MTI WA MWAROBAINI
HUTIBU MAGONJWA YA NGOZI
The Fadhaget Sanitarium Clinic siku ya leo imeona itoe elimu ya faida za
mti wa mwarobaini hasa katika suala zima la magonjwa ya ngozi
yanayosumbua sana wanadamu.
Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa
kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko
India na Burma . Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na
una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini Tanzania, mti wa mwarobaini
huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na
vijijini.
Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu
magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mbegu za mwarobaini vimekuwa
vikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu katika nchi mbalimbali duniani.
Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja na
matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi,
malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na
magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.
Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni.
Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu
wanaoharibu mimea shambani.
Tumekwisha ziona faida mbalimbali za mti wa mwarobaini, leo
nitakufundisha namna ya kutumia mti wa mwarobaini kujitibu magonjwa ya
ngozi.
MAHITAJI :
Majani ya mti wa mwarobaini.
Sufuria
Mwiko
Jiko la gesi, mkaa au jiko la mafuta.
HATUA ZA KUFUATA:
Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye
sufuria.
Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na ui injike
kwenye jiko lenye moto wa wastani.
Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi
yakauke bila kuungua.
Majani yako yakiisha kauka, ipua sufuria yako, chukua majani yako
yaliyo kauka, yasage kisha hifadhi unga unga wako kwenye chombo cha
plastiki.
MATUMIZI :
Tumia vijiko viwili vya chai kwenye kikombe cha robo lita chenye maji ya
moto, mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment