Monday, March 24, 2014

BARABARA ZA MKATA -HANDENI NA KOROGWE – HANDENI MKOANI TANGA ZAFUNGULIWA NA MHE. RAIS DK. JAKAYA KIKWETE

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye koti jeusi katikati) akiwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa mkoa wa Tanga wakishiriki kuifungua rasmi barabara ya Handeni – Mkata na Handeni - Korogwe huko mkoani Tanga.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyenyoosha mkono) akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anayempongeza kiongozi wa kikundi cha ngoma ya Selo baada ya kutumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mkata – Handeni - Korogwe. Anayeangalia (kulia) ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Handeni Dkt. Abdallah Kigoda. 

TAMASHA LA BAGAMOYO MARATHON LAZINDULIWA

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel (kushoto) akishikana mikono na Mkurugrenzi wa Kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman baada ya kuzindua  Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo Wilayani  Bagamoyo, Pwani .  Anayeangalia ni,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 4Beli, Deogratius Soka (kulia) akisoma hotuba wakati wa uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.













No comments:

Post a Comment