Friday, March 21, 2014

Pwani yaelemewa na uuzaji ardhi

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha KaziZumbwi, wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Shughuli kuu ya kiuchumi ya wakazi hao ni kuchoma mkaa na kilimo cha mihogo.
Kasi ya uuzaji wa ardhi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, inatishia uhai wa misitu michache iliyobakia.

Unapotembelea wilaya hiyo unaona maeneo ya vichaka, misitu na mashamba yamesafishwa kwa ajili ya kilimo. Umaskini unajidhihirisha kwa wakazi wa eneo hilo.

Wanunuzi  wa ardhi hiyo wengi wanadaiwa kutoka jijini Dar es Salaam. Husafisha mashamba yao kwa ajili ya  maandalizi ya  kilimo kwa kukata miti na kuchoma moto.

Baadhi  hujipenyeza kwa mgongo wa uwekezaji na kutwaa  mapande makubwa ya ardhi na kuyaacha muda mrefu bila kuyaendeleza  huku wananchi hawaruhusiwi kuingia ndani ya eneo husika.

Kutokana na ukuaji wa miji, misitu ya mkoa wa Pwani inachukuliwa kuwa ni mapafu ya mkoa wa Dar es Salaam , kwa ajili ya kunyoya hewa chafu inayotokana na moshi wa magari, viwandani na shughuli za kibinadamu.

Kisayansi misitu pekee ndiyo uwezo wa kunyonya hewa chafu na kutoa hewa safi ambayo inahitajika kwa maisha ya binadamu.

Hata hivyo, wakazi wengi wa mkoa huo, shughuli kubwa za kuwaingizia kipato vijijini ni kilimo na uchomaji mkaa, unauzwa maeneo ya miji. Jiji la Dar es salaam linatumia
zaidi ya asilimia 90 ya mkaa unaozalishwa kwenye mistu inayokana na jiji hilo.

Hivi karibuni Waandishi wa Habari saba wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (Jet), walitembelea wilaya ya Kibaha na kujionea hali halisi ya usimamizi, utunzaji wa misitu na jinsi inavyowanufasha wanajamii.

Ziara hiyo ni sehemu ya  kampeni ya Mama Misitu ambayo Jet ni mtekelezaji ngazi ya Taifa na kubaini  kasi ya uuzwaji wa ardhi inayofanywa na wananchi kwa lengo la kujipatia kipato kwa ajili ya maisha yao.

Uchumi wa wananchi hao ni kilimo ambacho kimeyumba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababishwa na uharibifu wa mazingira, na kuwalazimisha wategemee uzalishaji wa mkaa na mbao na uuzaji wa ardhi kwa wageni.

Karibu kila kijiji wilayani humo kimeuza sehemu kubwa ya ardhi, ambayo wamiliki wapya wamesafisha kwa ajili ya kilimo  kukata miti na ardhi kubaki tupu.

Vijiji vilivyotembelewa ni Mpiji Station ambako wananchi hawana msitu wa asili na kuibuka mgogoro baina ya mwekezaji Mohamed Enteepresies anayemiliki  eneo kubwa la ardhi, huku wananchi wakidai msitu huo ni mali yao.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Said Mwenyedua, anasema wamesimamishwa kufanya jambo lolote kwenye eneo hilo ambalo tangu mwaka 1974 vilivyoanzishwa vijiji walikuwa wakiulinda na kuutunza.

“Wakati tukiendelea kutunza na tukiamini ni msitu wetu, alijitokeza mwekezaji huyo na kudai ni eneo lake, Halmashauri ilitusimamisha na wataalamu wanafuatilia ili kujua mmiliki halisi ni nani,” alisema

Nassoro Magombe, anasema tangu alipozaliwa  ameukuta msitu huo, ameshangazwa na kauli za siku za karibuni kuwa si mali yao na kusimamishwa wasifanye shughuli yoyote ndani yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha, Tatu Selemani, anasema vijiji vya Kipangege, Mpiji Station na Soga, vyote vipo kwenye eneo linalodaiwa kuwa la mwekezaji huyo.

“Tulichokifanya ni kufanya tathimini ya eneo na kumtaka Mohamed Entepreses kuleta vithibitisho kuwa eneo ni mali yake, inaonyesha aliuziwa chini ya sheria ya ardhi namba 5 na sasa kuna mvutano,“anasema

Anasema suala hilo limefikishwa  kwa Waziri Mkuu na vijiji
hivyo vimesajiliwa vinatambulika kisheria na mvutano kuwa mkubwa kwa wananchi kuona wana haki kisheria na mwekezaji vile vile.

Anasema mwekezaji huyo kaendeleza shamba hilo kwa asilimia 15. Kati ya ekari 20,000 ni  3,000 tu zilizopo katika  kijiji cha Soga ndio zimeendelezwa  na kusababisha wananchi waamini kuwa maeneo hayo ni mali yao.

Selemani anasema, idadi kubwa ya wanunuzi wa ardhi ni kutoka Dar es Salaam, ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kumaliza misitu muhi mu ya mkoa huo.

