Thursday, January 1, 2015

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Philip Mangula amesema kuwa kikao cha kamati kuu kinachoundwa na wajumbe 14 (7 kutoka kila upande wa muungano) kimeitishwa kujadili hatima ya mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Prof Anna Tibaijuka (Pichani).

Kikao hicho kitaamua hatma yake ikiwemo ama kubakizwa katika kamati hiyo,kufukuzwa au kunyanganywa kadi na kufukuzwa kabisa katika chama kutokana na sakata la Escrow ambapo yeye alipata mgao kutoka kwa mmoja wa wabia wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

No comments:

Post a Comment