Idadi kubwa ya wafanyabiashara KARIAKOO hawalipi kodi
Fri Jan 23 2015
Waziri wa fedha SAADA MKUYA
Idadi kubwa ya wafanyabiashara wa eneo la kariakoo jijini dsm, hawalipi kodi baada ya wafanyabiashara hao kuonekana kuuza bidhaa zao bila kutumia mashine za elektroniki za kutolea risiti- EFD.
Wafanyabiashara hao pia wanakwepa kodi kwa kutoa risiki faki kwa kutumia vitabu ambavyo havitambuliki na mamlaka ya mapato nchini TRA na wafanyabiashara wengine wanauza bidhaa zao bila kutoa risiti.
Hayo yamegundulika wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na na Waziri wa fedha SAADA MKUYA kwenye maduka yaliyopo eneo la KARIAKOO ambapo amewataka wafanyabiashara hao kutoa risiti kwa kutumia mashine za EFD.
Mmoja wa wateja wa wafanyabiashara hao amedai kuwa hiyo ni kawaida kwa baadhi ya wafanyabiara wa kariakoo kutoa risiti feki kwa visingizio mbalimbali ikiwemo mashine za EFD kushindwa kufanyakazi.

No comments:
Post a Comment