Wednesday, March 26, 2014

Bunge Maalum la Katiba lashindwa kuendelea na kikao chake Jioni ya leo kwa kile kinachodaiwa na wajumbe kuwa ni ukiukwaji wa kanuni, 26 March 2014

habari
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Fenella Mukangara (kulia) na Anne Kilango Malechela(kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.
kajubi
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kajubi Mwakajanga (kushoto) na Yusuph Omar Chunda(kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.
kigunge
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Paul Makonda(kulia),Anne Makinda(wa pili kulia),Yusuph Singo(wa pili kushoto)  na Kingunge Ngombale Mwiru(kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.
makaidi
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kingunge Ngomabale Mwiru (kushoto) na Dkt.Emmanuel John Makaidi(kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.
mbowe
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Profesa Ibrahim Haruna Lipumba (kushoto) na Freeman Mbowe(kulia)  wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika kikao cha Bunge hilo.
ukawa
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambao pia ni wanachama wa UKAWA wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika kikao cha Bunge hilo.
ndungai
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akibadilishana mawazo leo mjini Dodoma  na waandishi wa habari kabla ya kikao cha Bunge hilo.
mwenykit
Mwenyekiti wa  Bunge Maalum la Katiba  Samwel Sitta akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
sita
Mwenyekiti wa  Bunge Maalum la Katiba  Samwel Sitta akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali leo mjini Dodoma kabla ya  kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.(Picha na Tiganya Vincent, Dodoma).

Tuesday, March 25, 2014

 Washiriki wa Maisha Plus walivyoingia kijijini jana Jumatatu  Machi 24, 2014

Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi...
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao.
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).
Mkuu wa Kijiji... Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe.
Wageni waalikwa. 
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. 
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa. 
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini. 
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5.
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka... wengine walitamani kughairi kuendelea na safari.
Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo.
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe...
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo. 
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 

Tressa yazinduliwa rasmi jijini Mwanza

Hatimaye bidhaa ya vipodozi vya nyewele ya Kitanzania ijulikanayo kama TreSSa Proffesionals imezinduliwa leo katika hoteli ya Golden Crest ,jijini Mwanza. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wamiliki wa saluni, wanamuziki na wanamitindo maarufu na waandishi wa habari. 
TreSSa Proffesionals ni bidhaa mpya ya vipodozi vya nyewele iliotengenezwa mahususi kwa ajili ya nywele za mwanamke wa Kitanzania. Tressa Professionals ni ubunifu kwenye tasnia ya utunzaji nywele, ikiwa na mchanganyiko wa kipekee wa sayansi na asili. 
Bidhaa za TreSSa zina viungo kama vile; Parachichi, Mafuta ya Jojoba, Indian Hemp na protini za nywele kama vile Keratin. Bidhaa hizi vimefanyiwa uchunguzi na kujaribiwa kwenye nywele za Kitanzania na kumpa Uhuru mwanamke wa Kiafrika wa kutokatika kwa nywele. 
Sasa mwanamke ana uhuru wa kuchagua bidhaa inayoendana na mtindo wa nywele aupendao. TreSSa ina bidhaa mbalimbali za vipodozi vya nywele zikiwemo; Relaxers (aina ya regular na super), Neutralising plus Strengthening Shampoo inayoweza kutumika kila siku, Hair Food (iliyo na mafuta ya Jojoba na Indian Hemp) inayong’arisha na kupoza nyewele na ngozi ya kichwa, Moisturising Pink Lotion kwa matumizi ya kila siku na Hair Mayonnaise iliyo na protini kwa nywele zenye afya.
 Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Mkuu was masoko , Chemi cotex, Bwana R.N. Ojha, alisema, “Kampuni ya Chemicotex imekuwa mstari wa mbele kuleta bidhaa zenye ubora kwa watu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. TreSSa ni mfano wa ahadi endelevu wa ahadi zetu wa kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa watu wa Tanzania”. 
 Tressa Professionals ni bidhaa iliyotengenezwa na kampuni ya Chemicotex, ambao ni watengenezaji maarufu wa dawa ya meno ya Whitedent na Bannister’s Glycerine. Afisa Meneja wa kitaifa was biashara wa masoko, Chemicotex, Bwana Manoj Kumar, alisisitiza, “Utafiti umetuonyesha kwamba utunzaji wa nywele ni jambo la muhimu kwa wanawake wa Kitanzania. Hatimaye TreSSa imewapa wanawake uhuru wa kutokatika kwa nywele, ambalo ni tatizo kwa wanawake wengi wakati wakitengeneza nywele.” 
 Tuna mipango ya kuwafikia wanawake wote nchini kupitia semina, warsha, vipindi vya tv na ushirikiano wetu na saluni ili kuhakikisha mwanamke anapata fursa ya kutengeneza mitindo ya nywele aipendayo kwa kutumia TreSSa.” 
Bwana Ojha aliongezea alipokuwa akizungumzia mipango ya TreSSa. Kampuni hii ina mipango madhubuti ya kimasoko na kuitangaza bidhaa ya TreSSa, aidha kampuni ina malengo ya kumiliki asilimia 25 ya soko la utunzaji nywele ndani ya miaka 3.









