Muarobaini kudhibiti magonjwa ya mikorosho
Wakati
dawa na sumu za viwandani zinaendelea kushika kasi kubwa katika
kudhibiti madhibiti magonjwa ya mimea, utafiti wa matumizi ya muarobaini
kudhibiti magonjwa ya mikorosho umetoa matokeo ya kuridhisha.
Matokeo hayo ya matumzi ya dawa za asili zisizo na kemikali yanayotoa faraja kubwa, kwa watu wanaohitaji mazao yatokanayo na kilimo kinachotumia mbinu za kiasili za kudhibiti visumbufu vya mimea (Kilimo Hai) na kupunguza ongezeko la sumu katika mazingira ya kilimo ili kutoa nafasi kwa viumbe rafiki wa mkulima, kuzaana, kuongezeka na hatimaye kupunguza visumbufu kwa njia asilia.
Utafiti unafanywa na kampuni iitwayo Neem Botanical Phamacy Roy ya Tanga kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania, kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao ya kilimo Naliendele Mtwara (NARI) kwa ajili ya kutibu zao la mkorosho kwa kutumia muarubaini.
Mkurugenzi wa Neem Botanical Phamacy Roy Nicolaus Erio akizungumzia utafiti huo anasema kuwa,wanatumia dawa za asili kama mbinu mpya ya za kiasili za kudhibiti visumbufu vya mimea ili kupunguza ongezeko la sumu katika mazingira ya kilimo na kutoa nafasi kwa viumbe rafiki wa mkulima, kuzaana na kuongezeka kisha kupunguza visumbufu kwa njia asilia.
“Baadhi ya dawa zenye kemikali hukaa muda mrefu bila kuisha nguvu….baada ya mboga kuvunwa na kutumiwa kama chakula kemikali hujikusanya kwenye mwili wa binadamu na matokeo yake ni kusababisha magonjwa yakiwemo kansa. Hii ni tofauti na dawa za asili ambayo huishiwa nguvu haraka, hivyo hayana madhara kwa binadamu,” anafafanua mtaalamu huyo na kuendelea.
“Dawa za asili ni viuatilifu (dawa) zinazotokana na vitu vya asili kama mimea, mifugo, udongo na majivu yanayotumika kuzuia au kuangamiza magonjwa na wadudu waharibifu.Baadhi ya dawa au mimea hii, hutoa sumu inayonyunyiziwa dawa hizi za asili na matokeo yake ni kuwa
mashambulizi yanapungua, mavuno na ubora wa mazao vinaongezeka bila kuharibu mazingira,” anafafanua Mtaalamu wa Erio.
Kimsingi Erio anasema kuwa, kinachohitajika ni kudhibiti visumbufu vya mimea kwa kutumia viuatilifu mbadala ambavyo ni salama kwa mimea, watumiaji, walaji na mazingira yanayotokana na madhara yatokanayo na sumu za viwandani hivyo kudumisha uzalishaji endelevu na salama bila kutegemea sana sumu za viwandani.
Ndio maana kampuni yake anasema kuwa, imeungana na Bodi ya korosho Tanzania kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele Mtwara (NARI) kwa ajili ya kutibu zao la mkorosho kwa kutumia muarobaini.
Mradi huo kwa mujibu wa Erio, ulionyesha mafanikio makubwa kwa kutibu mikorosho mingi iliyokuwa imeshambuliwa na magonjwa mbalimbali tena kwa gharama nafuu.
Dawa ya muarobaini kwa ajili ya mimea inakinga mimea isishambuliwe na wadudu gharama zake ni nafuu sana ikilinganishwa na zile za kiwandani.
“ Dawa ya asili ya kudhibiti visumbufu yapo kwenye mazingira yetu, hivyo mkulima anaweza kuongeza kipato kwa gharama nafuu…baadhi ya visumbufu vimekuwa sugu kwa sumu za viwandani,”anasema Erio.
Kampuni ya Neem ilianzishwa mwaka 1999 chini ya usimamizi wa Mzee Nicolaus Erio ( kwa sasa marehemu) kwa lengo la kufanya utafiti wa tiba kupitia zao la muarobaini kwa wanyama, binadamu na mimea. Utafiti huo,ulianza kupata mafanikio ya kubaini dawa mbalimbali za magonjwa yanayoshambulia makundi hayo matatu.
Mwaka 2002 walianza kutengeneza dawa kwa kutumia zao la muarobaini kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa wanyama, mimea na binadamu.
Baadhi ya bidhaa zitokanazo na muarobaini Erio amezitaja kuwa ni sabuni za kutibu magonjwa ya ngozi, cream kwa walioathirika na mkorogo, dawa za kisukari, dawa za kifua na pumu, dawa ya malaria, meno na kwa ajili ya madonda sugu.
Dawa ya muarobaini hutumika kutibu na kuua wadudu wanaoshambulia mimea na ugonjwa wa ukungu. Kwa upande wa wanyama, hutibu aina zote za minyoo ya mifugo, magonjwa ya kideri kwa kuku na kuogeshea wanyama.
Kama hiyo haitoshi, kampuni hiyo sasa ipo katika utafiti wa dawa za magonjwa yanayoathiri minazi hususan ile iliyopo katika maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi.
“Minazi mingi iliyopo katika Pwani ya bahari ya Hindi imeathiriwa na magonjwa …tumeanza utafiti wa tatizo hilo na tunataka tiba ipatikane kwa kutumia muarobaini,” anasema.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, hakuna kinachotupwa katika matumizi ya zao hilo kutokana na ukweli kuwa kila kiungo cha mti huo kimekuwa na matumizi yake tofauti.
“Kuanzia majani, mbegu,maua,mizizi na kila sehemu zina kazi tofauti katika utoaji wa tiba iwe ya mimea, binadamu au wanyama.Hata mabaki ya muarobaini ni mbolea ya asili ya kukuzia mimea na kuua wadudu shambani, “ anasema Erio.
Kuhusu soko la bidhaa zitokanazo na muarobaini, anasema kuwa, soko lipo ndani na nje ya nchi, na kwamba kwa wote waliozitumia zimeleta mafanikio makubwa kimatibabu.
“Nchi jirani kama Kenya, Congo na Rwanda wanazipenda sana hasa wale wenye hoteli za kitalii hununua kwa ajili ya matumizi ya hotelini,”anasema.
Kwa upande wa malengo ya baadaye,anasema ni kujenga kiwanda kikubwa kitakachotengeneza bidhaa zitokanazo na muarobaini, na shule itakayofundisha umuhimu wa matumizi ya bidhaa za asili kama muarobaini katika utoaji wa tiba kwa magonjwa ya wanyama,mimea na binadamu.
Kampuni hiyo imekuwa ikinunua bidhaa za muarobaini kutoka kwa wananchi na ina shamba kubwa la zao hilo.
“Tuna shamba kubwa la miarobaini tu…ambalo halitoshi hivyo tunanunua mbegu na majani ya muarobaini kutoka kwa wananchi. Nawashauri wananchi wasikate miti ovyo kwani ni rasilimali kubwa sana na muhimu kwa jamii yetu hasa katika suala zima la hifadhi ya mazingira ,“Anasisitiza.
Kampuni hiyo, imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) cha Morogoro kila mwaka kwa ajili ya kujifunza namna zao hilo linavyofanya kazi kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho.

No comments:
Post a Comment