha Hondogo katika Kata ya Mandera ndani ya Jimbo la Chalinze,wakinyoosha mikono juu kuashiria kumpigia kura Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati Mkutano wa Kampeni zake zilizofanyika Machi 29,2014.Picha na Othman Michuzi.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

3 days ago

Michuzi

MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA CHALINZE ULIVYOKABILIWA CHANGAMOTO YA BARABARA

Mwenyekiti wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze,Saleh Mpwimbwi akiangalia gari linaloongoza Msafara wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze wa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete likipita kwa shinda kwenye barabara yenye tope kutoka Kijiji cha Hondogo kwenda Kilemela,wakati wa safari ya kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo,Machi 29,2014.hali hiyo imekuja kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo katika Maeneo mbali mbali hapa nchini.Ridhiwani Kikwete amewaahidi wakazi wa Kijiji cha Kilemela kuwa,moja ya kazi zake za awali atakazoanza nazo pindi atakapopata Ubunge ni kuhakikisha barabara hii inapitika vizuri kwa kipindi chote. Gari hilo likiendelea kwenda kwa shida shida huku likiteleza na kupelekwa pembeni ya barabara kama inavyoonekana pichani. Likafika mahala likanasa. Wadau wakijaribu kulinasua gari hilo. Mbinu mbadala za kulitoa gari hilo zikiendelea. Mambo yakiendelea na baadae walifanikiwa kulinasua gari hilo na kulirudisha barabarani ili liendelee na safari yake.

3 days ago

Fullshangwe

MWENYEKITI WA CCM PWANI:RIDHIWANI KIKWETE NI (TANGANYIKA JEKI) ITAWAKWAMUA WANACHALINZE KATIKA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO

1Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mhalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Kibindu na kuhudhuriwa na wakazi wa kijiji hicho, akimuombea kura Ridhiwani Kikwete mgombea wa kupitia Chama cha Mapinduzi amemfananisha mgombea huyo na Jeki aina ya (Tanganyika Jack) na kusema atawakwamua wana Chalinze katika changamoto zinazowakabili katika maendeleo jimboni humo,Uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu.(PICHA NA KUKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE) 2

3 days ago

Tanzania Daima

Wawekezaji Chalinze feki wamkera diwani

DIWANI wa Lugoba, Rehema Mwene, amelalamikia kitendo cha baadhi ya wawekezaji kuomba kuwekeza na kushindwa kutekeleza makubaliano ya maombi yao. Mwene alitoa kauli hiyo juzi kwenye mikutano ya kampeni ya...

4 days ago

Fullshangwe

RIDHIWANI KIKWETE AFUNIKA KATA YA PERA CHALINZE

1 
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwahutubia  wananchi  katika viwanja vya kwa Mwarabu  kata ya Pera Chalinze  leo wakati wa  mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE) 2

WENGI WAMPA UBUNGE RIDHIWANI CHALINZE

Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwan Kikwete. WANANCHI wa vijiji kadhaa vilivyomo katika Jimbo la Chalinze, ambalo Aprili 6, mwaka huu litafanya uchaguzi mdogo wa Ubunge, wamempa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Ijumaa katika vijiji saba vya jimbo hilo, wengi wa waliohojiwa kuhusu mshindi wa nafasi hiyo, walisema…

5 days ago

Habarileo

CCM: Ridhiwani suluhisho Chalinze


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Mwishee Mlau amesema mwenye uwezo wa kutatua changamoto zilizopo katika Jimbo la Chalinze ni mgombea wa chama hicho, Ridhiwani Kikwete na sio mgombe



RIDHIWANI KIKWETE APIGA KAMPENI VIJIJI VYA CHAHUA NA MATULI CHALINZE

1Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Matuli kata ya Chalinze kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)

KAMPENI ZAKE JIMBO LA CHALINZE ZASHIKA KASI ZAIDI
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Saleni,Kata ya Lugoba ndani ya Jimbo hilo wakati akiendelea na Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze leo Machi 26,2014. Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa muendelezo wa Mikutano ya Kampeni za CCM kwenye Kata ya Msata.
Diwani wa Kata ya Msoga,Mohamed Mzimba akitoa taarifa ya Kata yake mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM katika Kata hiyo ya Msoga.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye (kulia) akishiriki kucheza Ngoma na wazee wa Kabila la Wakwere wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI