Maalim Seif alipowasili Mjini Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Ufunguzi wa Bunge Maalum la Katiba ,litakalohutubiwa na Rais Kikwete,
Thursday, March 20, 2014
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif amewasili
Mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba
utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete.
Katka uwanja wa ndege wa Dodoma, Maalim Seif amepokelewa na viongozi wa
Mkoa huo pamoja na Wabunge, Wawakilishi na viongozi mbali mbali wa CUF.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na Mbunge wa Mji Mkongwe Mhe. Ibrahim Sanya, baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Dodoma.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Dodoma. (Picha na Salmin Said, OMKR)
No comments:
Post a Comment