“Tunawaelimisha wananchi wasiuze ardhi ovyo, watendaji wa vijiji na kata wamepewa barua kama kuna mtu anataka kununua ardhi watoe taarifa wilayani, tunataka ununuzi uanzie Halmashauri ambayo ndiyo inajua kitaalamu panapofaa kuuza kwa shughuli fulani,” anasema

Uuzaji wa ardhi kiholela  anasema kuwa ni tishio kwa misitu wilayani humo na kwa sasa utapeli wa kuuza ardhi umeingia hadi kwenye msitu wa Serikali Kuu wa Ruvu Kusini katika eneo la Zumbamlonga ambako watu wameuziwa ardhi.

Wauzaji hao huuza kwa bei ya kutupwa ya Sh 30,000 kwa ekari hali  inayovuta wengi na wanapouziwa hawakumbuki kwenda Halmashauri kujua mpango wa matumizi bora ya ardhi umelelekeza nini kwenye eneo analouziwa.

Baraza la Madiwani wameliona tatizo la uuzaji ardhi holela na kupeleka ngazi za juu kwa ajili ya  nguvu kisheria ya kuuza ardhi na si vijiji au kata.

Wanunuzi wengi wanatoka Dar es Salaam ambako ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali hakuna. Wengine huanza kilimo na wanaokubali ushauri wa kupanda miti hufanya
hivyo ili kulinda mazingira. Baadhi huona miti haina faida ya haraka kama mazao ya muda mfupi.

Anasema kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu kanda ya Mashariki na mashirika yasiyo ya kiserikali mojawapo likiwa mradi wa Mama Misitu, wanaelimisha jamii kutunza mazingira kwa manufaa endelevu
na kuepukana na uuzaji ardhi kiholela ili kulinda misitu michache iliyobakia.

Kaimu Afisa Misitu wa Halmashauri ya Kibaha, Dustun Mnyenye, anasema wanahamasisha wenye mashamba kupanda miti, lakini  mwitikio ni mdogo sana kwa
wenyeji kwa sababu wanataka faida ya haraka na baadhi ya wageni hawakubali.

Kampeni ya upandaji miti hufanyika kila mwaka kwa miti milion 1.5 hupandwa na  watu binafsi ambao hupewa miti baada ya kuandaa maeneo ya kupanda, shule za msingi na sekondari kuwa na mashamba ya miti ili kuanzisha misitu mipya.

Kaimu Meneja Wakala wa Huduma za Misitu kanda ya Mashariki, Bakari Mohamed, anasema kasi ya uuzaji wa maeneo holela imewasukuma kuomba kibali cha serikali kuu kuunda timu maalumu ya kufuatilia ngazi ya vijiji na kata ili isiuzwe.

Uuzaji wa ardhi umesababisha ardhi kubaki wazi, kwani wengi husafishisha mashamba kwa madai ya kuanzisha kilimo.

Changamoto zilizopo ni mahitaji ya nishati ya mkaa kwa maeneo ya mjini yamechangia kumaliza misitu. Kipaumbele kwenye dhana ya Kilimo Kwanza nayo imechangia kumaliza
misitu, kwani wastaafu wengi hutumia fedha zao kununua mapande makubwa ya ardhi na kufyeka miti na kuanzisha mashamba ya mahindi au maharagwe.

Wananchi wa maeneo hayo kwa kutojua wamejikuta wakisafisha ardhi yenye misitu kwa ajili ya kilimo na dhana iliyojengeka miongoni mwao kuwa ardhi hiyo  inafaa kwa kilimo.

Nyingine ni baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwa sehemu ya uharibifu wa mazingira kwa kuingilia kati  wanapokamatwa wahalifu wa uharibifu wa misitu.

Anasema hivi karibuni walikamata kundi la ng’ombe zaidi ya 3,000 baada ya  kupigiwa simu na viongozi wa ngazi za juu serikalini na kuwataka waachie wafugaji hiyo bila kuwatoza faini yoyote.

Nyingine ni baadhi ya  wananchi  kwa tama ya kipato cha haraka huingia msituni  kukata miti ,kuchoma mkaa na kupasua mbao.

Anasema  baadhi ya watendaji katika ngazi ya mahakama wanatumika kuharibu mazingira kwa kuwaachia wahalifu,

kutoa adhabu ndogo au kuvuruga kesi katika mazingira ya kutatanishwa na hivyo wanaofanya vitendo hivyo kuendelea kwa kuamini wanalindwa.

Uuzwaji wa maeneo ya kando mwa bahari ya Hindi ni tatizo kubwa na hufanywa na  baadhi ya viongozi wakubwa hali inayotishia uhai wa miti aina ya mikoko.

Anasema miti hiyo kwenye baadhi ya maeneo ya kisiwa, wananchi wanaruhusiwa kuvuna kila baada ya muda fulani, ili kupata kipato kutokana na hali ya maeneo yao hawana shughuli nyingine za kuingiza kipato.

Shughuli za wakala ni ulinzi wa misitu, iliyohifadhiwa iendelee kuhifadhiwa na kuwa na matumizi endelevu kwa ulinzi shirikishi na jamii za maeneo husika.

Uanzishwaji wa misitu mipya kwenye maeneo mapya kama ya Rufiji, Morogoro na Pwani, kupanda miti na kuzungusha mipaka kwenye misitu ya serikali na kutunza miti ya mikoko.

Anasema wananchi wanashirikishwa kulinda misitu kwa kila kijiji kuwa na kamati ya maliasili, na kuna makubalinao kwa kinachopatikana kugawanywa kwa usawa.

Ili kuwa na uvunaji endelevu kwa kushirikiana na Mama Misitu
wameviwezesha vikundi mbalimbali vilivyopo kwenye vijiji kuwa na mizinga ya ufugaji nyuki ili kupata kipato na kuachana na ukataji miti.

Anasema jamii inapaswa kuelewa bila misitu hakuna maisha na kutokana na jiji la Dar es Salaam, kumaliza misitu kwa ajili ya uanzishwaji wa makazi, tegemeo kubwa ni mkoa wa Pwani ambako misitu inakwisha.

Bila Serikali na Mamlaka zake kuingilia kati kikamilifu hali ni mbaya kwenye misitu ya jamii na  ya Serikali nafanyika.

Subira Juma ni Katibu wa Kikundi cha nguvukazi Soga, ambacho hujishughulisha na uzalishaji wa mkaa kwa kutumia nyasi, maranda na pumba za mpunga, ambao ni mbadala wa mkaa wa miti.

Iwapo tekinolojia hiyo itawezeshwa kuwafikia wananchi wengi wataachana na ukataji miti kwa kuwa wataweza kupata kipato kwa kuuza mkaa huo.

Wanashirikiana na jamii kulinda msitu wa Ruvu Kusini,
unaokabiliwa na wavamizi kutoka nje ya mkoa huo kwa kuvuna mbao na mkaa.

Rais Jakaya Kikwete alihutubia Bunge Maalumu la Katiba.

Awaonya wabunge wa bunge Maalumu la katiba kuhusu mgawanyiko,awataka wawe wamoja na wazingatie maslahi ya Taifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JakayaMrisho Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelihutubia bunge maalumu la Katiba na kutaka wajumbe wa bunge hilo kuhakikisha kuwa katiba inayopatikana itakuwa ni katiba yenye kuheshimu haki za binadamu, kudumisha upendo, katiba inayotekelezeka, na wananchi kunufaika na maendeleo yatakayopatikana kutokana na katiba hiyo.

Aidha amewataka wajumbe hao kusoma na kuelewa kilichoandikwa na kufanya uamuzi mzuri wa mawazo yao binafsi pasipo kushauriwa na wenzao ama makundi .
Rais Kikwete amesema kuwa wajumbe hao wana wanawajibu wa kuchambua kwa kina rasimu hiyo ya pili ya katiba kifungu kwa kifungu, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi, neno kwa neno, na kuboresha pale wanapoona panastahili maboresho na ikiwa kuna jambo ambalo halifai wanao wajibu wa kuliondoa ili kupata katiba itakayo dumu kwa muda mrefu.
Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kufanya mchakato wa kuwa na katiba mpya ambapo mwaka 1965 iliandaliwa katiba ya muda na mwaka 1977 katiba ya kudumu ilitengenezwa ambayo ndiyo inatumika hadi sasa.
Mchakato wa sasa wa katiba mpya ya Tanzania kwa mara ya kwanza umewashirikisha wananchi ambao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho kuhusu katiba hiyo kwa kupiga kura ya maoni.


 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Kikwete, anazindua Bunge Maalum la Katiba hapa Dodoma kuanzia saa 10 kamili jioni. Katika uzinduzi huo, Rais Kikwete ameambatana na ujumbe mzito kama vile Marais Wastaafu wa pande mbili za Muungano, wake wa waasisi wa taifa, na mawaziri wakuu wastaafu.

Kwenye msafara huo ni pia yupo Rais mstaafu Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dr Salmin Amour, Aman Abeid Karume, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. wengine ni Jaji Joseph Sinde Warioba, Cleopa Msuya, John Malecela, Dr Salim Ahmed Salim, Friedereck Sumaye na Edward Lowasa. Mbali na viongozi hao, pia Rais Kikwete ataambatana na Rais wa Zanzibar, Mr Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Seif Sharif Hamad na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa bunge la katiba.

Pia wapo wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii, wawakilishi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa, mabalozi wa nchi mbalimbali na wengineo.

Imeripotiwa kuwa viongozi wakuu wa vyama vya Upinzani, Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamepongeza uamuzi huo wa Rais kuambatana na msafara huo. Pia wamewaomba wabunge wenzao hasa wa upinzani kuonesha hali ya utulivu wakati wote wa tukio hilo muhimu la kihistoria.

--------------------------------------------------------------------------------
Kinachojiri sasa Bungeni; kwa maandalizi ya Hotuba ya Rais Kikwete
--------------------------------------------------------------------------------

- Wabunge wanaingia kwa wingi ukumbini. Naona leo hali ya mahudhurio imekuwa nzuri

- Kwa mujibu wa Ratiba ni kwambq kikao cha abunge kilipaswa kuanza saa 9.10. Ila ratiba huenda itachelewa kidogo. Wageni waliofika ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Mkuu wa Tanzania na Zanzibar

- Mzee Karume naye yupo nje ya viwanja vya bunge

- Naam namuona Mheshimiwa Freeman Mbowe anawasili na sasa anateta jambo na ajames Mbatia

- Naam, kule nje namuona Makamu wa Rais, Gharib Bilal

- Hakika ukumbi wa bunge umependeza sana leo. Wabunge wengi wamejitokeza na kuna wageni wengi pia

- Naaam sasa Rais JK anaingia Ukumbini kwa kupitia ule mlango wa VIP

- Mheshimiwa Abeid Amani Karume sasa Anaingia

- Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi anaingia sasa

- Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Makungu anaingia Bungeni sasa

- Jaji Mkuu, Mohamed Chande aorhman anaingia sasa

- Makamu wa Kwanza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anaingia ukumbini

- Anayefuata ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Mohamed Shein

- Anayefuata ni Makamu wa Rais, Dr Mohamed Ghalib Bilal

- Wageni wote muhimu wamewasili na sasa anayesubiriwa ni Mheshimiwa Rais kuingia Bungeni

- Naam mzee wa Speed and Standard anamsindikiza Rais JK kuingia ukumbini. Mayowe yanapigwa kuashiria furaha ya wabunge. Namuona mheshimiwa mnyaa anapiga meza muda wote

- Mzee Malecela naye yumo. Pia kuna Pius Msekwa, mama Maria Nyerere na wake za viongozi


--------------------------------------

- Rais JK anaanza kuhutubia kwa kucheka na kusema "haijapata kutokea". Sijui ana maana gani...

- Rais anawaponyeza Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwa kishindo. Anawapongeza pia wabunge kwa fursa hii waliyopata ya kuwa wabunge wa bunge la katiba. Anasema kuwa wabunge watatunga katiba inayokubalika na watanzania, inayotekelezeka, itakayoondoa changamoto za muungano zilizopo, itakayoimarisha muungano, itakayodumisha amani na usalama, itakayostawisha demokrasia, kuimarisha utawala wa kisheria, kupunguza maovu, kukuza uchumi na kuleta maendeleo sawia kwa wananchi

Rais anasema kuwa hii ni mara ya Tatu Tanzania kuandaa katiba. 1965, 1977 na huu wa sasa. Ila anasema huu wa sasa unashirikisha wananchi kwa kutoa maoni yao, mabaraza ya katiba na kwa kura ya maoni. Tofauti na michakato iliyotanguloa ambapo ni wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano tu, mchakato wa sasa una wengi na unashirikisha makundi mengi

Rais anasema kuwa kelele za kutaka kuwa na katiba mpya zimekuwepo sana wakati wa mfumo wa vyama vingi

Anampongeza jaji Warioba na wajumbe wote wa tume.

Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo anataka litafakariwe kwa makini. Anawataka wajumbe watafakari kwa kina kuhusu hilo. Kwamba lina uzuri na ubaya wake

Sasa anajadili kuhusu muundo wa Muungano. Anasema kuwa jambo hili limezua mjadala mzito tangu Rasimu ya mwanzo hadi ya mwisho. Anasema kuwa jambo hilo linasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi. Karika hilo anaroa ushauri ufuatao



  1. Wabunge waepuke jazba wakati wa kujadili suala hilo
  2. wajumbe watafakari madhara yanayoweza kujitokeza iwapo jambo hilo halitapatiwa ufumbuzi kwa njia ya utulivu  
  3. Anasema kuwa mjadala wa muundo wa katiba moya si mheni kama alivyoeleza Warioba. Kwamba mwaka 1984 ulikuwa chanzo cha machafuko Zanzibar. Pia mwaka 1993 jambo hilo lilikuwa ni chanzo na G55

- Rais Kikwete anasema kuwa sababu za kuwa na serikali mbili ni mbili

  1. Kuhakikisha kuwa Zanzibar haimezwi kwenye Muungano
  2. kuepuka gharama kwa Tanzania Bara kugharamia serikali ya bara na ya muungano

- Rais anasema kuwa kwa mujibu wa Jaji Warioba ni Muundo wa serikali Tatu, umependekezwa kutokana na sababu mbili.

  1. Kwamba watanzania wengi wamependekeza muundo huo
  2. unatoa majibu ya matatizo ya serikali mbili


Maalim Seif  alipowasili Mjini Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Ufunguzi wa Bunge Maalum la Katiba ,litakalohutubiwa na Rais Kikwete, 

Thursday, March 20, 2014

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif amewasili Mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Katka uwanja wa ndege wa Dodoma, Maalim Seif amepokelewa na viongozi wa Mkoa huo pamoja na Wabunge, Wawakilishi na viongozi mbali mbali wa CUF.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mbunge wa Mji Mkongwe Mhe. Ibrahim Sanya, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Chadema yaahidi amani, maendeleo Chalinze Ijumaa, Marchi21  2014  saa 11:40 AM
  • Waeleza mikakati yao na kuwaomba wafuasi wao kuepuka vurugu.
Bagamoyo. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana  (Chadema) Mkoa wa Pwani, Elison Kinyaha amesema ili kudumisha maendeleo, upendo na amani ndani ya Jimbo la Chalinze, upo ulazima wa wakazi wa jimbo hilo kumchagua Mathayo Torongey katika uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika mapema Aprili 6, mwaka huu.
Kinyaha alisema kutokana na uelewa mpana wa wakazi wa jimbo hilo ni wazi kuwa chama hicho ndicho kinachoweza kuibuka na ushindi kwani mtu anayegombea nafasi hiyo ni mpigania haki za wanyonge na anayetambua shida zinazowakabili kwa kipindi kirefu.
Alisema kumpitisha mgombea huyo hawakukurupuka bali walitumia utashi na heshima kubwa iliyomo ndani ya uongozi wa Chadema, hivyo mpaka sasa wanatambua kuwa, kazi wanayoifanya sasa ya kampeni si ya kubahatisha bali ni kushika uongozi wa ubunge ndani ya Jimbo la Chalinze.
 “Sisi leo tuko Kata ya Pera na Kijiji cha Chamakweza, tukiendelea na kampeni ambayo tuliizindua tangu Jumapili. Kikubwa ni kuzungumza na wananchi kwa ustaarabu na kuwajulisha chama wanachopaswa kukichagua ambacho ni Chadema pekee kinachojali shida za wanyonge,”

Alisema kuwa katika kipindi kifupi tangu chama hicho kilipozindua kampeni, hali ya mwitikio imekuwa ya kutia matumaini hususan katika mahudhurio ya kampeni kwenye maeneo mbalimbali na kudai hilo linaonyesha ni kukubaliwa kwa sera za chama hicho ambazo zaidi zinajikita kwenye kutetea wanyonge na usawa.
Alisema katika zoezi zima la kampeni, chama chao kitafanya kazi hiyo kwa ustaarabu na kuepusha vurugu na ni imani yake wana Chadema wote watajiepusha na hali yoyote inayoweza kutokea kwa upande wa vyama vingine.
Wakati huohuo juzi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza alisema katika kuhakikisha Uchaguzi wa Jimbo la Chalinze unafanyika kwa amani na utulivu  ni vyema viongozi wa dini zote wakafanya maombi kwa Mungu.
Alisema viongozi hao wanayo nafasi kubwa kutokana na imani tangu enzi na kuwataka kuhubiri mema kwa waumini wao ambao wengi ni wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo mdogo.
“Ndugu zangu viongozi wa dini, msijisahau katika maombi yenu ombeeni na huu uchaguzi mdogo utakaofanyika mapema mwezi ujao ili haki, amani na hekima itawale kwenye zoezi zima la kazi hiyo muhimu,” alisema.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE ANATARAJIWA KULIHUTUBIA BUNGE LA KATIBA LEO SAA 10:00 JIONI
Rais Kikwete akipitia hotuba inayotarajiwa kusomwa  katika Bunge Maalum la Katiba alipokuwa katika ndege kuelekea mjini Dodoma jana. 

Rais Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na ujumbe mzito wa marais na mawaziri wakuu wastaafu wa pande mbili za Muungano, leo atalihutubia na kulizindua Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, kulingana na Kanuni ya 75 (1) ya Bunge hilo.
Uamuzi wa kuambatana na viongozi wastaafu wa kitaifa unatafsiriwa na wengi kama ishara ya kuupa uzito mchakato wa Katiba Mpya na uhalali wa kisiasa na kuleta umoja na utengamano miongoni mwa makundi ya wajumbe wanaounda Bunge hilo la kihistoria.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa mjadala katika Bunge hilo, kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni juzi kabla ya Rais kuzindua Bunge kama Kanuni zinavyoelekeza.
Itakumbukwa kwamba mjadala huo ulizua mtafaruku baada ya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu hiyo Jumatatu iliyopita hadi kilipofanyika kikao cha maridhiano usiku wa siku hiyo na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu hiyo juzi na Rais ahutubie Bunge leo.
Mabishano hayo yalitokana na baadhi ya wajumbe kujenga dhana kwamba ukiukwaji huo wa Kanuni ulilenga kumpa Rais fursa ya kujibu mapigo na kupangua hoja za Jaji Warioba kutokana na wajumbe wengi wa chama chake cha CCM kuonyesha wazi kupinga na kubeza mapendekezo nyeti yaliyomo kwenye Rasimu hiyo, ambayo Jaji Warioba aliiwasilisha bungeni kwa ufasaha, umakini na ustadi mkubwa kiasi cha kuwafungua macho wengi, hasa pale alipowafafanulia mambo mengi ambayo wamekiri walikuwa hawayafahamu wala kuyaelewa.
Tunaupongeza uongozi wa Bunge na wajumbe wote kwa jumla kwa kutumia busara na kuendelea na shughuli za Bunge ambazo zilikuwa zimesimama. Vinginevyo, Bunge lingesambaratika na kufuta ndoto za wananchi za kupata Katiba Mpya inayokubalika kwa wengi. Hata hivyo, mtafaruku huo ulitoa somo kwa uongozi wa Bunge kwamba Bunge hilo lisipoendeshwa kwa kufuata na kuheshimu Kanuni zilizowekwa, litasambaratika.

  • Mheshimiwa Rais anatarajiwa kuambatana  na viongozi wastaafu wa kitaifa kama ishara ya kuupa uzito mchakato wa Katiba Mpya na uhalali wa kisiasa na kuleta umoja na utengamano miongoni mwa makundi ya wajumbe wanaounda Bunge hilo la kihistoria
Pamoja na kutoa pongezi hizo, tungependa kumshauri Rais Kikwete atambue kwamba leo atakuwa akilihutubia Bunge ambalo wajumbe wake wamegawanyika, hasa kutokana na msimamo wa CCM wa kuvikataa vifungu muhimu vya Rasimu ya Katiba. Tunasema hivyo baada ya viongozi na wajumbe wengi wa CCM kutoa kauli za kuendeleza misimamo mikali inayokinzana na maoni yaliyotolewa na wananchi na kuingizwa kwenye Rasimu hii ya Katiba.
Hotuba ya Rais inaweza kugusia maudhui yaliyomo katika Rasimu ya Katiba, lakini tunadhani kufanya hivyo itakuwa kosa kubwa kwa kua atakuwa ameingia katika mtego wa kujibu hoja zilizomo katika hotuba ya Jaji Warioba aliyoitoa juzi bungeni. Akifanya hivyo atakuwa analiingiza Bunge katika sintofahamu itakayolisambaratisha, kwani yeye si sehemu ya Bunge, bali  atakwenda pale kama mkuu wa nchi.
Kwa maana hiyo, hatutarajii alihutubie Bunge kuelezea misimamo yake binafsi au misimamo ya chama chake cha CCM au kundi jingine lolote lile.
Hivyo, atafanya vyema iwapo atakwenda pale kama kiunganishi muhimu cha makundi yote yaliyo bungeni. Tunadhani umoja, utengamano na nia ya serikali yake kuhakikisha Katiba Mpya inayokubalika kwa wengi inapatikana katika muda uliopangwa ndio mambo muhimu na ambao utalinusuru Bunge la Katiba.




Amos Wako aitahadharisha Tanzania kuhusu uundaji wa Katiba Mpya

By Beatrice Bandawe ;   21st March 2014

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya ambaye sasa ni Mbunge wa Busia Mashariki nchini humo, Amos Wako, akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Wako alikuwa akitoa uzoefu wa Kenya kwenye kuandika katiba mpya. Picha/Khalfan Said
Watanazania  wametahadharishwa kutoiga uzoefu wa mchakato wa kupata katiba mpya kutoka nchi nyingine za Kiafrika ikiwamo Kenya kwa kuwa mchakato huo sio Biblia.

Seneta Amos Wako, Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa serikali ya Kenya, aidha, alisema sababu nyingine ni kila nchi kuwa na mazingira yake.

Akitoa mada kwenye semina ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba jana mjini hapa, Seneta Wako alisema mifumo ya upataji katiba unatofautiana kati ya nchi na nchi.

“Natoa tahadhari, msiige uzoefu kutoka nchi nyingine, inaweza kuwa isiwe na faida kwenu, hii siyo Biblia," alisema.

Alisema  katiba yao ina mfumo wa  mgawanyo wa madaraka kwa sababu wakati inaundwa Wakenya wengi waliona madaraka mengi yanapaswa kwenda kwa wananchi na kwamba baada ya kupatika kwa katiba hiyo, iliundwa Tume ya kusimamia utekelezaji wa Katiba.

Seneta Wako aliyeshika wadhifa huo katika awamu mbili za uongozi za Daniel Arap Moi na Mwai Kibaki, alisema tume hiyo ni huru ambayo inafuatilia utekelezaji wa katiba na kutoa ushauri kwa serikali.

Alieleza kuwa eneo ambalo Tume hiyo ilifanikiwa ni siku ambayo Rais wa Kenya  alipowateua Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu kwa siku moja na ilisema ni kinyume na katiba na bunge lilisema ni kinyume na katiba na kuwa uamuzi ulitenguliwa.

Aidha, alisema waliona hakuna mfumo mzuri wa mgawanyo wa rasilimali na mgawanyo wa bajeti mahali ilipo serikali au kuliko na wananchi wengi ambako hakuna maendeleo kuwe na umuhimu wa pekee katika katiba.

Pia, alisema Katiba ya Kenya ina mfumo wa majimbo 47 ya utawala na kuwa wakati Kenya inapata uhuru kulikuwa na wilaya 42 na kuwa  inaonekana  huo utakuwa mwanzo mzuri.

Alitoa mfano kwamba jimbo lake la Busia ambalo lina wabunge saba, majimbo mengi ya Kenya yana wajumbe watano na maeneo katika Jiji la Nairobi yana wabunge 16.

Alisema kila jimbo kuna seneta mmoja na vile vile kuna Gavana ambaye ni kama afisa mtendaji mkuu wa eneo na ana kamati ya watendaji inayomzunguka katika kutekeleza majukumu.

Alisema baada ya kupitishwa kwa Katiba ya Kenya kwenye mikutano ya hadhara magavana hao wanaonekana kama marais wa maeneo wanayotoka na wajumbe wa kamati ya utendaji wanajiita mawaziri katika maeneo husika.

Seneta Wako alisema mfumo huo wa mgawanyo wa madaraka ni wa pekee na unatumika Kenya na kwamba huenda usifanye kazi sehemu nyingine.

Alisema walioamua kufanya hivyo ili kupata maendeleo ya haraka na kwamba umepata mafanikio kutokana na hivi sasa halmashauri nyingi kujiendesha zenyewe.

Kadhalika, Seneta Wako alisema kuwa katiba mpya ya Kenya imempunguzia Rais madaraka ya uteuzi kutokana na maofisa waandamizi kuomba kazi hizo.

Kwa mfano, alisema kuwa nafasi za Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mawaziri hawateuliwi na rais moja kwa moja, bali nafasi zao hutangazwa na baadaye hufanyiwa usaili kupitia televisheni na baadaye walioshinda kuthibitishwa na Bunge.

Akiuliza swali kuhusu uzoefu huo, Mjumbe Profesa Abdallah Safari alisema, ibara  8-178 ya Katiba ya Kenya, inasema Kiswahili ndio lugha ya taifa ya Kenya, lakini katika mikutano ya hadhara na hata elimu nchini humo inatolewa kwa Kiingereza na mfano mzuri ni yeye (Wako) kutoa mada yake kwa Kiingereza jana, hivyo anatoa ushauri gani kuhusiana na namna ya kukienzi Kiswahili?

Mjumbe mwingine, Dk. Nancy Mrikaria alitaka kujua kwa nini michakato ya katiba inayofanyika katika nchi za kiafrika kunatokea matatizo ya watu kupoteza maisha na wengine kuishia jela.

Naye Job Ndugai alitaka kujua Wako anachukuliaje  akiwa mshiriki mkuu wa kuandika rasimu ya  katiba ya Kenya na ilipopelekwa kwa wananchi ilishindwa?

Akijibu hoja hizo, Seneta Wako alisema Kiswahili ni lugha ya taifa nchini Kenya, lakini kutokana na Wakenya wengi kutoizungumza vizuri, wanaendelea kujifunza.

Hata hivyo, alisema kwa sasa Wakenya wengi wanajitahidi kuzungumza lugha hiyo.

Kuhusu rasimu ya kwanza kutokubaliwa, Seneta Wako alisema hali hiyo ilitokana na mchakato wake kushirikisha wajumbe wengi wa chama tawala bila kushirikisha vyama na taasisi zingine.

Akizungumzia vurugu, alisema alisema hali hiyo inatokana na  mchakato huo kuwa jambo jipya, ambalo  siyo rahisi kukubalika kwa urahisi.
 
SOURCE: NIPASHE 

Amos Wako: Msipuuze maoni ya wananchi

Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali ya Kenya, Seneta Amos Wako akizungumza jana, wakati wa Semina ya Bunge Maalumu la Katiba. Picha na Salim Shao 
Na Habel Chidawali na Editha Majura, Mwananchi
  • Awataka Wajumbe wa Bunge la Katiba watunge Katiba inayotokana na maoni na matakwa ya wananchi ili kuepusha migogoro.

Dodoma. Mwanasheria Mkuu (AG) mstaafu wa Kenya, Amos Wako amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutokupuuza maoni ya wananchi katika kutunga Katiba ya nchi vinginevyo watazua mgogoro.
Wako, ambaye kwa sasa ni Seneta wa Busia ya Mashariki nchini Kenya, alitoa ushauri huo jana katika semina kwa wajumbe wa Bunge la Katiba kuhusu uzoefu wa namna nchi hiyo ilivyopitia misukosuko ya kuipata Katiba mpya.
Wako ambaye kwa miaka 21 alikuwa katika wadhifa wa AG, alisema matukio mengi yaliyosababisha Kenya kutokupata Katiba yao kwa wakati, yalitokana na kutokuwashirikisha wananchi moja kwa moja katika mchakato.
Katika hotuba yake iliyodumu kwa saa 2: 11, mwanasheria huyo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya alionya pia kuwa Katiba inayotengenezwa hapa nchini isiwe ya kunukuu kutoka katika mataifa mengine kwa sababu mahitaji yanatofautiana kwa kila nchi.
“Katiba isiwe ya mazungumzo kutoka kwa viongozi pale Dar es Salaam, kwani itakuwa ni mali ya watu wachache na ambayo lazima itapingwa, hata sisi tulianza hivyo lakini tulishindwa vibaya,” alionya Wako.
Aliimwagia sifa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni Jumanne iliyopita, kwamba kwa mtindo ilivyowasilishwa inaonekana kuwajali na kuwapa nafasi zaidi wananchi wa hali ya chini.
“Pamoja na hayo, lakini Katiba hii ikiingiliwa zaidi na kutekwa na wanasiasa au kikundi cha watu wachache kwa masilahi yao, inaweza kuharibika kama ilivyotokea kwetu Kenya ambako Kanu walikuwa wakipinga kila kitu wakatufanya tuingie katika mgogoro.”
Alisema kuwa mitazamo ya wanasiasa huwa ni tatizo na hatari katika kutafuta Katiba mpya na dawa pekee na ya maana ni kutoa nafasi kwa wananchi waamue wenyewe.
“Mfumo uliowekwa katika mchakato wa kuunda Katiba mpya nchini kwenu, kwamba Rasimu ya mwisho ya Katiba itoke bungeni na kupelekwa moja kwa moja kwa wananchi ni mzuri, ni muhimu maoni ya wananchi ya awali yazingatiwe,” alisisitiza.
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, Bunge Maalumu limeaminika kufanya kazi hiyo ili kuwasaidia wananchi kufikia malengo yao.
Uzoefu wa Kenya
Akizungumzia uzoefu wa Kenya katika kupata Katiba mpya alisema walianza kwa kukabiliana na changamoto kubwa ya ukabila ambayo kila jamii ilikuwa haiamini kundi jingine katika kutafuta usawa, jambo alilosema ni tofauti na Tanzania.
 
 
 
 
 

Wednesday, March 19, 2014

Matukio katika picha wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam

image




















Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (mwenye tai nyekundu), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ndg John Mngodo (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi wa Wizara Ndg. Kirenga Ndemino (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) Ndg. Ephraim Mgawe (wa kwanza kulia) wakimsubiri Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe Dkt Mary Nagu kabla ya ufunguzi wa Kituo cha Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.

image

























Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu (MB) siku ya Alhamisi tarehe 26 Julai 2012, alizindua rasmi Kituo cha Uwekezaji (One Stop Centre) kilichopo katika Bandari ya Dar es Salaam. Kituo hiki kitakuwa na ofisi zifuatazo; TBS, TFDA, TAEC, GCLA, TFS, Port Health, Plant Health na Zoosanitary.
 Wadau mbalimbali wakisubiri ujio wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu kabla ya uzinduzi wa Kituo cha Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.

image

 image


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(mwenye tai nyekundu) akimtambulisha Mhe.Dkt Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji kwa Meneja Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam.
image image

 
image.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (mwenye tai nyekundu), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ndg John Mngodo (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi wa Wizara Ndg. Kirenga Ndemino (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) Ndg. Ephraim Mgawe (wa kwanza kulia) wakimsubiri Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe Dkt Mary Nagu kabla ya ufunguzi wa Kituo cha Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.

image.

image

Wadau mbalimbali wakisubiri ujio wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu kabla ya uzinduzi wa Kituo cha Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.

image

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(mwenye tai nyekundu) akimtambulisha Mhe.Dkt Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji kwa Meneja Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam.

image

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (mwenye tai nyekundu) akimtambulisha Mhe.Dkt Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Ndg Ephraim Mgawe. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Ndg. John Mngodo (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Ndg. Kirenga Ndemino (wa tatu kushoto).


 image
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu akibalishana mawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ndg Penaeli Lyimo (wa kwanza kutoka kulia) kabla ya ufunguzi wa Kituo cha Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.
 image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu akisikiliza hotuba ya Mkurugenzi wa Shirika la Msaada la Marekani (USAID) Tanzania Bw. Robert Cunnane (aliyesimama). Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo(wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ndg Penaeli Lyimo(wa kwanza kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ndg Ephraim Mgawe.

 image
 image
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kituo cha Uwekezaji. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
Mhandisi Omar Chambo (wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ndg Penaeli Lyimo(wa kwanza kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ndg Ephraim Mgawe(wa kwanza kutoka kushoto).

 image
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo (wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ndg Penaeli Lyimo (wa kwanza kutoka kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Msaada la Marekani (USAID)Tanzania Bw. Robert Cunnanena (wa tatu kutoka kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndg Ephraim Mgawe (wa pili kutoka kushoto) na Meneja Mkuu Bandari ya Dar es salaam (wa kwanza kushoto).
 image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Uwekezaji huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
Mhandisi Omar Chambo (mwenye tai nyekundu), Meneja Mkuu Bandari ya Dar es salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Msaada la Marekani (USAID) Tanzania Bw. Robert Cunnanena
wakishuhudia.