 Chemi Cotex the manufacturers of popular brands such as the Super brand White dent Toothpaste , Bannister's cream and Glycerine has launched its new range of hair care products under the Brand name “Tressa Professional” in a star studded ceremony held at the Golden Crest hotel mwanza on the 24th of March 2014 . The event which was graced by  Top Salon owners, celebrities of the fashion and music world , members of the press and top management of Chemi Cotex.

“Tressa Professionals” range is an innovation in the hair care industry and has a combination of natural ingredients and science and has been made by one of the top manufacturers in South Africa. The product has been researched and tested on Tanzanian hair and give the African woman freedom from hair breakages, and also gives her the choice to choose products best suited for her hair.

The Tressa range has products like Relaxers (both regular and super), hair food with Jojoba oil and Indian hemp, Moisturising pink lotion, Neutralizing plus strengthening shampoo and hair mayonnaise. The products have been fortified with the goodness of keratin which is a relatively new concept in Tanzania.


With this initiative, and thanks to the special dose of magic during the launch that defined a new concept in the hair care category, Chemi & Cotex industries limited  has created a more direct and emotive link with all women who identify and express themselves with the need for good quality products in Tanzania. Chemi Cotex the dominant ORAL CARE player in Tanzania is redefining its international character by this inspirational development and launch of the world class “Tressa Professional” range.  

Le sel South Africa one of the most internationally experienced companies in the field of hair care, has worked with Chemi Cotex for developing this range for their new venture into the world of hair care.
CHEMICOTEX is one of East Africa’s leading fast moving consumer goods companies .The company‘s largest and best know brand is Whitedent toothpaste which is used by more than 20 million Tanzanians everyday ! Whitedent is the clear market leader in Tanzania and is also available to consumers in Rwanda, Kenya, Zambia, Malawi and South Africa

WATENDAJI DAR WAASWA KUSHIRIKIANA ILI KUWEKA JIJI KATIKA HALI YA USAFI

DSC_1151
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande (mwenye suti ya damu ya mzee) akinyoosha kidole kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (wa pili kulia) sehemu korofi za kutiririsha maji machafu barabara ya Morogoro kati kati ya jiji. 

Na Damas Makangale

WATENDAJI wa Mamlaka za Maji Safi na Taka, Manispaa, Halmashauri, Wakala wa Barabara na Mabasi yaendayo kasi wameshauri kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na kushirikiana kwa pamoja ili kuleta tija katika usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu, kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo amesema kuwa tatizo la jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa mkoa hawana mawasiliano ya kutosha katika utendaji kazi wa kila siku.

Shayo alizungumza hayo kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya kugagua hali ya usafi katika maeneo kadhaa pamoja na kuangalia maeneo korofi katika kutitirisha maji machafu kwenye mitaro kadhaa kati kati ya jiji.

“tatizo kubwa katika jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa jiji, manispaa, wakala wa barabara, Tanesco na mamlaka za maji safi na taka kutokuwa na utaratibu wa kuwasiliana katika utendaji kazi wa kila siku katika kuboresha usombaji wa taka kwenye jiji la Dar,” amesema Shayo
DSC_1173
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande akiwaonyesha baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu baadhi ya mashimo (Potholes) ambayo ni hatari kwa wananchi watembea kwa miguu baada ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.

Shayo alilisisitiza kwamba katika utendaji kazi wa jiji kama la Dar inahitajika ushirikiano wa dhati kati ya wadau wa kusomba taka na watendaji wa manispaa pamoja na jiji ili kuweka mkoa wa Dar es Salaam katika hali safi wakati wote.

Amesema kuwa ingawaje tatizo kubwa la uchafu linasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara na maji hasa kuelekea katika dampo kuu la mkoa sehemu ya Pugu Kinyamwezi, Gongo la Mboto.

Shayo ambaye kampuni yake inajishughulisha na usombaji wa taka ngumu na nyepesi katika mkoa wa Dar es Salaam amesema kwamba mamlaka zinazohusika kwa kushirikiana na wadau lazima watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi taka.

“sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi. inahitajika kampuni ya ujenzi yenye uwezo wa kuboresha miundombinu ya barabara kuelekea kwenye dampo ili kupunguza foleni ya magari ya taka na kuongeza tija ya kazi katika eneo husika,” aliongeza
DSC_1231
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick akiongoza msafara wa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika kuangalia hali ya usafi na miundombinu ya maji na barabara jijini Dar.

Kwa upande wake, Minael Mshanga Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, amesema jiji limejipanga kufanya ukarabati wa miundombinu ya barabara kuelekea dampo ili kuongeza kasi ya magari yanayokwenda kumwaga taka katika dampo hilo.

“hivi tupo katika hatua za mwisho na tumempata mkandarasi wa kuja kujenga na kutengeneza miundombinu ya barabara kuelekea katika dampo pamoja na kutengeneza mataa katika eneo husika ili kazi ya kutupa taka ifanyike usiku na mchana,” amesema Mshanga.

Aliongeza kwamba jiji lina mpango wa kuanza kushirikiana kwa karibu na wakandarasi wazalendo katika kuleta ufanisi wa usombaji taka ili kuzuia magonjwa ya mlipuko katika mkoa wa Dar es Salaam.
DSC_1240
Mbunge wa Ilala, Hassan Zungu akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick wakati wa ziara ya ghafla ya kugagua hali ya miundombinu ya maji na barabara kati kati ya jiji la Dar.
DSC_1310
Baadhi ya magari ya wakazi wa jiji yakipita kwa taabu katika madimbwi na mashimo ya maji machafu kati kati ya jiji la Dar es Salaam.
DSC_1337
Viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakijadili moja ya sehemu korofi kati kati ya jiji karibu na Haidery Plaza ambapo kipindi cha mvua maji taka yaliyochanganyikana na kinyesi yanatuama kwa kipindi kirefu ambapo hakuna mfereji wala mtaro wa maji machafu.
DSC_1350
Mashimo ya miaka nenda rudi yasiyopatiwa ufumbuzi lakini baada ya ziara yatarekebishwa.
DSC_1402
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa ushauri kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala (mwenye tai nyeusi).
DSC_0468
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka jiji, Enezael Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya taka yanavyomwaga taka katika dampo kuu la Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.
DSC_0477
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima Enterprises, Robert Ngeleshi akizungumza changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo.
DSC_0514
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akielezea jambo kwa mkuu wa mkoa wakati wa kuhitimisha ziara hiyo katika maeneo ya dampo Pugu Kinyamwezi.
DSC_0531
Moja ya Bull dozer linalorekebisha barabara likiwa limeharibika kutokana na miundombinu mibovu katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
DSC_0553
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael Mshanga (kulia kwa Mkuu wa Mkoa) akitoa ufafanuzi wa matatizo na changamoto za usombaji na utupaji taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
DSC_0560
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akiagana na wakandarasi wa usombaji taka na watendaji wa jiji. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
RIDHIWANI KIKWETE ASHIKA KASI KWENYE KAMPENI ZA UBUNGE WA CHALINZE


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi kumgombea Ubunge jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo wananchi hao walielezwa kitendo cha kuzuiwa kupiga kura ni sawa na ubakaji wa Demokrasia na CCM itakula sambamba na wabakaji wa Demokrasia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndiye Mratibu wa kampeni za mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akionyesha kadi Chadema  iliyorudishwa na Ndugu Subira Mrisho ambaye alikuwa mhamasishaji wa Chadema katika kijiji cha Mkoko,pia katika kata ya Msata Katibu Kata wa Chadema amerejea CCM anaitwa Mrisho Issa pamoja na mwananchama mwingine anayejulikana Kassim Msakamali wamerejea CCM
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
 Mtela Mwampamba akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko na kuwasihi wananchi hao kutambua mahusiano ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi.
 Diwani wa Kata ya Msata akiwahutubia wananchi wa kiji cha Mkoko wakati wa kumtano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kisarawe Ndugu Zena Mgaya akiwa na Shumia Sharif mjumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoka wilaya ya Bagamoyo na pia kiongozi wa kampeni kata ya Msata wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM kijiji cha Mkoko jimbo la Chalinze.
 Wananchi wa kijiji cha Mkoko wakionyesha picha za mgombea wao wa Ubunge Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni ulofanyika kijjini Mkoko.
 Mapokezi ya katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Mkoko.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge ambapo aliwaambia uongozi si kitu cha kujaribiwa hivyo wananchi wakapige kura kwenye chama kilichokuwa na uzoefu wa siasa na maendeleo kwa jumla.
 Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kihangaiko wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.

Kikundi cha Upendo kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM