Rais Jakaya Kikwete alihutubia Bunge Maalumu la Katiba.
Awaonya wabunge wa bunge Maalumu la katiba kuhusu mgawanyiko,awataka wawe wamoja na wazingatie maslahi ya Taifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JakayaMrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelihutubia bunge
maalumu la Katiba na kutaka wajumbe wa bunge hilo kuhakikisha kuwa
katiba inayopatikana itakuwa ni katiba yenye kuheshimu haki za binadamu,
kudumisha upendo, katiba inayotekelezeka, na wananchi kunufaika na
maendeleo yatakayopatikana kutokana na katiba hiyo.
Aidha amewataka wajumbe hao kusoma na kuelewa kilichoandikwa na
kufanya uamuzi mzuri wa mawazo yao binafsi pasipo kushauriwa na wenzao
ama makundi .
Rais Kikwete amesema kuwa wajumbe hao wana wanawajibu wa kuchambua
kwa kina rasimu hiyo ya pili ya katiba kifungu kwa kifungu, ibara kwa
ibara, sentensi kwa sentensi, neno kwa neno, na kuboresha pale wanapoona
panastahili maboresho na ikiwa kuna jambo ambalo halifai wanao wajibu
wa kuliondoa ili kupata katiba itakayo dumu kwa muda mrefu.
Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kufanya mchakato wa kuwa na katiba
mpya ambapo mwaka 1965 iliandaliwa katiba ya muda na mwaka 1977 katiba
ya kudumu ilitengenezwa ambayo ndiyo inatumika hadi sasa.
Mchakato wa sasa wa katiba mpya ya Tanzania kwa mara ya kwanza
umewashirikisha wananchi ambao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho kuhusu
katiba hiyo kwa kupiga kura ya maoni.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Kikwete, anazindua Bunge Maalum la Katiba hapa Dodoma kuanzia saa 10 kamili jioni. Katika uzinduzi huo, Rais Kikwete ameambatana na ujumbe mzito kama vile Marais Wastaafu wa pande mbili za Muungano, wake wa waasisi wa taifa, na mawaziri wakuu wastaafu.
Kwenye msafara huo ni pia yupo Rais mstaafu Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dr Salmin Amour, Aman Abeid Karume, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. wengine ni Jaji Joseph Sinde Warioba, Cleopa Msuya, John Malecela, Dr Salim Ahmed Salim, Friedereck Sumaye na Edward Lowasa. Mbali na viongozi hao, pia Rais Kikwete ataambatana na Rais wa Zanzibar, Mr Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Seif Sharif Hamad na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa bunge la katiba.
Pia wapo wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii, wawakilishi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa, mabalozi wa nchi mbalimbali na wengineo.
Imeripotiwa kuwa viongozi wakuu wa vyama vya Upinzani, Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamepongeza uamuzi huo wa Rais kuambatana na msafara huo. Pia wamewaomba wabunge wenzao hasa wa upinzani kuonesha hali ya utulivu wakati wote wa tukio hilo muhimu la kihistoria.
--------------------------------------------------------------------------------
Kinachojiri sasa Bungeni; kwa maandalizi ya Hotuba ya Rais Kikwete
--------------------------------------------------------------------------------
- Wabunge wanaingia kwa wingi ukumbini. Naona leo hali ya mahudhurio imekuwa nzuri
- Kwa mujibu wa Ratiba ni kwambq kikao cha abunge kilipaswa kuanza saa 9.10. Ila ratiba huenda itachelewa kidogo. Wageni waliofika ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Mkuu wa Tanzania na Zanzibar
- Mzee Karume naye yupo nje ya viwanja vya bunge
- Naam namuona Mheshimiwa Freeman Mbowe anawasili na sasa anateta jambo na ajames Mbatia
- Naam, kule nje namuona Makamu wa Rais, Gharib Bilal
- Hakika ukumbi wa bunge umependeza sana leo. Wabunge wengi wamejitokeza na kuna wageni wengi pia
- Naaam sasa Rais JK anaingia Ukumbini kwa kupitia ule mlango wa VIP
- Mheshimiwa Abeid Amani Karume sasa Anaingia
- Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi anaingia sasa
- Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Makungu anaingia Bungeni sasa
- Jaji Mkuu, Mohamed Chande aorhman anaingia sasa
- Makamu wa Kwanza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anaingia ukumbini
- Anayefuata ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Mohamed Shein
- Anayefuata ni Makamu wa Rais, Dr Mohamed Ghalib Bilal
- Wageni wote muhimu wamewasili na sasa anayesubiriwa ni Mheshimiwa Rais kuingia Bungeni
- Naam mzee wa Speed and Standard anamsindikiza Rais JK kuingia ukumbini. Mayowe yanapigwa kuashiria furaha ya wabunge. Namuona mheshimiwa mnyaa anapiga meza muda wote
- Mzee Malecela naye yumo. Pia kuna Pius Msekwa, mama Maria Nyerere na wake za viongozi
--------------------------------------
- Rais JK anaanza kuhutubia kwa kucheka na kusema "haijapata kutokea". Sijui ana maana gani...
- Rais anawaponyeza Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwa kishindo. Anawapongeza pia wabunge kwa fursa hii waliyopata ya kuwa wabunge wa bunge la katiba. Anasema kuwa wabunge watatunga katiba inayokubalika na watanzania, inayotekelezeka, itakayoondoa changamoto za muungano zilizopo, itakayoimarisha muungano, itakayodumisha amani na usalama, itakayostawisha demokrasia, kuimarisha utawala wa kisheria, kupunguza maovu, kukuza uchumi na kuleta maendeleo sawia kwa wananchi
Rais anasema kuwa hii ni mara ya Tatu Tanzania kuandaa katiba. 1965, 1977 na huu wa sasa. Ila anasema huu wa sasa unashirikisha wananchi kwa kutoa maoni yao, mabaraza ya katiba na kwa kura ya maoni. Tofauti na michakato iliyotanguloa ambapo ni wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano tu, mchakato wa sasa una wengi na unashirikisha makundi mengi
Rais anasema kuwa kelele za kutaka kuwa na katiba mpya zimekuwepo sana wakati wa mfumo wa vyama vingi
Anampongeza jaji Warioba na wajumbe wote wa tume.
Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo anataka litafakariwe kwa makini. Anawataka wajumbe watafakari kwa kina kuhusu hilo. Kwamba lina uzuri na ubaya wake
Sasa anajadili kuhusu muundo wa Muungano. Anasema kuwa jambo hili limezua mjadala mzito tangu Rasimu ya mwanzo hadi ya mwisho. Anasema kuwa jambo hilo linasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi. Karika hilo anaroa ushauri ufuatao
- Wabunge waepuke jazba wakati wa kujadili suala hilo
- wajumbe watafakari madhara yanayoweza kujitokeza iwapo jambo hilo halitapatiwa ufumbuzi kwa njia ya utulivu
- Anasema kuwa mjadala wa muundo wa katiba moya si mheni kama alivyoeleza Warioba. Kwamba mwaka 1984 ulikuwa chanzo cha machafuko Zanzibar. Pia mwaka 1993 jambo hilo lilikuwa ni chanzo na G55
- Rais Kikwete anasema kuwa sababu za kuwa na serikali mbili ni mbili
- Kuhakikisha kuwa Zanzibar haimezwi kwenye Muungano
- kuepuka gharama kwa Tanzania Bara kugharamia serikali ya bara na ya muungano
- Rais anasema kuwa kwa mujibu wa Jaji Warioba ni Muundo wa serikali Tatu, umependekezwa kutokana na sababu mbili.
- Kwamba watanzania wengi wamependekeza muundo huo
- unatoa majibu ya matatizo ya serikali mbili
No comments:
Post a Comment